AU's dilemna and the Libyan crisis

Mpevu na mimi ninafikiria hiyo hiyo inanisumbua kichwani! Sio kwamba namuunga mkono Ghadafi kuwauwa raia, hapana lakini je hawa mabwana wakubwa hawawaoni raia wa kisomali wanavyoendelea kuuwawa kwa miaka yote hiyo?
 
Walianza na ukabila haukulipa wakaja na ukanda haukulipa, wakaleta singo ya udini inachuja, sasa wameibuka na uhaini.
 
Wanafiki wakubwa hao. Walikuwa wapi siku zote? Bora wamezuiwa. Wakatatue matatizo yao ya kawaida kwanza kama njaa, Ukimwi, TB, ujinga n.k
 
Musevenis idea

The formation of the committee was informed by President Musevenis proposal that the Libya crisis was an African problem that called for an AU solution with the assistance of the wider international community.

Museveni si ana uzoefu wa ku deal na rebels? AU hawana lolote
 
nimekuja amini kuwa kuna baadhi ya waafrika wana mambo ya ajabu. nikuulize ni wananchi gani wanauliwa je hao wanauliwa wamafenya kosa gani na je wanadai nini?

long live gaddafi fungulia maghala watu wachukue silaha wapambaje na wavamizi

wakichukua silaha, so what??? kuwalaghai wafe wakati yeye akikimbia!!!!!!???? acha hizo, usitetee watu wanaobana demokrasia ya wengi kwa masilahi yao.
 
Lengo la Western kuwakamata kiakili limetimia...bwana mkubwa inama ufikiri,kwanini nchi za kiarabu? Ni mambo mangapi yanafanyika kinyume na utaratibu halisi kwenye nchi zisizo na maslah kwa wamagharibi yanafumbiwa macho? Kwanini unaowaonea huruma wasingeona ubaya wa Gadafi tokea awali...nani yuko nyuma ya haya? Kwa faida ya nani?
Km mtaamua kutumia akili zenu kutafakari mtagundua dhahiri kuna wish huyu bwana anatakiwa kugrant...
 
Mpevu namimi ninafira hiyo hiyo inanisumbua kichwani! Sio kwamba namwunga mkono Ghadafi kuwauwa raia, hapana lakini je hawa mabwana wakubwa hawawaoni raia wa kizomali wanavyoendelea kuuwawa kwa miaka yote hiyo?

Walichukia wa USA, raia wa somalia walipouwa wa Marekani na kuwaburuza mitaani huku wakiwa wamekatwa katwa vichwa; wakati wa USA walikuwa hapo Somalia kuwasaidia misaada ya kibinadamu kipindi cha mapinduzi ya bare!!!! Hiyo iliwafanya waamini wa Somalia siyo watu wanaotaka saidiwa; wanaroho ya kiunyama. Wakawaacha wajitawale wanavyotaka....hali ndo hivyo sasa!!!
 
Mpevu namimi ninafira hiyo hiyo inanisumbua kichwani! Sio kwamba namwunga mkono Ghadafi kuwauwa raia, hapana lakini je hawa mabwana wakubwa hawawaoni raia wa kizomali wanavyoendelea kuuwawa kwa miaka yote hiyo?

Ni kweli usemacho nami nimefatilia kwa karibu siasa za magharibi na jinsi wafanyavyo immediate invasions, Somalia inazaidi ya miongo 2 bila ya serikali madhubuti...na hawajatumia nguvu (?)

Ivory Coast pale kuna ulafi wa madaraka upo wazi tena ni koloni na rafiki wa karibu wa Ufaransa...tayari wameshaanza civil war na raia kuchinjwa pasipo any conducive majors kuchukuliwa kuepusha those killings.
Ikumbukwe ya kuwa nchi nyingi za magharibi hutegemea zaidi kirasilimali Africa na upande wa malighafi hutegemea nchi za ghuba na baadhi ya sehemu nchi za asia.

Hivyo haishangazi sana kwa kitokeacho, wangelijaribu diplomacy na kushindwa...HAPO NINGEUNGA MKONO moja kwa moja millitary invasion yao.
 
Lengo la Western kuwakamata kiakili limetimia...bwana mkubwa inama ufikiri,kwanini nchi za kiarabu? Ni mambo mangapi yanafanyika kinyume na utaratibu halisi kwenye nchi zisizo na maslah kwa wamagharibi yanafumbiwa macho? Kwanini unaowaonea huruma wasingeona ubaya wa Gadafi tokea awali...nani yuko nyuma ya haya? Kwa faida ya nani?
Km mtaamua kutumia akili zenu kutafakari mtagundua dhahiri kuna wish huyu bwana anatakiwa kugrant...
Nimekuja kugundua nafikiri hata wazungu wamegundua wakoloni waliondoka mapema Afrika kabla ya akili zetu kukomaa ndiyo maana wanarudi kutufundisha upya, mimi nasema acha waje.
 
