Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 118,344
- 219,709
Bado haijahamika kama hii ni ALBAKI baada ya ile hasara ya Bil 170 kufidiwa .
Kama unabisha shauri yako .
---
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile amesema baada ya Kampuni ya Ndege ya Air Tanzania(ATCL) kupata hasara ya takribani Tsh. bilioni 170 na kufanya maboresho kadhaa ya usimamizi hatimaye kampuni hiyo imeanza kutengeneza faida ya Tsh. bilioni 1.5 na kuendelea.
“Ruzuku ilikuwa 100% kwenye uendeshaji ambapo Shirika lilikuwa linategemea ruzuku Serikalini kwa 100% leo wanajitegemea kwa 99.6%, madeni yalikuwa zaidi ya Tsh. bilioni 200 leo yamebaki 40%, hasara ilikuwa ni karibu Tsh. bilioni 170 leo tunaanza tengeneza faida ya Tsh. bilioni 1.5 na kuendelea”
Kihenzile amesema hayo Jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao na Menejimenti ya Air Tanzania inayoongozwa na Mkurugenzi Eng. Ladislaus Matindi na kupokea taarifa yao ambapo amewapongeza kwa usimamizi wa Shirika “Serikali chini ya Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaidiwa na Makam wa Rais Dr. Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu Dkt. Dotto Biteko imefanya kazi kubwa sana”