Asante TBC FM: Leo nimeisikia sauti ya Hayati Edward Moringe Sokoine

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
23,914
23,079
Habari za Asubuhi wakuu, hongera kwa maandalizi safi kwa ajili ya sensa na Makazi ya Mwaka huu hapo kesho 23/08/2022.

Leo asubuhi muda kati ya saa mbili mpaka saa tatu. Nina furaha sana, kwa kufanikiwa kusikia sauti ya Hayati E. M. Sokoine kupitia Redio yetu ya Taifa ya TBC FM. Asante sana TBC FM.

Wanajukwaa la JF mtakumbuka niliwahi kuomba kupata audio ama video ya Hayati Sokoine hapa jukwaani. Na ni mwanaJF Mzee Mwanakijiji aliyefanikisha kutuwekea hapa jukwaani video ya Hayati Sokoine. Ninazidi kumshukuru pia mwnaJF huyu.

Ninaomba TBC kupitia Maktaba Yao hiyo iweke utaratibu wa kupata audio ama hotuba hizi ikiwezekana Hata kwa malipo maana kuna gharama za kutunza audio ama video hizi.

Kwa mara nyingine Asante sana TBC FM.
 
Sisi tunaugulia na tozo mkuu wewe unaleta habari za shujaa wetu. Dah umetuumiza zaidi kuliko tozo zenyewe.

Huyo jamaa angelikuwepo sipati picha nchi ingekuwa wapi leo.

Ila tunasema Muda utaamua!
 
Back
Top Bottom