Swahilian
JF-Expert Member
- Apr 28, 2009
- 591
- 66
CHUJI
Athumani Idi chuji, mwanasoka Tanzania.
Amejaliwa vipaji, nashindwa kuelezea.
Kakosa tu uchugaji,kondoo wangemezea.
Hiki kipaji cha chuji, ni matatizo makubwa.
Mpira kakomalia, shule hakupendelea.
Mama alikubalia,kandanda we endelea.
Wengi akawavutia ,nyotaye kuongelea.
Hiki kipaji cha soka,au cha kusingizia.
Ikawa chuji na Simba,wafurahi kidedea.
Ukuta kashika nyumba, msimbazi kupepea.
Sokani walikukumba, bado uliwachekea.
Hivi soka ikipanda , akili zenu huruka?
Mara ukaaanza kuponda, sekeseke za chakula.
Ugomvi na wako nyanda, kisa chenu ni Jamila.
Huna raha ukakonda, Simba ikawa madhila.
Hiki kipaji cha Idi, kina wingi wa vituko.
Usajili tafrani, hutaki tena nyumbani.
Wasema huna amani,wataka kwenda jangwani.
Wangangania benchini, nyumba mpya twigani.
Kipaji cha Brambati, sijaona duniani.
Kifungo kikawa mwisho, ukarudi uwanjani.
Tuliona zako jasho, ulijituma dimbani.
Walikwongeza na posho, washinda mwao vinywani.
Athumani wa kipaji, mwige nduguyo Pius
Taifa zima gumzo, madebe ukapigiwa.
Maximo akwite mwanzo, kiungo bora kaitwa.
Ukaanza zako bezo, dole kati likasutwa.
Chuji hiki kipaji, kutukana mashabiki?
Tamati yanigongea ,sifaze nisiandike.
Sisahau ya Songea, yachekesha ya Mwandike.
Soka hawakuchelea, miezi sita wamweke.
Idi kipaji tumia, uhuru sasa tulia.