Askofu Dkt. Shoo: Mbowe alikuwa mbunge wangu na nimekuwa naye karibu sijawahi kuona tabia ya ugaidi kwake, nitashangaa sana!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,230
146,643
Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi

Askofu Shoo amesema haki itendeke katika kesi hii ambayo inafuatiliwa na watu wenye mapenzi mema duniani kote.

Dr Shoo amesema haya kwenye mazishi ya mama mkwe wa Freeman Mbowe amnapo aliongoza misa ya mazishi.

Mungu ni mwema wakati wote!
 
Utetezi wa kijinga sana,rohoni kwa mtu ni mbali sana,askofu aache upuuzi,dola ina mkono mrefu sana
Haya maaskofu ndio huwa yanasema chaguo la Mungu nk,yule Aliyekuwa anatawala kwa mabavu alikuwa hamtaji Mungu?

Makonda je si alikuwa analia hadi kanisani? Kwani wazinzi na wala rushwa kwa mfano huwa hawamtaji Mungu makanisani na misikitini? Anazeeka vibaya.
 
Alichokisema Askofu Shoo ni sahihi kabisa. Haiwezekani Mbowe leo akawa gaidi wakati ameishi akilinda amani.
Ugaidi ni matokeo ya tabia na mwenendo wa kikatili dhidi ya binadamu wengine, haiwezekani mtu akawa gaidi na jamii inayomzunguka isijue hilo.
 
Jamani, tangu lini suala la mtu kuwa gaidi linapaswa kufanyia mikutano kwamba mimi nataka kuwa Gaidi? Si ni siri ya mtu?
 
Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi

Askofu Shoo amesema haki itendeke katika kesi hii ambayo inafuatiliwa na watu wenye mapenzi mema duniani kote.

Dr Shoo amesema haya kwenye mazishi ya mama mkwe wa Freeman Mbowe amnapo aliongoza misa ya mazishi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Mbowe si gaidi
 
Kama dau la kufanikisha matukio ya kigaidi hapa nchini ni Tsh 600,000/- basi wasiwasi wa Askofu Shoo utakuwa ni wenye kutiliwa shaka. Vinginevyo ni hakika ya kwamba Jeshi la Polisi nchini litakuwa na makamanda wa hovyo sana.

Na endapo mahakama itashindwa kumtia hatiani Mh. Mbowe kwa kosa la ugaidi, basi jeshi hili litapaswa kupuuzwa sana. Na hapo ndipo maneno ya hekima ya Askofu yatakapo thibitika.
 
Hata sisi tungeshangaa endapo usingemtetea ndugu yako.

Shoo na vyombo vya dola nani mwenye jukumu la ulinzi na usalama? Nani huwa wanachunguza hayo mambo?

Huyu anaingilia mahakamani sasa.
Askofu mkuu wa KKKT Dr Shoo amesema anamfahamu vizuri Freeman Mbowe ambaye amewahi pia kuwa mbunge wake na hakuwahi kuiona tabia ya ugaidi moyoni kwake, hivyo atashangaa sana kama Freeman ni gaidi

Askofu Shoo amesema haki itendeke katika kesi hii ambayo inafuatiliwa na watu wenye mapenzi mema duniani kote.

Dr Shoo amesema haya kwenye mazishi ya mama mkwe wa Freeman Mbowe amnapo aliongoza misa ya mazishi.

Mungu ni mwema wakati wote!
Mkuu wa Kanisa na siyo Askofu Mkuu.
 
Tabia ya huyo mtu ikoje? ndio yule alietaka maridhiano wakati ule? wacheni utoto wenu.
Maridhiano ya nini, kwani kuna shida gani TZ? TZ wakihitaji maridhiano then Sudan, Ethiopia, Afghan, Iraq, Syria wahitaji nini?
 
Back
Top Bottom