Uchaguzi 2020 Askofu Mwamakula: Ninakwenda katika msafara wa Lissu pamoja na uwezekano wa kupigwa mawe au kurushiwa mabomu na risasi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,015
NINAKWENDA KATIKA MSAFARA WA LISSU PAMOJA NA UWEZEKANO WA KUPIGWA MAWE AU KURUSHIWA MABOMU NA RISASI!

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi lilizuia Msafara wa Mheshimiwa Lissu eneo la Kiluvya jijini Dar es Salaam pasipo sababu za msingi kwani kama kungelikuwa na ukiukwaji wa taratibu za Kampeni basi Tume ingelimchukulia hatua. Nilipokwenda kumuona, Polisi waliokuwa na silaha walinitisha wakitaka kunizua nisiende kumuona Lissu. Kilikuwa ni kituko cha aina yake! Utamzuiaje kwa kumtisha Askofu huru katika nchi huru ili kumkataza kumuona raia huru katika mazingira huru? Walilenga kuficha nini kwa Askofu na kwa jumuiya ya kimataifa? Watu wengi hawajui kuwa Askofu ni jicho pia la Jumuiya ya Kimataifa katika nchi ye yote ile. Vitisho na zuio lao hata hivyo havikufanikiwa!

Jana tarehe 13 Oktoba 2020, nilipata muda wa kuongea kwa simu na baadhi ya walinzi wa Lissu baada ya kupata taarifa kuhusu shambulio dhidi ya Mheshimiwa Lissu kule Chato! Mmoja alikuwa ana maumivu makali katika bega baada ya kurushiwa mawe. Niliarifiwa kuwa watu kadhaa waliumizwa katika tukio lile.

Bado tunajiuliza maswali mengi kuhusu vurugu za Chato na Geita kwa ujumla dhidi ya Mheshimiwa Lissu. Hivi inakuwaje Mgombea Urais kufanyiwa chuki na vurugu kubwa kama zile nyumbani kwa Rais? Hivi ni nani na nini kilichokuwa nyuma ya hayo yote? Je, ni wivu, uhuni, chuki, wivu, au ukabila? Hiki ni kiashirio gani katika eneo ambalo asilimia kubwa ya wakazi wake ni Wakristo? Viongozi wakuu wa Kanisa katika Mkoa wa Geita wamelichukuliaje jambo hilo?

Tangu kampeni zianze, Lissu na Mgombea Mwenza wake wamekuwa wakilengwa kwa vurugu dhidi yao kutoka kwa makundi yanayoandaliwa kimkakati. Kama hilo halitoshi, manyanyaso kutoka Jeshi la Polisi katika baadhi ya maeneo na mikakati ya Tume kuengua Wagombea wa CHADEMA na ACT Wazalendo vimetumika kama mbinu ya kudhoofisha na kuhujumu upinzani katika Uchaguzi huu. Hii si HAKI hata kidogo.

Kama Askofu ninakemea vitendo hivyo na ninaomba viongozi wote wa dini tukiwa kama sauti ya maadili nchini tuungane katika kuonya na kukemea uovu huu na uporaji wa haki nchini.

Pamoja na vitisho hivyo, nipo njiani kwenda katika Msafara wa Mheshimiwa Lissu. Haki huinua taifa!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

+Emmmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.
 
Sauti ya mtumishi huyu wa Mungu ni sauti ya Mungu mwenyewe. Sauti ya wengi ni sauti pia ya Mungu, kwa kila aina visa na vitimbwi wanayomfanyia Tundu Lissu ndiyo ambavyo inazidi kumfanya kuwa imara na kumjengea umaarufu zaidi.

Uchaguzi huu ni "replica" ya mpambano kati ya mfalme Sauli na Daudi. Mmoja ijapokuwa yupo madarakani, lakini Mungu amemkataa, lakini mwingine ndiye mpakwa mafuta wa BWANA. Hongera sana askofu Mwamakula kwa kusimamia upande sahihi wa maono ya Mungu wetu Muumba.
 
Sauti ya mtumishi huyu wa Mungu ni sauti ya Mungu mwenyewe. Sauti ya wengi ni sauti pia ya Mungu, kwa kila aina visa na vitimbwi wanayomfanyia Tundu Lissu ndiyo ambavyo inazidi kumfanya kuwa imara na kumjengea umaarufu zaidi...
Mimi naona ni mapambano kati ya Musa na farao. Hebu tuone kama historia itajirudia
 
Askofu amejijengea heshima kwa kuendelea kuihubiri haki kwa vitendo, abarikiwe sana.

Wengine wanashindwa hata kutoa kauli tu za kukemea hayo matendo ya kihuni anayofanyiwa Lissu, wanatakiwa kuona aibu sasa, wajue dunia inawatazama.
 
Hii hali inanikumbushia nchini Kenya mwaka 1991 wakipigania kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Ilikuwa ni hatari sana polisi walikuwa busy wakipiga watu kama mbwa huku raia wengine wakifungwa jela na utawala wa kikatili wa marehemu Daniel arap Moi.

Ilibidi viongozi wa kidini waungane na wanaharakati na wanasiasa kujitoa sadaka ili kuurejesha mfumo wa vyama vingi huku wakisaidiwa na aliyekuwa balozi wa Marekani nchini humo Bw. Smith Hempston.

Baadaye Moi alikubali yaishe na kuachia mfumo wa vyama vingi urejeshwe japo kwa gharama kubwa, sasa hiyo hali ndio leo tunayo katika Tanzania chini ya Magufuli japo sio katika kupigania mfumo wa vyama vingi lkn kudai uchaguzi wa haki.

Kuondoa udikteta ni kazi ngumu sana ambayo inahitaji roho ngumu sana, udikteta haujawahi kushinda wananchi wanaopigania haki yao popote pale duniani historia inatufundisha hivyo.
 
Sauti ya mtumishi huyu wa Mungu ni sauti ya Mungu mwenyewe. Sauti ya wengi ni sauti pia ya Mungu, kwa kila aina visa na vitimbwi wanayomfanyia Tundu Lissu ndiyo ambavyo inazidi kumfanya kuwa imara na kumjengea umaarufu zaidi...
Hakika.historia ya Mfalme Sauli na Daudi .ni haha yanayo fanyika leo Tz.Dau alipata kibali Cha Mungu.Sauli alikuwa anapoteza mvuto siku Hadi siku.Sawa na Rais wa sasa
 
Da Haijawahi kutokea katika nchi yetu.
Hofu mashaka wasiwasi na taharuki ya Hali ya juu Sana.
Chaguzi zote Wakati wa Mkapa na Kikwete haikua hivi.
Utadhani nchi iko vitani yaani.
Mashaka na Hofu hizi mwanzilishi wake anafahamika kuwa ndiye aliyetakiwa kuzizuia Bali yeye anazianzisha na kuzisimamia.

Serikali inawezaje kuwafanyia Wananchi wake uharamia halafu bado iendelee kuwa halali?Nchi ya Amani huku ikinyima Haki watu wake!
Tubadili maisha yetu kwa kuwakataa hawa maharamia.
 
Back
Top Bottom