Auawa nje ya ubalozi wa Marekani, Ubalozi watangaza kufunga huduma zake leo

UPDATE

NAIROBI, KENYA: Ubalozi wa Marekani umeamua kuufunga kwa leo ubalozi wake kufuatia kisa ambapo mwanaume aliyekuwa na kisu alijaribu kumshambulia afisa wa usalama karibu na ubalozi huo jana Alhamisi.

Imearifiwa kuwa mwanamume huyo aliuawa kwa kupigwa risasi na hakuna afisa yeyote wa ubalozi huo aliyeathiriwa na kisa hicho.

“Ubalozi utafungwa Oktoba 28. Huduma zote za kibalozi zimesitishwa, lakini huduma za kibalozi za dharura kwa raia wa Marekani zitaendelea kutolewa,” Taarifa hiyo imetolewa kwenye tovuti ya ubalozi huo.

Maafisa wa ubalozi huo wametoa wito kwa raia na wafanyakazi wake kuwa makini kuhusu usalama wao.

Polisi nchini Kenya wanachunguza kubaini iwapo mwanamume huyo aliyepigwa risasi alikuwa na washirika, afisa mmoja mkuu wa polisi Vitalis Otieno aliambia Shirika la Habari la AFP.

Bw Otieno alisema mwanamume huyo alimdunga kisu afisa mmoja wa polisi lakini akapigwa risasi na kichwani na kuuawa na afisa aliyekuwa karibu.

Maafisa watano wa idara ya uchunguzi wa jinai ya Marekani (FBI) walifika eneo la tukio muda mfupi baadaye pamoja na polisi wa Kenya kufanya uchunguzi.

Msemaji wa polisi Kenya George Kinoti alisema mwanamume huyo wa miaka 24 alikuwa “mhalifu wa kuendesha shughuli zake kivyake”, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Hata hivyo, alisema uchunguzi unaendelea.

View attachment 425455

Mwanaume mmoja anayehisiwa kuwa wa kikundi cha Alshabaab ameuawa nje ya Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi baada ya kumshambulia mlinzi mmoja kwa kumchoma na kisu.

Inadaiwa mwanaume huyo alikuwa akijaribu kuingia kwa lazima kwenye ubalozi huo.

===========================================

A suspected Al-Shabaab terrorist was on Thursday shot dead after he stabbed a General Service Unit (GSU) officer at the heavily guarded US Embassy in Gigiri, Nairobi.

"The US Embassy confirms there was a shooting incident near the Embassy. No Embassy personnel were involved. We refer you to Kenyan authorities for further details," said a statement from the embassy.

The suspect, it is reported, was trying to forcibly gain entry into the embassy when he was blocked by the Kenyan officer at the gate.

The attacker stabbed the GSU officer on the head and right hand before the officer gunned him down.

Dressed in a dark blue jeans and grey sweat-shirt, he pretended to be passing by the Visa section gate when he attacked the officer.

Gigiri OCPD Vitalis Otieno said the suspect hails from Wajir County but could not give his name.

An eye witness said he saw the man attack the officer to ground and that the officer, however, managed to shoot and kill his attacker.

Investigations into the incident were taken over by five detectives from the Federal Bureau of Investigations (FBI) who collected samples and exhibits, including his blood samples.

Detectives said the suspect had no mobile phone but had a Safaricom SIM card in his pocket.

Documents found on him indicated that he had reported three cases at the Pangani police station but the OCPD did not give the details.

Security has been beefed up within Gigiri in the last one year following terror threats. Last month, Education Cabinet Secretary Fred Matiang’i directed the Kenya Technical Trainers College to be relocated to the former Kenya Science College along Ngong Road in a move seen as having been prompted by the security concerns.

Detectives are yet to establish the motive of the suspect who wanted to disarm the officer.

A senior police officer said he could be a lone-wolf terrorist, who commits violent acts alone, outside of any command structure and without material assistance from any group.


Source: Daily Nation
 
Acheni uzushi, je kuna kitu gani kinaonesha ni gaidi??? Mbona huyo anaonekana ni mpita njia tu ambaye kauliwa. Inasikitisha sana kama tutauana kwa kisingizio cha muonekano. Ifikie pahala tuaminiane.
Hicho kisu alkua amebeba cha nin? Angefanikiwa kufanya uovu wake nadhan ungekua WA Kwanza kulaum mamlaka za usalama
 
Hicho
Acheni uzushi, je kuna kitu gani kinaonesha ni gaidi??? Mbona huyo anaonekana ni mpita njia tu ambaye kauliwa. Inasikitisha sana kama tutauana kwa kisingizio cha muonekano. Ifikie pahala tuaminiane.
Hicho kisu alichokua nacho ni cha kukatia nini ubalozini?
We ni mpuuuzi sana... Very useless
 
Wee una uhakika gani na aliyeuwawa alikuwa gaidi? Au kwasababu hapo umewaona fbi? Dah
Ukisoma maandiko hapo juu wanasema alimvamia afisa mmojawapo kwa kisu akitaka kumchoma. Pitia upya hii thread kuanzia pale mwanzo.
 
Back
Top Bottom