Askari wa usalama barabarani waliopiga picha ya mahaba wakiwa na sare za Polisi wafukuzwa kazi

Aiseee!!! Mbona hao askari wanaonekana kama wako sehemu iliyo nje ya barabara(walikuwa na jenda gani ya ziada) na pili mbona huyo dada anaonekana kama kapakatwa (majanga!!).
Majanga yako wapi mamamdogo? mtu mzima unashangaa wapenzi kupakatana,niPM nikunyanganye cheo cha mama mdogo.
 
Last edited by a moderator:
Tanganyika wamezidi umalaya, Zanzibar ni stara tupu
Mbona mnatun'gan'gania kama ruba,kama tanganyika kuna matatizo?
Tumewapukuta weeee mdondoke hamtaki ndo mnazidi kuhamia k'koo
Kwenu mnajifanya mnazuia ili mje bara kufanya uhuni tuhesabike ni watanganyika,siku zenu zinahesabika.
 
Mmmmmh! ila huyo bint mwenyewe ana hips mzuri jamani!!!
Wameonewa sana,hawa walikuwa wanatangaza utamaduni wetu na kudumisha Mila. Au utamaduni unatangazwa na Nyalandu na Anti Jujuman peke yao tena Marekani.Au yule kijana wa smg Morogoro?
 
Polisi bana...........mwaka huu wamecharuka

images

Acha hizo unataka kumuharibia kazi mama wa watu familia yake itakula kwako? kwanza aliyevaa uniform sie aliye kifua wazi
 
wameoneqa tu kwanini hawajamuadabisha cpt yule wa ccm naye alipigwa picha yuko na dem...kazi kuonea wadogo tu
 
pambav , kazi niliyowatuma hawaifanyi , ndio maana kila wakirudi hesabu iko pungufu ……eti "leo afande hali mbaya" , kumbe haya ndio wanayoyafanya!!.
 
Ama kweli kukaa karibu na mahakama siyo kujua sheria na kutoijua sheria siyo kigezo cha kujitetea mahakamani. ADHABU HII NI KALI KWA HAWA WATOTO; WANGEPEWA ADHABU NYINGINE KWELI WAMEKOSEA LAKINI YAPO TAYARI MAKOSA YANAYOFANYA NA BAADHI YA MAAFISA HAWA AMBAYO NI HATARI KWA USALAMA KULIKO HAYA LAKINI NI KUHAMISHWA KAMA ADHABU YAKE TU. Mwezi Mei mwaka huu kuna maafisa wa kituo fulani hapa walikamatwa na madawa ya kulevya pamoja na Viroba wakivitoa Burundi tena mbaya zaidi wakitumia Gari ya serikali (ya kituo hicho cha polisi) lakini mkuu wa amehamishiwa mwanza na dereva kapelekwa Wilaya mpya ya Buhigwe na mwingine Karya kigoma kusini mwambao wa ziwa Tanganyika.

Pia hapa huenda huyu mpiga picha - Fadhili alikuwa na uadui na binti yangu - Veronica au kijana - Mpaji maana si vizuri kwa mtu mnaefanya naye kazi kama rafiki yako kuweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii pasipo ruhusa yake. Tena mbaya zaidi picha ya namna hii. Hata kama Jeshi lisingingilia kisheria alikusudia kutenganisha ndoa yake.

Mwanangu huyu na Mpaji wamevunja sheria kushindwa kuvumiliana mpaka mwisho wa kazi kama wamezidiwa heri wangesingizia wanaumwa matumbo (Kuharisha) kama asili ya watz - uongo kisha wakafanye hayo pasipo kuvaa jezi hilo. Hapo tatizo ni kufanya kitendo hicho wakiwa wamevaa mavazi hayo.

Ndg Mkuu wa polisi naomba wasamehe kwa hilo hawatarudia tena na kama ni fundisho wamejifunza. Hapo juu awaliosababisha mgonjwa kufariki dunia kwa kutafuta makosa WAO WAMEHAMISHWA LAKINI WAMEUA.

