Askofu Malasusa: Msipende umaarufu kupitia misaada

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,816
4,566
1626087474226.png
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki na Pwani (DMP), Dk. Alex Malasusa, amekemea baadhi ya Wakristo nchini wanaotumia njia ya kuwasaidia wahitaji ili kujipatia umaarufu au kukubalika zaidi katika jamii.

Alisema kutenda matendo mema na kuyatumia kama njia ya kujitafutia umaarufu au kukubalika zaidi mbele ya jamii ni jambo ambalo halikubaliki mbele ya Mungu.

Dk. Malasusa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua harambee ya kuchangia ujenzi wa Chuo cha Ufundi kwa wenye ulemavu wa akili kwa vituo vya Udiakonia vilivyopo Mtoni Mtongani, uzinduzi uliofanyika katika Usharika wa Boko, Kinondoni, Dar es Salaam.

Alisema ipo tabia kwa baadhi ya watu makanisani ambao hupitia kusaidia wenye uhitaji ili wajulikane zaidi kwenye jamii. "Wakristo wanahitaji kutenda matendo mema na siyo kuyatumia kama kitu cha kuwafanya wajulikane zaidi au kukubalika katika jamii, wapo wachache makanisani ambao wakitoa wanataka wajulikane," alisema Dk. Malasusa.

"Mtumikieni Mungu kwa kusaidia wahitaji na iwe kama tabia, toa au saidia na ikiwezekana hata Askofu wako asijue ila Mungu tu ndiye ajue, na watu wa namna hii wanaopenda kujulikana wanaposaidia ndiyo wale wanaoangalia sadaka kama kodi, na wanapotoa wanamuangalia mchungaji na siyo Mungu, hauwezi kusema unampenda Mungu kama husaidii wahitaji."

"Na kutenda mema siyo kwa matajiri tu ni kwa kila mtu na hii ni tabia binafsi na ndiyo maana kunapotokea harambee kama hizi watu wanaalika tu wale wenye kampuni, kumtolea Mungu au kumsaidia mwenye uhitaji hakuhitaji tajiri tu, huu ni moyo wa mtu ambaye anatoa kile alichonacho kwa ukamilifu."

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu huduma za jamii, kutoka katika kituo cha Udiakonia KKKT Mtoni Mtongani, wilayani Temeke, Agnes Lema, alisema ujenzi wa chuo hicho kwa ajili ya vijana wenye ulemavu wa akili utasaidia kuongeza nafasi za kupata elimu bora kwa watoto wenye ulemavu huo wa akili.

"Wazo la kuwa na chuo hiki cha ufundi kwa wenye ulemavu lilikuja baada ya kushuhudia vilio vya miaka mingi kutoka kwa wazazi na watoto pindi wanapomaliza muda wa kukaa kwenye kituo chetu cha Mtoni na wengine walikuwa wakikataa kuondoka," alisema Lema.
 
Namfahamu mwanasiasa aliahidi kuchanga ujenzi wa Kanisa na hakutoa chochote licha ya kupigiwa makofi.

Alipofuatwa alisema, "Ilikuwa lazima niseme, si unajua tena.....!"

Nikajua hana Roho wa Mungu ndani yake.
 
Huyu nae ni TAKATAKA
 
Waluteri wa Tanzania amkeni. Malasussa analipasua kabisa vioande kwa wivu wake tu dhidi ya watu ambao wana upako.

Yeye alipoteza mvuto baada ya kuwa wakala wa Dikteta Magufuli
 
Back
Top Bottom