asilimia 94 ya Watanzania hawanawi mikono

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ASILIMIA nne hadi sita ya Watanzania ndio wanaodaiwa kujua kunawa mikono kabla na baada ya kula huku kundi kubwa likionekana kutokujali kabisa afya zao, ilielezwa.Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando wakati akikabidhi choo kwa mshindi wa shindano la ‘fyatua choo na ushinde’.

Dk Mmbando alisema idadi kubwa ya Watanzania yaani zaidi ya asilimia 94 hawana mazoea ya kunawa kabla ya kula na baada ya kula jambo ambalo ni hatari sana katika afya zao.

Alisema ingawa kwa Waafrika wengi hilo limekuwa ni tatizo, lakini kwa Watanzania linakuwa ni tatizo sugu ambalo linatakiwa kushughulikiwa kwa kila mtu kubadili tabia yake katika kuijali afya yake na familia yake.
Mkurugenzi huyo alisema kama kila mmoja atamua kwa dhati katika kuanzisha mapambano juu ya afya yake hakuna jambo ambalo linaweza kushindikana.

Katika zoezi hilo ambalo alimkabidhi choo chenye thamani ya zaidi ya Sh 22 milioni Fatuma Ally, Mmbando aliwataka Watanzania kujenga tabia ya kutumia vyoo na si kuvijenga na kuvitelekeza.
Alisema wengi wamekuwa wakijenga vyoo vyao, lakini badala ya kuvitumia kwa kazi inayokusudiwa wamekuwa hawavitumia na matokeo yake vinabaki kama urembo wa nyumba.

Mtaalamu huyo wa afya alilaani pia kitendo cha madereva wa magari makubwa wanaopenda kusimamisha magari yao maporini kwa mtindo wa kuchimba dawa na kusema kuwa wanahatarisha afya za wasafiri wao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), Judina Mtenga aliahidi kumsaidia Fatuma tanki la maji lenye ujazo wa lita 3,000 ili choo hicho chenye matundu manane kianze kutumika hata kabla ya maji hayajafika katika eneo hilo.

Fatuma alijengewa choo hicho kwa ajili ya kukifanyia biashara kati ya makubaliano yake na Manispaa ya Dodoma katika eneo linakotarajiwa kujengwa Soko la Kisasa katika Kata ya Chang’ombe na kwamba uongozi wa Manispaa kupitia kwa Naibu Meya Jumanne Ngede uliahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali ili kuuweka mji huo katika hali ya usafi.
 
ASILIMIA nne hadi sita ya Watanzania ndio wanaodaiwa kujua kunawa mikono kabla na baada ya kula huku kundi kubwa likionekana kutokujali kabisa afya zao, ilielezwa.Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkurugenzi wa Idara ya Kinga katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Donan Mmbando wakati akikabidhi choo kwa mshindi wa shindano la ‘fyatua choo na ushinde'.

Dk Mmbando alisema idadi kubwa ya Watanzania yaani zaidi ya asilimia 94 hawana mazoea ya kunawa kabla ya kula na baada ya kula jambo ambalo ni hatari sana katika afya zao.

Alisema ingawa kwa Waafrika wengi hilo limekuwa ni tatizo, lakini kwa Watanzania linakuwa ni tatizo sugu ambalo linatakiwa kushughulikiwa kwa kila mtu kubadili tabia yake katika kuijali afya yake na familia yake.
Mkurugenzi huyo alisema kama kila mmoja atamua kwa dhati katika kuanzisha mapambano juu ya afya yake hakuna jambo ambalo linaweza kushindikana.

Katika zoezi hilo ambalo alimkabidhi choo chenye thamani ya zaidi ya Sh 22 milioni Fatuma Ally, Mmbando aliwataka Watanzania kujenga tabia ya kutumia vyoo na si kuvijenga na kuvitelekeza.
Alisema wengi wamekuwa wakijenga vyoo vyao, lakini badala ya kuvitumia kwa kazi inayokusudiwa wamekuwa hawavitumia na matokeo yake vinabaki kama urembo wa nyumba.

