Awekewa moyo wa plastiki

Mshume Kiyate

JF-Expert Member
Feb 27, 2011
6,766
894
Madaktari nchi nchini Uingereza wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kumwekea binadamu moyo wa plasitiki unaondeshwa na nguvu ya betri.
Matthew Green (40), amewekewa moyo huo wa plasitiki katika Hospitali ya Papworth kwenye Mji wa Cambrige na aliruhusiwa kurejea nyumbani na moyo huo, akisema umerejeshwa upya uhai wake.
Akionyesha furaha mbele ya wanahabari, Matthew ambaye ni baba wa mtoto mmoja alisema Ni ajabu kwangu, moyo wa plasitiki umenirudishia uhai, sasa najisikia vizuri mwenye afya na maisha mema.
Kwa mujibu wa madaktari Matthew analazimika kutembea na mkoba ulio na betri zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu zinazofanya kazi ya kuendesha moyo huo usambaze damu mwilini.
SOURCE: BBC NEWS
 
Tanzania sijui wangeweka nini! Sijaele vice versa ya moyo wa plastic sijajua. Nakumbuka ya kichwa na miguu.
 
Naona hawa wazungu wanaMbeep Mungu sasa!
Papworth-e1312391448417-480x345.jpg
 
Nasikia hata moyo wa kitimoto huwa unamfaa sana mwanadamu. Kwa nini hawakumwekea huo?
 
Hawezi kudumu muda mrefu kutokana na sababu za kibaiologia, ila wenzetu ni daring katika sayansi kwa hiyo mtu ku volunteer ili atumike kwa experiments huwa sio tatizo sana.
 
Huyu jamaa aliowekewa huo moyo Matthew alizua taharuki katika mkutano wake na wanahabari, baada ya kengele maalumu iliyounganishwa kwenye moyo wake kulia.
Ilimfanya Matthew naye kushtuka na kukatiza mazungumzo yake na wanahabari kabla ya kengele hiyo kunyamaza baada kupunguza msukumo wa damu kwa kupumzika.
Lakini muda mfupi baadae alisema. Hiyo inanikumbusha niwe makini kila wakati, kama nikipata mshutuko hata kidogo moyo huu hautaki kabisa
 
Back
Top Bottom