SACO
JF-Expert Member
- Jul 25, 2011
- 2,321
- 2,914
WANAJESHI SUDAN WAWALINDA WAANDAMANAJI: Askari wa Jeshi la Sudan wamechukua hatua ya kuwalinda waandamanaji mjini Khartoum baada ya vikosi vya usalama kufyatua mabomu ya gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji hao.
Hatua hiyo imekuja kwa mshangao baada ya wanajeshi hao kuyakimbiza magari yaliyokuwa yakifyatua gesi ya kutoa machozi, katika siku ya pili ya waandamanaji waliokusanyika na kumtaka Rais Omar al-Bashir kujiuzulu.
Waandamanaji wamepata hifadhi katika kambi ya askari wa jeshi la wanamaji, ambapo inaoneka wazi kuwepo kwa mgawanyiko miongoni mwa majeshi ya nchi hiyo.
Rais Bashir mpaka sasa amekataa maombi ya kutaka kuwepo kwa serikali ya mpito atakapojiuzulu.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Sudan Tawi la Uingereza, Sara Abdelgalil amesema kilichotokea nchini Algeria kimekuwa chachu ya wananchi wa Sudan kutaka Rais Bashir ajiuzulu kama ilivyotokea kwa Rais Bouteflika wa Algeria.