Mtaalamu huyo wa afya alilaani pia kitendo cha madereva wa magari makubwa wanaopenda kusimamisha magari yao maporini kwa mtindo wa kuchimba dawa na kusema kuwa wanahatarisha afya za wasafiri wao.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef), Judina Mtenga aliahidi kumsaidia Fatuma tanki la maji lenye ujazo wa lita 3,000 ili choo hicho chenye matundu manane kianze kutumika hata kabla ya maji hayajafika katika eneo hilo.

Fatuma alijengewa choo hicho kwa ajili ya kukifanyia biashara kati ya makubaliano yake na Manispaa ya Dodoma katika eneo linakotarajiwa kujengwa Soko la Kisasa katika Kata ya Chang'ombe na kwamba uongozi wa Manispaa kupitia kwa Naibu Meya Jumanne Ngede uliahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali ili kuuweka mji huo katika hali ya usafi.
Habari hii haina utafiti.
Kweli kuna watu wanakula bila kunawa , na hawanawi baaa ya kula, lakini si kwa asilimia hizo...94%??!
 
Mhh sidhani kama wanafika wengi hivyo ila wapo!Unakuta mtu anatoka chooni hanawi alafu dkk tano baadae anakula tena bila wasiwasi!
 
Mb ona tunaona mpaka huku vyuo watu wakikuta mnagonga ugali nao wanaingia tu kwenda kunawa mkono anafikiri atachelewa au watu watamuwahi kushusha mzigo!
 
mmmhh hii ni ngumu kuamini 94%..??????????????????
duuuhh mkuu hii number ni kubwa sana yaani.
 
Nakubaliana na hili watanzania ni wavivi!!(?) kunawa mara kwa mara hasa linapokuja swala la kula vitu kama matunda,karanga,mihogo hata dawa na vingine vidogovidogo lakini vinakwenda tumboni.Tukumbuke kupeana mikono,matumizi ya ATM,simu nk vinaweza kuifanya mikono kua michafu sio kwenda chooni tu.
 
Mb ona tunaona mpaka huku vyuo watu wakikuta mnagonga ugali nao wanaingia tu kwenda kunawa mkono anafikiri atachelewa au watu watamuwahi kushusha mzigo!
Hatari kweli!Ndo maana mi nashauri kila mtu kupewa sahani yake!Kwa style hiyo kama mnashare hata alienawa atapata uchafu wa asienawa!
 
kwa tuliokulia familia za kisocialist kwa mtu kupewa sahani yake ni kosa kubwa sana kwani linatengwa sinia kubwa na bakuli kubwa moja ya mboga na huruhusiwi kuchukua nyama mpaka mkubwa aanze wanasema kila mmoja akijipakulia mboga ya kwake na msosi wa kwake kuna watu wanakua hawashibi na mboga haitotosha!
 
Kwa watoto ni sawa kwasababu wanakua directed kunawa mikono kabla ya kuanza kula..tena mara nyingi kila mtu ananawishwa pale pale mezani!!
 
mkuu tatizo linakua wote mnanawa kwenye bakuli moja la kunawia!sasa hapo mnakua mmesolve nini?
 
Kama hii habari ni ya kweli, basi asilimia 94% pia walipaswa waugue kipindupindu!! Kama si kipindupindu basi ni typhoid, safura, minyoo nk.

Tatizo letu kubwa ni Malaria, ambalo halina shida ya kutokunawa mikono.
 
mkuu tatizo linakua wote mnanawa kwenye bakuli moja la kunawia!sasa hapo mnakua mmesolve nini?

Hahahaha hiyo kali nyingine..unatoa uchafu kwa uchafu!Ustaarabu ni kua na mabakuli mawili..moja la maji masafi na lingine la kukingia machafu!
 
"Mtaalamu huyo wa afya alilaani pia kitendo cha madereva wa magari makubwa wanaopenda kusimamisha magari yao maporini kwa mtindo wa kuchimba dawa na kusema kuwa wanahatarisha afya za wasafiri wao"

Sasa kwa hili lakuchimba dawa tunafanyaje?
 
Nitakubali iwapo utasema asilimia 94 ya watanzania hawanawi mikono wanapomaliza kujisaidia.
 
Sijui wamefanyaje utafiti wao ingawa najua kuna ukweli hapo. Halafu na tulivyo na tabia ya kujisaidia hovyo hovyo vichakani...mweh!
 
Back
Top Bottom