Priva mella
Member
- Oct 31, 2012
- 81
- 28
Hali isiyo ya kawaida polisi wa kituo kikuu cha Rombo wasababisha kifo cha kijana Massawe katika maeneo ya rombo baada yakuombwa rushwa ya Tsh laki tatu kwa lengo la wao kumsamehe kumpeleka kituoni cha polisi, kijana huyo alikamatwa akiwa na mbao ambazo zimekatazwa kuvumwa kwa kipindi hiki, bwana Massawe aliwaeleza askari kwamba anazo laki mbili nyumbani, askari hao waliongozana na kijana huyo hadi nyumbani na kijana huyo aliwapatia laki mbili askari hao walikataa ikampelekea kijana huyo kunywa sumu mbele ya askari hao, juhudi binafsi zilifanyika na baadhi ya watu kuenda ofisi ya takukuru wilaya na leo itafanyika paredi ya askari wote kwa lengo la mke wa masawe kuweza kuwatambua, mazishi yenyewe yatafanyika kesho tarehe 23.11.2012, Wito wangu Kwa jeshi la Polisi hasa kwa Saidi Mwema vijana wako wanakuharibia kazi, angalia vijana tusiidai damu ya ndugu yetu polisi lifuatilieni kwa ukaribu jambo hili.