Avuliwa Nguo Kwa Kushindwa Kumlipa Dereva Taksi Ujerumani

Dr. Chapa Kiuno

JF-Expert Member
Sep 11, 2009
443
18
September 30, 2009

Msafiri mmoja wa nchini Ujerumani alilazimika kujisitiri kwa kutumia magazeti kwenye uwanja wa ndege wa Munich baada ya dereva taksi kumvua nguo zake zote kwa kushindwa kumlipa pesa kamili. Frank E. (46) toka mji wa Leipzig ilibidi ajisitiri kwa kutumia magazeti baada ya dereva taksi kumvua nguo zake zote pamoja na kumnyang'anya mali zake alizokuwa nazo kwa kushindwa kutoa malipo kamili ya safari yake.

Akiongea na gazeti la Bild la Ujerumani, Frank alisema kwamba alikodisha taksi imchukue toka kwenye kumbi moja ya starehe mjini Munich kumpeleka uwanja wa ndege wa Munich kuwahi ndege iliyokuwa ikirudi mji wa Leipzig mapema asubuhi ya siku iliyofuatia.

Lakini kizaazaa kilianza walipofika uwanja wa ndege wa Munich na Frank kutakiwa na dereva taksi alipe euro 64.20 wakati mfukoni alikuwa na euro 60 tu.

Dereva taksi alimwambia Frank lazima alipe euro 4.20 zilizopungua.

"Alininyang'anya simu yangu, mawani na funguo zangu na kisha kunilazimisha nivue nguo zangu zote mpaka nguo ya ndani", alisema Frank.

Frank alishushwa kwenye taksi hiyo akiwa mtupu hana nguo hata moja na ilibidi wafanya usafi kwenye uwanja huo wa ndege huo wampe magazeti ajisitiri.

Frank aliripoti tukio hilo kwenye kituo cha polisi kilichopo kwenye uwanja wa ndege huo na alipewa kaptula na fulana ajisitiri na kuendelea na safari yake wakati polisi wakianza kazi ya kumtafuta dereva taksi huyo.

Polisi waliripoti jana kwamba hadi sasa bado hawajafanikiwa kumnasa dereva taksi huyo wala kuliona gari lake.

Polisi wanamtafuta dereva taksi huyo kila kona ya Ujerumani na akikamatwa atapandishwa kizimbani kwa kosa la unyang'anyi.
 
Back
Top Bottom