ATCL kuanza direct flights to Mumbai

You better keep quiet if you know nothing my dear. We have a decease called UJUAJI. Same person is a Driver, Police Economist, Teacher and kilakitu. Siyo fair jamani. Acheni watu wafanye kazi zao. Kama wewe ni Mchumi acha mtu wa Mipango nae afanye yake. Mwalimu acha Mlinzi afanye yake. Mhasibu acha daktari afanye kazi yake. Huwezi kufahamu kila kitu ndugu. Mnajiaibisha. Hata wakipata hasara hawatakuwa wa kwanza maana Kenya Airways wanazipata na wanasonga mbele. Acheni ujuaji. Tunawachoka.
Hao ndio timu pingapinga kila kitu kutoka upande wa pili. Kila jambo jema wanapinga tu.
 
Safi sana. Watanzania wengi wanaenda india kwa masomo na matibabu. Itasaidia sana maana safari itakua fupi sio kama ukipanda madege ya ethiopia, oman,dubai,n.k. itabidi uende hizo nchi hivo kuongeza gharama na uchovu wa safari.
Wenye roho za kushindwa kaeni mbali na hii thread.
 
Ni swala zuri sana ila je abiria wapo kiasi gani? Isije kuwa kama KQ walienda wakaamua kupunguza safari maana ndege ilikua yarudi robo.

Afu ni ngumu MTU kuacha Emirates, Qatar na Etihad kupanda ATCL/KQ
Wewe ndiye hujui chochote kwenye air travel. Yaani msafiri anayekuja Tanzania kutoka Mumbai (Bombay), India aache kupanda direct flight, badala yake aende kulala airport Dubai, Abu Dhabi au Doha! Wewe ni bre kabisa!
 
Ni shida sana ndege za moja kwa moja kwenda india, nimeshaenda mara kibao lazima upitie dubai ama abudhabi ni usumbufu sana. Na abiria ni wengi. Nakumbuka nliahirisha safari yangu siku moja ilikiwa saa 12 jioni, baadae nikaresume saa tatu usiku nikaambiwa ndege imejaa ilikuwa direct flight to bangarole
Kweli mkuu muda unaotumia toka Dar kwenda Dubai(masaa matano unusu) unaweza kuta unatosha kukufikisha Mumbai.
Ukifika Dubai unaweza kaa hata masaa saba unasubiri ndege ya Mumbai.
 
Tatizo letu
1. Tuko na mawazo hasi kila wakati hata jema lifanywe tutaliona baya na hiyo imetuathiri mpaka katika maisha yetu ya kawaida mtu akifanya hata jambo zuri tunaponda yaani utafikiri tumerogwa aisee.
2.Maneno mengi mno tunaongea sana vitendo sifuri tubadilike wandugu.Kwani hayo makampuni makubwa kama EMIRATES walianza kila kitu wanaweza? Au ndio vile tunapenda kusifia vya wengine vyetu tunaponda? Vijana tubadilike.
3. Vijana ifike wakati tubadilishe mindset sio kila kitu negative negative tu haitokaa ikatusaidia. Nia aibu kwa kijana kuwa na NEGATIVE ATTITUDE kila wakati utafikiri zuri hata moja hakuna.HATA SHETANI ALIWAHI KUWA MALAIKA.
Yes watanzania wengi sana wana negative attitude kazi kulalamika kwa kila kitu.
Wanaongea sana vitendo sifuri. Bora tumepata rais wa vitendo ili watu watie akili na ulalamishi wao na uzuri anawapaga watu makavu live.
 
ATC wakijitahidi hii ni route nzuri sana. Ni matatizo yetu wenyewe ndiyo yana tusumbua. Abiria wengi hata wa Kenya airways wangependa sana kusafiri na Air Tanzania tatizo tulikuwa hatuna ndege ya kutupeleka huko.
Nakumbuka enzi ya Djibouti Muscat Dubai ATC ilibidi waanzishe route ya Mombasa ili ibebe abiria wa route hizo. Abiria wengi kutoka Mombasa walikuwa transit kuelekea Dubai. Hata Air Malawi wakajiunga wakala joint venture.
Hii route ni nzuri sana tuombe mambo twende vizuri.
Yaani hapo ATcl itasomba hadi wanaoenda Bangalore,Chennai na miji mingine ya India coz wakifika Mumbai abiria wanachukua local flight kwenda mji mwingine.
 
Mimi si mtaalam wa masuala ya anga lakini navoona ndege sahihi ambayo ingepependeza zaid na gharama ndogo ingekuwa bombardier cs 300 kutokana uwezo na pia ndio kwanza tunaanza, pia penetration iwe katika price ndogo tu kwa point kuwa, wasafiri wengi wa hii njia kuwa wale wabahiri.
Uwezo cs
Maximum range 6117 km
Passenger capacity130 into two classes, 160 in one class
Distance ya kutoka DSM mpka Mumbai ni 4905 km ha kuna bakio LA kama km kadhaaa za ujazo
Kwasababu inakuja kabla ya CS300 then baadaye CS300 itaweza kwenda. Lakini pia wataangalia kama abiria wengi wataendelea kutumia 787.
 
