Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,896
SALAMU ZA MWAKA MPYA.!
Siku chache baada ya Askofu Zacharia Kakobe wa FGBF kutishiwa na vyombo vya dola baada ya kutoa maoni yake kuhusu imani yake na nchi yake, Mkuu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dr.Frederick Shoo (PhD) amesema Watanzania hivi sasa wanajengewa hofu ili wasiseme ukweli wa kile wanachokiamini.
“Kuna watu wanajaribu kuwajaza wengine hofu ili wasiseme ukweli na wasikae katika kweli. Watu wanajazwa hofu ili wasitetee kile wanachokiona ni cha haki. Watu wanajazwa hofu ili wasiwe huru kutoa mawazo yao kuhusu Kristo. Wengine wanajazwa hofu ili wasiweze kutoa maoni yao kuhusu nchi yao. Na wengine wanapotoa maoni yao kuhusu imani yao wanatishiwa. Hii si sawa. Ni lazima tuikubali kweli. Na tukidumu katika kweli tutakuwa na uhuru wa kusema na kutembea bila woga.” amesema Askofu Shoo.