Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Klabu Atletico Madrid ya Hispania imejichomoza mwaka huu wa ligi 2013/2014 kama timu ya ushindani na inayotaka kubeba makombe. Ikiwa chini ya Diego Simeone,kiungo wa zamani wa Argentina, Atletico imeonyesha kuiva na kuimarika kwake katika kusakata kandanda la nguvu,kasi,ufundi na ushindi.
Sasa inakabiliwa na fainali mbili.Ya kwanza ni ya La Liga.Ikiwa inaongoza kwa alama 89 na huku Barcelona ikifuatia kwa alama 86,Atletico itahitaji sare ya iana yoyote au ushindi dhidi ya Barcelona hapo tarehe 17/5/2014 katika uwanja wa Camp Nou ili kutwaa ubingwa wa La Liga. Ikifungwa,Barcelona itatwaa ubingwa kwakuwa ina uwiano mzuri kuliko Atletico katika mabao ya kufunga.
Fainali ya pili itacheza mnamo tarehe 24/5/2014 katika jiji la Lisboni,Ureno.Itakuwa ni fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.Katika mechi hii,Atletico itahitaji ushindi kutwaa kombe hilo la vilabu bingwa Barani Ulaya. Atletico itajaribu kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia yake.
Katika fainali zake mbili,Atletico anapambana na wababe wa Hispania na Ulaya. Atachomoza na kutwaa makombe yote au hata moja?