Askari Traffic na Taa za Barabarani

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Wakati barabara ya Maendela taa hazijawashwa, askari traffic walikuwa hawaongozi magari kwenye mataa. Kila siku pale uhasibu/kilwa rd kulikuwa kunatokea ajali mara kwa mara the same na pale Chang'ombe. Hivi sasa taa zimewashwa askari ndo wako kimbelembele kuongoza magari. Hivi askari wanapata ''raha'' gani kuongoza magari?. Maana utaona mchana wa jua kali au mvua inanyesha askari anaongoza magari! kwanini wasiache taa ziongoze magari.

Hivi sasa askari ndo chanzo cha foleni kwa sababu hawawezi kubalance kuita magari toka kila upande. Wazo la askari kuongoza magari lilikuwa zuri wakati ule msongamano wa magari ulikuwa unakuwa kwa baadhi ya barabara lakini hivi sasa msongamano ni kila barabara na kila upande....hivyo huna haja ya kuwa na askari. Mfano pale Ubungo mataa pande zote kuna magari sawa acha taa ifanye fair kuliko askari.

Ushauri mwingine malori barabara ya Mandela yaaanze kutoka bandarini saa tatu usiku itasaidia sana kupunguza foleni....halafu vitengo vya Bandarini wafanye kazi masaa 24 au angalau hadi sanaa sita usiku....itasaidia sana kupunguza foleni
 
Mkuu wazo lako zuri sana lakini hao Askari watakula wapi ikiwa hawapo kwenye matta?
hapo sio panapopatikana kulaaaaaa
 
Hii nchi unadhani hata ukipiga kelele na kutoa mawazo hivyo wahusika watakusikiliza!
 
Mida ya saa sita jamaa kamporomoshea matusi ya nguoni askari pale mataa ya Ubungo kwa kuyasahau kabisa magari yanotokea Mandela RD....askari kajibaraguza kujidai anaita wenzie walifuatiliea hilo gari la mtukana matusi...
 
Ndugu Mleta mada Nakuunga Mkono kwa asilimia 250% Hakuna kitu kinachoniudhi kama uwepo wa hawa madubwana kwenye maungio (Junction ya barabara) Hawa wamekuwa ndio kero na mwanzo wa usumbufu Mkubwa!! Fikiria Mtu anatumia utashi Binafsi Kuongoza Magari!! Je ndio lengo la sayansi na Technologia litatufikia? ? Mtu anaweza kuongoza na kuwa Biased na kuchelewesha upande Mmoja Hadi Dakika 20!! Hii ni kawaida kwa pale Ubungo Mataa!! Njia ya sum Nujoma inakuwa kama haina umuhimu kwani waweza kucheleweshwa hadi Dakika 20 bila sababu Yoyote!!

Mimi nawaomba hawa polisi wawepo kuamasisha watu kuheshimu Taa na sio Kutuletea hizi kero zote!!
 
Back
Top Bottom