Auwawa na mumewe kwa kuchomwa kisu baada ya kukataa kwenda kuokota embe usiku

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
VILIO simanzi vilitawala katika mazishi ya msichana Khadija Daudi (22), mkazi wa Mbagala Charambe, ambaye aliuawa na mumewe, Sharif Kondo, kwa kuchomwa na kisu mgongoni kwa kile kilichodaiwa kuwa ni baada ya kukataa kuamka usiku kwenda kuokota embe.


Tukio hilo lilitokea baada ya mumewe kumuasha na kumtaka aende nje ya nyumba yao kuokota embe lakini aligoma na kudai kwa kuwa ni usiku asingeweza kwenda nje kufanya kazi hiyo.


Inadaiwa kuwa kutokana na majibu hayo mumewe alikasirika na ndipo alipochukua kisu na kumchoma mgongoni. Baada ya kupiga kelele majirani walijitokeza kumpa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya Temeke.


Hata hivyo, kwa bahati mbaya mwanamke huyo alifariki muda mfupi baada ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Wakizungumza na mwandishi, majirani wa binti huyo wamedai kuwa walisikia kelele za kuomba msaada katika chumba cha mpangaji mwenzao na mara baada ya kuingia ndani kwake kujua kilichotokea ndipo walipokuta kitanda chake kimelowa damu na huku akiugulia maumivu.


Majirani hao wamesema kutokana na hali hiyo walijaribu kumtafuta mumewe lakini hakupatikana ndipo walipokwenda kumwamsha baba mzazi wa mwanamke huyo anayeishi Charambe na kumuelezea yaliyompata binti yake.


Familia ya mwanamke huyo iliungana na majirani kutoa taarifa polisi na kumkimbiza hospitali.


Kwa mujibu wa baba mzazi wa mwanamke huyo, Daudi Rashid, akiwa nyumbani kwake na familia yake walipokea taarifa kuwa binti yao amechomwa kisu na mumewe.


Amedai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 9, mwaka huu, saa 8 usiku nyumbani kwa binti yake Charambe.


Wakati akiugulila maumivu, marehemu alimweleza baba yake kuwa alikuwa akigombana na mumewe mara kwa mara tangu walipooana Machi mwaka huu.


Mzee Daudi anasema yeye binafsi anaona kuwa kilichosababisha wivu wa mapenzi kwa kuwa mwanamume huyo alikuwa hataki kumuona mke wake akiongea na mtu yoyote, awe mwanamume au mke, kwa madai kuwa wanamtongozea kwa wanaume.


“Mimi naona kilichosababisha kifo cha mwanangu ni wivu wa mapenzi.


Siku za hivi karibuni aliwahi kumpiga hadi ujauzito wa miezi sita ukaharibika, hali inayoonesha kuwa kijana huyu si mwema, hivyo naomba Serikali ichukue hatua za kisheria,” alisema Mzee Daudi.


Msichana huyo alizikwa juzi katika makaburi ya Charambe na mtuhumiwa anashikiliwa katika kituo cha Polisi Chang'ombe.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Liberatus Sabasi, ameliambia gazeti hili kuwa mtuhumiwa huyo tayari amekamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo
source :dullonet.com
 
du this is too much now...!! tatizo hakuna sheria kali za kuwatetea wanawake
 
Sio hakuna sheria hiki ni kiashiria kikubwa cha umaskini. Huu sio wivu, kumuamsha mtu usiku kwenda kuchuma maembe ina maana hawakuwa na chakula humo ndani.[/quote]

kweli kabisa, kuna watu bongo msimu huu wa embe wanazila kama lunch na dinner...mimi nimeshaona familia za hivi live pale Chanika kwa sababu ya umasikini
 
janaume pumbavu sana hili

yaami watu wengine ni shida tu
sasa huyu nae kesi itachukua mwaka?
 
Back
Top Bottom