Na nyie watoto zangu tambueni baba yenu ni masikini sikusoma na sifahamiki kwa wakubwa mkifanya makosa hamna wa kuwatetea.
 
Mbona mnatun'gan'gania kama ruba,kama tanganyika kuna matatizo?
Tumewapukuta weeee mdondoke hamtaki ndo mnazidi kuhamia k'koo
Kwenu mnajifanya mnazuia ili mje bara kufanya uhuni tuhesabike ni watanganyika,siku zenu zinahesabika.

Wanaon'gan'gania ni wahafidhina wa CCM ambao maslahi yao yapo Tanganyika, majority ya Wazanzibar hawana shida na Tanganyika. Ngoja utaona mziki mpya wa kuidai Zanzibar endapo CCM mutapitisha katiba yenu ya chama cha mapinduzi.
 
Mbona mnatun'gan'gania kama ruba,kama tanganyika kuna matatizo?
Tumewapukuta weeee mdondoke hamtaki ndo mnazidi kuhamia k'koo
Kwenu mnajifanya mnazuia ili mje bara kufanya uhuni tuhesabike ni watanganyika,siku zenu zinahesabika.

Unauliza nini? aliyelia ni mzanzibar ambaye Sitta alimpigisha kura ya NDIO bila mwenyewe kuwepo bungeni na kutokupiga kura kwa nji yeyote ile. Safari mpya itaanza kuidai Zanzibar tunagoja tuone matokeo kama chama cha mapinduzi italazimisha kupitisha katiba yake kwa mtutu wa bunduki.
 
mbona wengi tu tena wakubwa wanafanya hayo?
ila kwa ushauri watanzania tujiheshimu sanq siku hizi kila mtu ni mwandishi wa habari na mitandao ya jamii ni muda mfupi tu picha zinafika
 
...

Pia hapa huenda huyu mpiga picha - Fadhili alikuwa na uadui na binti yangu - Veronica au kijana - Mpaji maana si vizuri kwa mtu mnaefanya naye kazi kama rafiki yako kuweka picha yake kwenye mitandao ya kijamii pasipo ruhusa yake. Tena mbaya zaidi picha ya namna hii. Hata kama Jeshi lisingingilia kisheria alikusudia kutenganisha ndoa yake.

...

Hivi kwani aliewapiga ndie alieposti mtandaoni? Kuna ushahidi wa hilo? Kuna nyakati simu inaharibika au kompyuta unapeleka kwa fundi na anadowload yako ya siri inakua balaa. Udhibiti wa faragha zetu unahitajika sana nyakati hizi za uhuru wa mitandao ya kijamii.

Halafu kwa posts zilizopita, inaelekea huyu mdada kashapata shida sana na hicho kiungo chake adhimu. Kama vile alizalishwa akiwa form four... na sasa kibarua kimeota nyasi. Wala shetani si wa kusingiziwa hapo.

Wengi wanatetea kwa kufananisha na makosa ya wakubwa zao au wanasiasa. Iko hivi, ukikamatwa jitetee mwenyewe. Huwezi sema uliiba kwa kuwa Mjusi, Banjoo na Massawe ni wezi na hawajakamatwa. Wallah hutapona adhabu...
Hivi mbona hatuletewi picha za wakubwa wa Polisi wakifanya vituko? Kwa anaesema nao ni wakosaji, azilete zao halafu tuone kama hawatawajibishwa!
 
mbona wengi tu tena wakubwa wanafanya hayo? ...

Mkuu, natamani hizo picha za hao wakubwa wa polisi zianikwe ili tuone kama hawatawajibishwa. Kwa zile za wanasiasa, labda maadili yao ni tofauti na polisi na ndio maana walihalalishaga rushwa kwa kuiita takrima.
 
Inaelekea hujui umuhimu wa kucha zako na meno kama Ulimboka.
 
Back
Top Bottom