Askari wa TANAPA apotelea porini, ahofiwa kuuawa na wafugaji na kuzikwa

Hjalte

Member
Oct 20, 2023
25
100
Askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) aliyekuwa akifanya kazi zake katika Hifadhi ya Kigosi iliyoko Kahama, Julius Katambi, anahofiwa kuuawa tangu Ijumaa ya wiki iliyopita (Oktoba 20) usiku, na mwili wake haujapatikana hadi sasa huku juhudi za kuutafuta zikiendelea bila mafanikio.

Askari huyo akiwa Mgambo wawili, wanadaiwa kwenda kukamata mifugo iliyokuwa ndani ya hifadhi hiyo na alipokawakuta wafugaji hao na kukamata mifugo, walimuomba pembeni askari huyo ili "wayamalize" na ndipo askari akiwa silaha ya moto aliitikia wito wa wafugaji hao na kwenda nao faragha, huku wale mgambo wakibaki kulinda Ile mifugo iliyokamatwa.

Baada ya muda, mgambo hao walisikia mlio wa risasi, kwa vile hawakuwa na silaha, walilazimika kukimbia ili kujiokoa na kwenda kutoa taarifa hifadhini ambapo zoezi la kumtafuta lilianza Ijumaa hiyohiyo ya October 20 hadi leo October 26 hakuna mwili wala taarifa za aliko afande Katambi.

TANAPA inaendelea kumtafuta askari wake huyo hadi kwa kutumia ndege ndogo bila mafanikio na haijatoa taarifa yoyote kwa umma kuhusu tukio hilo.

Taarifa zaidi utazipata jamvini hapa.

Screenshot_20231026-083027.jpg
 
baada ya muda, mgambo hao walisikia mlio wa risasi, na kwa vile hawakuwa na silaha, walilazimika kukimbia ili kujiokoa, na kwenda kutoa taarifa hifadhini

Mgambo uchwara hao...

Wamesikia mlio wa risasi pasipo kujua aliyetumia silaha ni nani, lakini wao madai yao mbio zao zilikuwa ni za kujiokoa...

Isijekuwa wao ndio waliochonga mchongo mzima...
 
Askari wa hifadhi ya taifa (Tanapa) aliyekuwa akifanya kazi zake katika hifadhi ya Kigosi iliyoko Kahama, Julius Katambi, anahofiwa kuuawa tangu Ijumaa ya wiki iliyopita (Oktoba 20) usiku, na mwili wake haujapatikana hadi Sasa huku juhudi za kuutafuta zikiendelea bila mafanikio.

Askari huyo akiwa mgambo wawili, wanadaiwa kwenda kukamata mifugo iliyokuwa ndani ya hifadhi hiyo na alipokawakuta wafugaji hao na kukamata mifugo, walimuomba pembeni askari huyo ili "wayamalize" na ndipo askari akiwa silaha ya moto aliitikia wito wa wafugaji hao na kwenda nao faragha, huku wale mgambo wakibaki kulinda Ile mifugo iliyokamatwa, baada ya muda, mgambo hao walisikia mlio wa risasi, na kwa vile hawakuwa na silaha, walilazimika kukimbia ili kujiokoa, na kwenda kutoa taarifa hifadhini ambapo zoezi la kumtafuta lilianza Ijumaa hiyo hiyo ya October 20 hadi leo October 26 hakuna mwili wala taarifa za aliko afande Katambi.

TANAPA inaendelea kumtafuta askari wake huyo hadi kwa kutumia ndege ndogo bila mafanikio na haijatoa taarifa yoyote kwa umma kuhusu tukio hilo.

Taarifa zaidi utazipata jamvini hapa.

Tamaa ya kwenda kupata chochote ukiamini kuwa na silaha basi utaogopwa, maandiko yapo wazi ridhikeni na mishahara yenu.
 
Back
Top Bottom