Ndio kuna watalii wengi Huko? Tuliambiwa hili dege ni mahususi kwa kuvutia watalii kuja kutembea nchini kwetu, Leo linageuzwa kuwa ambulance, mweee
Kuna chaka tunaingizwa hapa ndg Bujibuji. Hio route waliishindwa Air India na Gulf Air, sisi tutaiweza? Oman air, Etihad, Dubai One, Qatar Airways na Emirates kila mmoja anapeleka midege yake huko na service zao ni world class. Sie tutaweza kweli na catering za Shishy Baby?
 
Kiukweli, binafsi siwezi acha kupanda emirates nikapande atcl. No way. (brand loyalty)

Hii ndege lengo lake ni kuwa "ambulance" kwanini wasingeweka direct route ya guangzhou china inayotumiwa na wafanyabiashara wengi wa kitz?
 
Watalii hawashindwi kuja sababu ya kukosa ndege shida ni Yale makodi waliyoyaweka kwenye utalii,MBONA awamu iliyopita walikuwa wakija wengi sana kuliko awamu hii na kulikuwa hakuna ndege

Tanzania hata kwa Africa haiko kwenye top three countries. Kwa rasilimali zetu inabidi tushindane na France wanaopata watalii zaidi ya 82 millions kila mwaka.

Hata tukipata 20 millions kila mwaka. Wanalipa pesa ya visa, usafiri, Malazi,chakula ni pesa nyingi sana. Kama kila mtalii anatumia 400 USD hapa bongo hiyo ni zaidi ya 10 billionsb USD kila mwaka.

Inabidi tufanye kuwa rahisi watalii kupata visa, tujenge hotels, miundombinu na kufanya JKIA kuwa international hub ya East, Central and Southetn Africa.
 
Sijaponda ila nime-think Critically. Cha muhimu ilikuwa ni kujiimarisha katika route za mikoani na nchi jirani ili ATCL iweze ku-feed Emirates. Juzi imeshuhudiwa Emirates wakifanya utafiti wa JNIA kuweza kuhudumia ndege kubwa kwa kusingizia kuwa hali ya hewa ya Mauritius ilikuwa mbaya. Wale walikuwa kwenye utafiti.
Hakuna utafiti wa kijinga hivyo, pia huwezi kufanya utafiti kwa kujalibu kuland dege la trilion 200, kuituisha kwa kujaribia. Walishatuma ma engineer kufanya study wakadecrale kuwa a380 inaweza kutua. Na ujue kuwalaza abiria siku2 five star hotel ni hasara ujue, ile ndege nishaipanda mara mbili inameza abiria 860. Jiulize kama ilikuwa full mzigo hao wote walale hoteli ya laki3 ni sh ngapi hapo. So before you comment fikiria kwanza
 
You better keep quiet if you know nothing my dear. We have a decease called UJUAJI. Same person is a Driver, Police Economist, Teacher and kilakitu. Siyo fair jamani. Acheni watu wafanye kazi zao. Kama wewe ni Mchumi acha mtu wa Mipango nae afanye yake. Mwalimu acha Mlinzi afanye yake. Mhasibu acha daktari afanye kazi yake. Huwezi kufahamu kila kitu ndugu. Mnajiaibisha. Hata wakipata hasara hawatakuwa wa kwanza maana Kenya Airways wanazipata na wanasonga mbele. Acheni ujuaji. Tunawachoka.
Ndugu yangu tumia kiswahili ili ujumbe ufike vizuri.Unapovurga maneno unapoteza hata maana.Sema DISEASE siyo DECEACE.
 
Tanzania hata kwa Africa haiko kwenye top three countries. Kwa rasilimali zetu inabidi tushindane na France wanaopata watalii zaidi ya 82 millions kila mwaka.

Hata tukipata 20 millions kila mwaka. Wanalipa pesa ya visa, usafiri, Malazi,chakula ni pesa nyingi sana. Kama kila mtalii anatumia 400 USD hapa bongo hiyo ni zaidi ya 10 billionsb USD kila mwaka.

Inabidi tufanye kuwa rahisi watalii kupata visa, tujenge hotels, miundombinu na kufanya JKIA kuwa international hub ya East, Central and Southetn Africa.
Inawezekana kama tutakuwa na nia ya kufanya hivo na kuondoa vikwazo vikwamishavyo biashara ya utalii ikiwemo kodi,kuzuia nchi kuchafuka kimataifa.
 
Ndio kuna watalii wengi Huko? Tuliambiwa hili dege ni mahususi kwa kuvutia watalii kuja kutembea nchini kwetu, Leo linageuzwa kuwa ambulance, mweee
Kidogokidogo. Njia kuombwa kwenda na kutiliana sahihi. Alipokuja PM wa India tulisaini. Wataomba njia subiri Hii sio daladala
 
Back
Top Bottom