Askofu Mwamakula: Awamu ya TANO na ya SITA

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,039
AWAMU YA TANO
Rais John Magufuli: Hakuna Mikutano ya Siasa ya Hadhara! Uchumi wetu umekua sana! Sisi ni matajiri! Tanzania imeingia Uchumi wa Kati! Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni wa Kifisadi! Ni kichaa tu anayeweza kuukubali! Kuna watu wanatumwa na mabeberu!

Spika Ndugai na Wabunge: Atake asitake tutabadilisha Katiba ili Magufuli aendelee kutawala! Tutamlazimisha!

Waziri Kangi Lugola: Magufuli ni kama Yesu!

Mkuu wa Mkoa Mwanri: Mungu tunakuomba utusaidie kumshukuru Rais Magufuli!

Askofu Mwamakula: Msimpe Rais sifa za kupindukia! Nitaongoza Matembezi ya Hiyari kudai Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya!

AWAMU YA SITA
Rais Samia Suluhu: Serikali yangu iko tayari kukosolewa! Fungueni vyombo vya Habari vilivyokuwa vimefungiwa! Msipore Fedha za Wafanyabiashara! Nitazungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa nchini! Serikali inafufua Mazungumzo kuhusu Mradi wa Bandari ya Bagamoyo! Katiba Mpya na Mikutano ya Siasa ya Hadhara visubiri kwanza! Nipeni muda ninyanyue kwanza Uchumi!

Mbunge: Rais Samia atawale hadi 20....!

Waziri Kabudi: Katiba iliyopo ipo imara! Ilitupitisha katika kipindi kigumu!

Mkuu wa Mkoa Chalamila: Mimi nilidhani Rais akiwa madarakani hafi!

Wapinzani: Kama Rais Magufuli alisema Uchumi ulipanda na kufikia Uchumi wa Kati, ni nani kaushusha hadi Rais Samia aombe muda wa kuupandisha tena? Tunataka Katiba Mpya!

Askofu Mwamakula: Adhma ya Kudai Katiba Mpya iko palepale! Gari likikufikisha salama katika safari yako, huwezi kuahirisha mpango wa kununua gari jipya!

Jaji (mstaafu) Werema: Madai ya Katiba Mpya yasipuuzwe!

Askofu Bagonza: Taifa lisilojadili limekufa!

Freeman Mbowe: Tumemuandikia Rais Samia ili tukutane naye! Hajatuita hadi sasa! Sisi hatutabembeleza! Tusipoitwa na Rais kujadili mambo ya msingi tutakutana mitaani!

Tundu Lissu: Katiba ni lazima, iwe kwa Heri au kwa Shari!

BAVICHA: Tunataka Katiba Mpya!

UVCCM: Hatutaki Katiba Mpya!

Zitto Kabwe na ACT Wazalendo: Watoa Tamko!

Wahitimu: Hakuna ajira!

Wafanyakazi: Hatujapandishwa mishara na madaraja kwa muda wa miaka 6.

Mdude: Wembe ule ule!

Kihongosi na UVCCM: Mdude kamtukana Rais....! Hatutakubali!

Vijana wa CHADEMA: Kihongosi na UVCCM wangelimkemea kwanza James Heri....!

Hii ndiyo Tanzania aliyoiacha Nyerere ambayo wastaafu waliambiwa wanyamaze kwa kuwa zama zao zilikwisha kupita. Waliambiwa kuwa kama wakiendelea kuwashwawashwa watatwangwatwangwa! Hii ndiyo Tanzania ambayo wakosoaji waliambiwa ni mbwa wanaobweka!

Pomoja na hayo, sisi tunayo matumaini makubwa kuwa Mungu bado hajalala. Tunaendelea kushauri kuwa katika mazingira kama haya, mazungumzo na maridhiano ndiyo mambo ya msingi kufanyika. Je, ni nani mwenye hekima na ushawishi wa kuwaambia wakubwa kuhusu umuhimu wa Maridhiano katika Taifa? Wajibu wetu tumeutimiza na tunaendelea kuutimiza (Ezekieli 2:1-10).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

EF888A43-C7CE-40CA-AC5D-137169E413A1.jpeg
 
Wanaoenda kuswalishwa na huyo askofu punda wa ngada hawana akili wote.

Askofu haelewi hata kwamba Tanzania iliingia uchumi wa kati mapema zaidi kwa miaka 5.

Askofu haelewi hata kwamba kuna Corona na nchi nyingi zimekumbana na negative economic growth isipokuwa Tanzania.
 
Ingeacha kwanza wajadili wenye akili, wanaoweza kujadili hoja.
 
Mkuu hawa Viongozi wa dini wachache ambao wameamua kujitoa kwenye huu mjadala muhimu kuhusu mustakabali wa nchi yetu wananipa matumaini makubwa sana. Natamani Viongozi wengi wa dini nao wangeshiriki lakini kwa sasa hawa waliopo kwenye huu mjadala muhimu si haba.

Aiseeee !!!
 
Wanaoenda kuswalishwa na huyo askofu punda wa ngada hawana akili wote.

Askofu haelewi hata kwamba Tanzania iliingia uchumi wa kati mapema zaidi kwa miaka 5.

Askofu haelewi hata kwamba kuna Corona na nchi nyingi zimekumbana na negative economic growth isipokuwa Tanzania.
Dawa imekukolea ASKOFU KAWAMBIA UKWELI MTU
 
Wanaoenda kuswalishwa na huyo askofu punda wa ngada hawana akili wote.

Askofu haelewi hata kwamba Tanzania iliingia uchumi wa kati mapema zaidi kwa miaka 5.

Askofu haelewi hata kwamba kuna Corona na nchi nyingi zimekumbana na negative economic growth isipokuwa Tanzania.
Askofu kawanukuu waliosema tumikia Akili
 
Back
Top Bottom