Askofu Mwamakula: Mheshimiwa Rais asipewe utukufu wa Mungu!

Kuna Yule RC wa Iringa aliisema
"HAKUNA na hasifananishwe na kiumbe/mtu yeyote labda MUNGU TU"
kwa manaa Nyingine halisema wamfananishe na Mungu

Hawa viongozi huwa wanajisahau Sana
na kwa unafiki wa viongozi wa dini.
Jumapili utakuta akienda kusali watamchekea Tu.na kumsafisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Na bashite naye alishawai kujiita yeye ni mungu wa dar es salaam na akaenda mbali zaidi na kudai Mungu hana nafasi tena kwenye dunia hii
 
N
Mfalme Herode Agripa I alikuwa ni mjukuu wa Mfalme Herode Mkuu. Alipanda ngazi hadi kuwa mtawala wa Galilaya, Samaria, na Uyahudi. Alitawala eneo kubwa sana na alikuwa na madaraka makubwa sana akimwakilisha Mfalme wa Kirumi. Baada ya mgogoro wa muda mrefu na Nchi za Tiro na Sidoni (Lebanoni ya sasa), Mfalme Herode alikwenda Kaisaria (Ikulu) na kupanga siku ya kukutana na watu wa Tiro na Sidoni kwa ajili ya mapatano. Katibu Kiongozi wa wakati ule aliyeitwa Blastus ndiye aliyefanikisha kuitisha mkutano ule.

Ilipofika siku yenyewe ambayo pia ilikuwa siku ya Kumbukumbu ya Kaisari Claudiusi, Mfalme Herode alivalia mavazi yake ya kifalme yenye gharama na fahari kuu. Alitoa hotuba nzuri sana iliyomaliza mgogoro na kuwaunganisha watu. Wasaidizi wake walimsifia sana kwa hotuba ile sambamba na watu wote walioisikia. Wapambe wake walikwenda mbali mno kwa kusema sauti au hotuba ile (ya Herode) haikuwa ya mwanadamu bali ilikuwa ni sauti ya Mungu. Kwa maneno mengine walikuwa wanasema kuwa Herode hakuwa binadamu wa kawaida bali alikuwa ni Mungu! Herode aliposikia vile alifurahi sana kufananishwa na Mungu. Biblia inaeleza kuwa 'malaika wa Bwana alimpiga pale pale na akafa kwa kuwa hakumpa Mungu utukufu! Mwanahistoria maarufu wa Kiyahudi aliyeitwa Josephus anaeleza kuwa Herode alipatwa na maumivu makali, alikufa baada ya siku tano. Huo ulikuwa Mwaka 44 BK. Mfalme Herode ndiye aliyemuua Mtume Yakobo na pia alijitahidi kutaka kumuua Mtume Petro bila mafanikio. Unaweza pia kusoma zaidi kuhusu kisa cha Mfalme Herode Agripa I katika Matendo ya Mitume 12: 18 - 25

Leo nilistuka, nilishangaa, na niliogopa sana nilipoiona 'recorded clip' moja ikisambaa mitandaoni ikimuonyesha kiongozi mmoja ambaye pamoja na mambo mengine, amesikika akimtaka au akimuomba Mungu ili amshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri....!

Inawezekana kiongozi yule alisema maneno yale kwa mihemko au hisia tu! Lakini tunaaswa sote kuwa tunapofikia kutaja jina la Mungu yatupasa tufikiri na tujichunguze. Wapambe wa Herode walimponza Herode kwa kauli zao za kumlinganisha na Mungu! Herode naye aliponzeka kwa kupenda sifa na kulewa sifa zile. Badala ya kumrudishia Mungu utukufu alikubali kuubeba utukufu ule!

Mheshimiwa Rais Magufuli anajua kuwa hakushinda kiti cha Urais kwa uweza wake mwenyewe! Maana mara kadhaa amesikika akisema kuwa hakutoa hata rushwa ili kupata Urais. Kwa hiyo anajua fika kuwa Mungu ndiye aliyeruhusu yeye awe Rais. Kama ni hivyo, basi Mheshimiwa Rais pamoja na wateule wake wote wanatakiwa wamshukuru Mungu kwa kazi ye yote wanayoiona kuwa ni nzuri iliyofanywa na Rais. Sio Mungu ndio amshukuru Rais kwa kazi iliyofanywa na Rais kwa ajili ya Watanzania. Pia, na sisi wengine kama kuna kazi nzuri tunayoiona kuwa imefanywa na Mheshimiwa Rais, basi tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha Rais kuifanya hiyo kazi, siyo sisi kumtaka au kumuomba Mungu ili amshukuru Rais!