Twende mbele turudi nyuma. Hivi Gadaffi alikuwa akiwashambulia waandamanaji au waasi? Libya kuna waasi walijitenga huko Benghazi na si waandamanaji. Waandamanaji gani wanakuwa na silaha na ndege za kivita? Juzi walenga shabaha wa Yemen wamewalenga waandamanaji na kuua makumi hatujasikia UN ikitoa Azimio!! Azimio la hao UN ni no fly zone lakini Marekani na mabeberu wenzake wanashambulia makazi ya Gadaffi na raia wasio na hatia, huo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu!! Huko Somalia raia wasio na hatia wanauawa kila kukicha lakini Mabeberu wanaangalia tu kwa kuwa hakuna maslahi. Marekani na mabeberu wenzake wanataka ku justify ili waishambulie Iran si vinginevyo. Afrika tusipokuwa makini tutatawaliwa na hao wajua haki za binadamu ambazo nazo zinachagua, Libya na siyo yemen!!
 
Endeleni kuwa worship hao mashetani wa magharibi bado wanatunyatia na sisi tutakuja kumia siku zina hesbau I HATE WESTERN .YAANI KWELI WA LIBYA WANAHITAJI MSAADA KIASI HICHO MHHHHHHHHHH UONGO MKUBWA NI MAFUTA YANAWAPELEKA IPO SIKU YAO .IMSIJIFANYE MNATATETEA DEMOCRACY ILA UKWELI UTABAKI KWA SASA WAZUNGU WAMEANDA KUPORA NA SI KUOKOA WALIBYA.
 
Sikutegemea kukuta waafrika wanaendelea kushangilia kinachotokea Libya sasa hivi bali walipaswa kusikitika na kuinamisha vichwa chini wakilia, mnampongeza Obama na sirkozy shame on you! Hamuoni ni jinsi gani wao kwa mashambulio ya siku moja tu wameua raia 64 na majeruhi zaid 100 sasa anaeua raia ni nani Gaddafi au wamarekani?

Af unadiriki kusema wazi kuwa raia hawamtaki Gaddafi ni asilimia ngapi ya raia wote wasiomtaka Gaddafi au ni kikundi cha watu wachache wenye uchu na madaraka wanaosapotiwa na wamagharibi ndo hawamtaki gaddafi, eti wanalinda raia, mbona Palestina kila kukicha Israeli anawauwa watu haendi huko kwalinda, miaka mingapi leo somalia watu wanakufa mbona haendi huko, mbona kongo watu wanakufa haendi huko, vp kuhusu bahrain ambako serikali inawaua waandamanaji na sio waasi na wala hausikii wakisemwa hata kwa maneno nini kupigwa na majeshi, acheni kuwa na fikra finyu huku mkijisifia kuwa wananchama wa jf kisima cha fikra pevu, MKIENDELEA kuwa na mawazo mgando kama hayo hamna haja hata ya kuwepo humu JF ni bora mkaangalie utaratibu mwingine lakini katika hili la libya western countries wana ajenda ya siri kubwa tu nyuma yao ambayo kwa kifupi ni strategic reason.
 
Leo nimeamka nikiwa na furaha manake nilijua walibya wamepata watetezi.

Haiwezekani kutumia mizinga madege mavifaru kashambulia raia wako. Hivi kama Gadafi anaipenda Libya kwa nini asingeondoka kama Misri?

Alimaanisha nini kuwafungua maghala ya silaha wananchi ili kila mtu amiliki silaha?? Namshauri azitumie kupambana na wanaume wenzie wa magharibi.
 
Twende mbele turudi nyuma. Hivi Gadaffi alikuwa akiwashambulia waandamanaji au waasi? Libya kuna waasi walijitenga huko Benghazi na si waandamanaji. Waandamanaji gani wanakuwa na silaha na ndege za kivita? Juzi walenga shabaha wa Yemen wamewalenga waandamanaji na kuua makumi hatujasikia UN ikitoa Azimio!! Azimio la hao UN ni no fly zone lakini Marekani na mabeberu wenzake wanashambulia makazi ya Gadaffi na raia wasio na hatia, huo ni ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu!! Huko Somalia raia wasio na hatia wanauawa kila kukicha lakini Mabeberu wanaangalia tu kwa kuwa hakuna maslahi. Marekani na mabeberu wenzake wanataka ku justify ili waishambulie Iran si vinginevyo. Afrika tusipokuwa makini tutatawaliwa na hao wajua haki za binadamu ambazo nazo zinachagua, Libya na siyo yemen!!

Mkuu tofauti kati ya waandamanaji na waasi au wapigania haki na magaidi inategemea na matakwa na nia ya anayetoa hiyo tafsiri.

Mapinduzi ya Misiri na Tunisia nayo yangeweza kuitwa maasi na waandamanaji kupigwa/kuuawa, lakini baada ya demokrasia kuachwa ifanye kazi maisha/mali yaliyopotea kwenye vuguvugu hilo halikuwa kubwa kutokana na watawala wa nchi hizo kuyachukulia kama harakati za kisheria za wananchi wa nchi zile kuchagua utawala na watawala wanaowataka, Libya wale wale waliokuwa wanaitwa wapigania haki walibadirishwa jina na kuitwa waasi ili kukidhi matakwa ya watawala na kuweza kuwapa justification ya kuwashambulia kwa mitutu kama maadaui wao!

AMUKA!
 
These folks are foolish.. They waited for final call to back up Gaddaffi..but it is too late though.
 
Back
Top Bottom