Askari wa barabarani apokea rushwa live bila woga, abiria wacharuka, dereva awatuliza

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Wadau niko kwenye hiace nasafiri kutoka kigoma kuelekea kibondo.
Tumejazwa kama dagaa kwenye maboksi, gari imepakia mizigo na linakimbia sijawahi kuona, Kinachonishangaza hapa ni kwamba tumeshavipita vituo viwili vya trafic lkn kila tunapofika kwenye vituo hivyo dereva anaenda kusimama mbele zaidi hlf anarudi nyuma anaongea na trafik na safari inaendelea hawa jamaa hawakagui usalama wa gari na abiria hata kidogo tumemuuliza dereva amesema hiyo ni kawaida wao wamezoea.
Nimepanga tukifika kituoni niende kushitaki kwa mkuu wa wilaya au wadau mnasemaje?

Vema kama una simu yenye camera chukua picha ya huyo dereva anapoongea na traffic iwe ushahidi, maana polisi hatakiwa azungumze na dereva kwa siri mbali na gari lake na askari huyo bila hata kuja kuangalia kinachojilia ndani ya gari na wasafiri hali kadhalika usalama wa abiria waliomo ndani ya gari.

Hivi hicho ni kitu cha kuleta hapa jamvini ili kijadiliwe? Kuna umuhimu wa kuuliza kiwango cha elimu cha mtu kabla hajawa member wa JF.

Kaka kama haya mambo ya ku ignore issue hizi za rushwa ndio yametufikisha hapa tulipo leo, nchi imejaa uvundo wa rushwa, kama kuna wazalendo kama hawa wanajitokeza na kuonesha kukera kwao na rushwa, wewe unaona ni wajinga hadi kustahili kutaka kujua elimu yake, napata shuku kidogo kuwa anaestahili kuhojiwa elimu yake ni wewe na wala sio mleta mada. Ni mwisho ujue tu elimu bila busara haina maana, leo hii nchi hii inaongozwa na wasomi lakini wasio na busara na sasa tuko hapa tulipo!

Hivi hicho ni kitu cha kuleta hapa jamvini ili kijadiliwe? Kuna umuhimu wa kuuliza kiwango cha elimu cha mtu kabla hajawa member wa JF.
ni mawazo yako, kujadili kitu chochote ni hiyali ya mtu mwenyewe, hakuna anayekulazimisha ku-comment kwenye thread yoyote. Km wewe unaona suala la rushwa ni dogo sijui ungependa ni mambo gani yaletwe jamvini, angalia mgao wa umeme, matatizo ya mafuta, kupanda kwa gharama za maisha, watu kupokea posho zaid ya moja na mengine mengi km hayo chanzo chake ni rushwa.

Wadau niko kwenye hiace nasafiri kutoka kigoma kuelekea kibondo.
Tumejazwa kama dagaa kwenye maboksi, gari imepakia mizigo na linakimbia sijawahi kuona, Kinachonishangaza hapa ni kwamba tumeshavipita vituo viwili vya trafic lkn kila tunapofika kwenye vituo hivyo dereva anaenda kusimama mbele zaidi hlf anarudi nyuma anaongea na trafik na safari inaendelea hawa jamaa hawakagui usalama wa gari na abiria hata kidogo tumemuuliza dereva amesema hiyo ni kawaida wao wamezoea.
Nimepanga tukifika kituoni niende kushitaki kwa mkuu wa wilaya au wadau mnasemaje?

Huo ni ujinga wenu, mpangwe kama dagaa kwani nyie ni maiti.hamna ufahamu wa kukataa kupangwa, au kama gari unaona limejaa kwanini ung'ang'anie kupanda.

Unaongea tu kwa sababu hujui shida ya usafiri mikoani. Utapanda gari mwanzoni level seat, lakini kila baada ya hatua watasimama na kujaza abiria wapendavyo huku traffic wakipewa kitu kidogo na kuruhusu gari liendelee na safari wakafie mbele.

Utamu wa ngoma ingia ucheze. Hawa wanaoshangaa hawajui taabu ya usafiri. Lakini, mbona hata Dar watu wanajazwa kama dagaa kwaenye daladala hasa wakati wa peak. Palipo na shida, kuna mengi.

Hivi hicho ni kitu cha kuleta hapa jamvini ili kijadiliwe? Kuna umuhimu wa kuuliza kiwango cha elimu cha mtu kabla hajawa member wa JF.
mie nilijua ukiandika kiingereza chako ndo huwa unacomments pumba,kumba hata ukiandika kiswahili ni pumba pia!!!! uwe unaishia kusoma tu si lazima utoe maoni. aaaaaaaaaargh!!!!!!!!!!

Mara nyingi ni sisi wenyewe tunalazimisha kupanda kwenye Magari ambayo yameshajaa. Dereva na Konda wake ni wafanya biashara, wao wanachojali ni Mshiko tu, na Askari wetu ndio kama tunavyowajuwa tena!!!!!!!

Hivi hicho ni kitu cha kuleta hapa jamvini ili kijadiliwe? Kuna umuhimu wa kuuliza kiwango cha elimu cha mtu kabla hajawa member wa JF.

We kaka mbona unawaangusha watu wa Musoma wewe? Unadhani elimu ndio kila kitu mdogo wangu? Kwanza ili uite mtu msomi unaanzia wapi? La saba? Form 4? Form 6? Diploma? Degree moja? masters? PHD? Degree mbili zote bachelor? Master moja jumlisha Diploma au una kigezo gani unatumia?

kwani kuna mtu kakulazimisha uchangie au hata usome tu? Si usome vile vyako ulivyozoea vya vya jokes, chat, MMU na mambo ya wakubwa?

Hivi hicho ni kitu cha kuleta hapa jamvini ili kijadiliwe? Kuna umuhimu wa kuuliza kiwango cha elimu cha mtu kabla hajawa member wa JF.

Tupo member ambao tumeishia darasa la tano lakini tuna comments zenye tija kuliko wewe msomi unaechangia pumba kila upitapo. Doesnt matter how educated you are, what you do whth your education counts the most.

Back
Top Bottom