Kama viongozi wa Kanisa, na Kanisa kama mwili wa Kristo hatuwezi kunyamaza kimya tunaposikia kauli zinazoelekea kuchukua utukufu wa Mungu! Kwa kuwa tunawapenda hawa viongozi na tunawaombea, tunao wajibu wa kuwaambia na kuwakumbusha kuhusu nafasi ya Mungu. Tuna imani pia kuwa kwa kuwa Mheshimiwa Rais, anajua ukuu na utukufu wa Mungu atawakumbusha na kuwaonya wateule wake ili wawe makini wawapo majukwaani wasije wakautwaa utukufu wa Mungu na kumpa yeye (Mheshimiwa Rais)!

Ninaomba rehema kwa kiongozi husika na watu wengine wa namna yake ili Mungu awasamehe na ili asiwahesabie dhambi hii. Ninaomba pia Mungu awape neema ya kujua ukosefu huo na awape neema ya kuomba toba na rehema wao wenyewe kwa vinywa vyao. Maombi haya ya rehema na toba yanasindikizwa kwa Neno la Mungu kutoka Isaya 6:1-7.

Sent using Jamii Forums mobile app
NAAM ! MUNGU NI MUNGU MWENYE WIVU! YEYE TU NDIO ASILI YA VITU VYOTE VYENYE KUSTAHILI KUSIFIWA.

PANAPOKUWA NA JAMBO LOLOTE JEMA LENYE KUSTAHIKI SIFA BASI SIFA HIZO ZOTE ZIMWELEKEE MUNGU
 
Heading yako; Unamweleza Askofu asimpe Utukufu Rais!!,ni kwa Namna ipi kauli yako hii!!?,Aliyoyasema MWANRY (SIYO RAIS) unamhusishaje Askofu kumpa Rais Utukufu!!!?,mwisho unakwepa Jukumu la kuchunga kondoo kwa Mafundisho kama haya!,bado unamtaka mheshimiwa Rais afanye afanye kazi hiyo!!,TIMIZA WAJIBU WAKO MOJA KWA MOJA KWA MHUSIKA BADALA YA KUMRUSHIA ASKOFU MPIRA MITANDAONI NA MUACHE RAIS WETU ANAKAZI NYINGI AMBAZO NIMEHISI ANAKUKERA!, maana inawezekana SADAKA zimekuwa Chache sikuhiz huko Kanisani kwako Mtumishi!!!:D:D:D
Pole sana!

Pumbavu!
 
Tuwaombee viongozi wetu Mungu awahurumie maana wameamua kumzidi yeye aliyewaumba na wameanza kumpangia majukumu

Umeandika vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama zamani, kakobe na gwajima wangesha pandisha mizuka, Ila baada ya kuubusu mkono wa mfalme hatuta sikia chochote.

USOGA WI KUA KATI MWINA NSONGOO
 
Maisha matamu Ndugu yangu. Kupotea kimya kimya bila kuacha hata alama ya kaburi, inatisha hivyo. Kilangila.
 
Heading yako; Unamweleza Askofu asimpe Utukufu Rais!!,ni kwa Namna ipi kauli yako hii!!?,Aliyoyasema MWANRY (SIYO RAIS) unamhusishaje Askofu kumpa Rais Utukufu!!!?,mwisho unakwepa Jukumu la kuchunga kondoo kwa Mafundisho kama haya!,bado unamtaka mheshimiwa Rais afanye afanye kazi hiyo!!,TIMIZA WAJIBU WAKO MOJA KWA MOJA KWA MHUSIKA BADALA YA KUMRUSHIA ASKOFU MPIRA MITANDAONI NA MUACHE RAIS WETU ANAKAZI NYINGI AMBAZO NIMEHISI ANAKUKERA!, maana inawezekana SADAKA zimekuwa Chache sikuhiz huko Kanisani kwako Mtumishi!!!:D:D:D

Sii kila kitu ni Chadema na Ccm
Shirikisha ubongo wako ipasavyo unapohitajika kuchangia kitu kwenye jamii yako iliyokuzunguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom