Asanteni wana JF

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,990
Ni muda kiasi japo si sana tangu nipate msiba wakumpoteza baba, nimepita katika majonzi na huzuni kubwa ambayo si rahisi kuielezea kwa maandishi.

Mwanzo nilipopata msiba nilikua nasita sita kutoa taatifa huku JF, moyo ulikua unaniambia sema ila kuna ka sauti kakawa kananiambia "usiseme"

Mwisho nikaona acha niseme tu, Basi nikawapa taarifa kama nilivyofanya. Kusema ukweli huu ni msiba wangu wa kwanza tangu dunia iumbwe ambao umetokea katka familia yangu ukanitingisha.

Nilipata bahati wazazi wangu wote walikua hai mpaka hivi karibuni Mungu alipoamua mchukua mmoja, kwahiyo sikuwahi elewa hata msiba ni nini, maumivu yako vipi, nilikua najua tu ukifiwa "unaumia" lakini sikuweza hisi wala otea yatakua ni maumivu ya aina gani.

Baba aliponiacha ndio nikaelewa Huwa inakuaga vipi mtu akisema "kafiwa" si na mzazi tu ila na mtu wake yeyote wa karibu, Hakika ni maumivu yasiosimulika na kuzoeleka, sijui kama yanazoeleka, sijui.

Nimepita kipindi ambacho nikiona mtu anacheka natamani ningekua ndio mimi nacheka, nikimuona mtu ana smile naona kama ni maajabu ya karne, lakini ndivyo ilivyokua kilikua ni kipindi changu cha Maumivu na Kilio na wala si cha kila mtu.

Katika kipindi hiki nimejua nani rafiki wa kweli, nimejua nani ndugu wa kweli, nimejua wanafki, nimejua kila aina ya watu wanaonizunguka.

Msiba huu umenisaidia kujua watu wanaonizunguka wapoje,wananichukuliaje,wananionaje nk.

JF ni mtandao mkubwa sana, niseme ukweli toka moyoni Wana JF mmenipa nguvu sana, wana JF mmenipa faraja kubwa kubwa kubwa.

Sikuwahi fikiria kama inbox yangu ya JF kuna siku naweza ikuta inasoma 500+ Unread Msg sikuwahi fikiri...

Kila msg nikifungua ni POLE POLE POLE POLE... kila mahali ni pole ni pole ni pole.

JF ina ID hazipo kbsa ktk comment ila watu wanazitumia niliziona hizo ID mpka nikashangaa "huyu kanijulia wapi" Asee Guys asanteni sana.

Mmenifuta machozi, Mmenifanya nijione mtu katika watu, nimeona thamani yangu humu JF nimeigundua kwakweli, sikuwahi fikiri nina thamani kiasi gani sikuwahi kabisa.

Lakini kupitia msiba huu nimeona thamani yangu, Asanteni wana JF woteee mlionipa Pole kwenye Thread na mliokuja INBOX asanteni woteeee kwa ujumla wenu.

Nimekaa nikasema nimjibu kila alienitumia inbox msg yapole hakika sitoweza kwa siku moja ila nitatoa tu asante kwa kila alienitumia POLE kwa njia ya msg nitatoa tu

kwasasa naomba tu nitoe asante kwa wna JAMII FORUM wote wote wote...

Asante kwa uongozi, Asante kwa kila kitu sina maneno mepesi yakuweza toa shukurani zangu , sina kwakweli..

ila nataka mfahamu kwamba CONTROLA amejisikia amani na faraja sana kwa namna mlivyokua mkinipa pole.

Nilivyokua msibani nilikua nashika simu naingia nasoma namna watu wananipa pole nilikua najiskia faraja, nilijiona kama nipo msibani na wana JF hakika ni jambo linalotia nguvu sana hasa watu wanapoacha kila wanalofanya na kuchukua muda wao kukufariji. ASANTENI na Mungu alie juu awabariki Mno.

Nimerudi Salama na Nina afya njema, Naanza upya tena Maisha ndio haya haya.

Sina uwezo wa kugawa pesa kwa kila mwana JF ila nina uwezo wa kuwamegea siri za mafanikio na namna ambazo kila mtu ataweza zitumia kujikwamua kiuchumi.

Yes,nipo hapa JF kwa lengo 1 tu kuinua kila alietayari kuinuka kupitia maandishi nitakayokua nayaandika.

Nawapenda Jana Leo na Kesho.
 
Pole broo. Binafsi sikupata taarifa hizi za msiba wa Baba. Nikupe pole sana kwa msiba huu mkubwa, and I can feel the pain. Mungu atabaki kuendelea kuwa Mungu hata kama hatajibu sawa na tunavyoomba.
 
KimsingiMwanadamu yupo kwako kwa sababu mbili (1) Ana benefits vipi kwako (2) Kukutumia aendelee kunufaika ni,kuishi kinafiki nafiki,maisha yanataka hivyo
 
Hebu tia neno juu ya tuhuma za Kumtapeli yule dada na kumtishia kumfanyia roho Mbaya.

Hapo ndipo utapata amani.

Anyway, pole sana.
Kwa kweli kabisa katika kutafuta Amani ya roho nlitegemea basi aombe hata msamaha kwa yeyote ambae amewahi kumkwaza kwa namna yoyote Ile ili roho yake ibaki nyeupe Kama theluji lkn mesoma mpk mwisho sijaona. Basi muda apatapo nafasi amcheki mdada yule hata inbobo ayamalize nae ili Mungu aweze muonesha amani katika roho yake.
 
Kwa kweli kabisa katika kutafuta Amani ya roho nlitegemea basi aombe hata msamaha kwa yeyote ambae amewahi kumkwaza kwa namna yoyote Ile ili roho yake ibaki nyeupe Kama theluji lkn mesoma mpk mwisho sijaona. Basi muda apatapo nafasi amcheki mdada yule hata inbobo ayamalize nae ili Mungu aweze muonesha amani katika roho yake.
Nami nikiw nasom nilitegemea aeke kuhusu yule dada lkn naona kimya.
 
Back
Top Bottom