Arusha: Watoto wawili watuhumiwa kumlawiti mdogo wao baada ya baba na mama kuikimbia familia

Shida ni mitandao, simu janja na vibanda vya kuonesha sinema usiku. Watoto wanaona mengi. Kungekuwepo na zuio kama vile kufunga vibanda hivyo, kukataza matumizi ya simu janja kwa watoto na pia vipindi vya tv. Mitandao ukithibiti simu janja hawawezi kuona mambo mabaya
hYo siyo dawa ya kutatua haya matatizo
 
Hayo majamaa mashenz kwel,yaan hayana hata na huruma na mdogo wao,kwanza kwa umri wao huo walipokimbiwa na wazazi walitakiwa kuingia mtaan na kusaka kazi ili waendeleze maisha yao na kumtunza mdogo wao

iNawezekana hata yenyew yameshajikula yachunguzwe
 
Haya matukio yanatokea uswahilini zaidi na sio kwa watoto wa matajiri wanaoishinda kwenye mitanda na television.
Shida ni mitandao, simu janja na vibanda vya kuonesha sinema usiku. Watoto wanaona mengi. Kungekuwepo na zuio kama vile kufunga vibanda hivyo, kukataza matumizi ya simu janja kwa watoto na pia vipindi vya tv. Mitandao ukithibiti simu janja hawawezi kuona mambo mabaya
 
Kamata mama, kamata baba tupa jela maisha....

Watoto wachukuliwe na kulelewa na serikali kupitia vituo vya kulelea yatima.

Serikali ianze kumilikia vituo vya malezi kwa kulea watoto wenye kesi kama hizi, kama tuna hela nyingi za kuiba kwanini tusijenge vituo speacial vya malezi..
 
Wakazi wa Kata ya Muriet, eneo la Barabara ya Nado, mitaa ambayo ni maarufu kwa jina la Muriet au Barabara ya East Afrika Mkoani Arusha, wamelalamikia kitendo cha wazazi wawili (mume na mke) kuwatelekeza watoto wao ambao wamejikuta wakiingia katika matatizo ya kimaadili.

Inaelezwa kuwa Wazazi hao ambao majina yao hayajapatikana walikuwa na mgogoro wa kifamilia, mume akaondoka lakini siku chache baadaye akarejea na wakakubaliana kuwa waendelee kulea Watoto hao licha ya tofauti zao binafsi.

Katika mazingira ambayo haijulikani nini kilitokea, mume alichukua maamuzi ya kuondoka na kutokomea kusikojulikana kisha siku chache baadaye mke naye akaondoka bila kuaga, hivyo wakawaacha watoto wao Gift ambaye inadaiwa ana umri wa miaka 17, George inadaiwa ana umri wa miaka 15 na Jovin ambaye inadaiwa ana umri wa miaka 6 au 7.

Mama wa Watoto akiwa mafichoni akawa anatuma hela kupitia kwa jirani yake ili awape wanaye kwa ajili ya matumizi ya chakula, baada ya siku kadhaa jirani huyo ambaye ni Mwanamke naye akakataa kupokea fedha hizo kwa kile kilichoelezwa kuwa anaogopa kuingia katika matatizo kwa kuonekana anaunga mkono kinachofanywa na mama Watoto aliyekimbia familia.

Wakati anaondoka mama mtu aliacha simu nyingine nyumbani kwake, ndipo akaendelea kuwasiliana nao kwa njia hiyo huku akiwatumia kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya matumizi.

Licha ya kutoonekana wakienda shule, hivi karibuni majirani waliona yule mtoto mdogo akitembea kwa kuchechemea, baada ya kumuuliza tatizo lake akaogopa kusema akiwaambia ametishiwa na kaka zake kuwa akisema watamua.

Majirani wakatumia ushawishi mwingi azungumze, ndipo Mtoto huyo akafichua kuwa amekuwa akiingiliwa kinyume cha maumbile (analawitiwa) na kaka zake kwa zamu.

Kaka zake hao walipoitwa na kubanwa kuhusu kufanya vitendo hivyo wakakana kufanya matukio hayo huku wakionesha kutokuwa tayari kutoa ushirikiano wa kuulizwa maswali zaidi.

Ndipo Balozi wa Mtaa wa Muriet, Zuhura Ally Toto akashirikiana na wananchi wakampeleka Mtoto aliyeathiriwa na ukatili wa ndugu zake hospitali, madaktari wakakataa kutoa huduma hadi wapate PF3 kutoka Polisi.

Baada ya maombi ya Balozi ndipo madaktari wakamfanyia uchunguzi na ikabainika kweli mtoto huyo ameingiliwa, wakasaidia kumpa dawa.

Akifafanua zaidi, Balozi wa Mtaa wa Muriet, Zuhura anasema “Hadi muda huu tunaye huyu mwathirika kwa kuwa tunajua tukimrudisha kule kwa wenzake wanaweza kumfanyia kitu kibaya zaidi, pia hata kiakiri ni wazi hayupo sawa.”

Anaongeza “Tumewasiliana na mama Watoto amekataa kurudi kwa kuwa anadai tunamdanganya ili arudi kisha wanaomdai waweze kumkamata. Tangu tumpe hizo taarifa hapokei tena simu.”

Inadaiwa yule jirani wa awali aliyekuwa akitumiwa hela ili awape Watoto naye alipomjulisha mama mzazi kuhusu tukio la ulawiti, inadaiwa aligoma kurudi kwa kuamini kuwa wanamdanganya ili akirudi akamatwe na wadeni wake.

Kuhusu madeni, inaelezwa kuwa kutokana na madeni ambayo mama huyo anadaiwa, baadhi ya wanaomdai walifika nyumbani kwake na kubeba baadhi ya vitu ikiwemo kitanda, hivyo Watoto hao wamekuwa wakilala chini.

Balozi Zuhura anasema “Tunawasiliana na Mwenyekiti wa Mtaa ili kulifikisha suala hili mbele zaidi kwenye vyombo husika kwa kuwa hakuna ushirikiano kutoka kwa wazazi na hata afya ya akili ya Watoto husika inaonekana haipo sawa.”
Kuna mtu atakuja kusema kulea watoto kwa kuwadekeza ndio kunafanya wawe mashoga (akili za kimaskini sana hizi) akati data zinasugest mashoga wengi wanatokea kwenye mazingira magumu..........
 
Hao watoto huenda waliwaona wazazi wao wananyanduana.
Inasikitisha kwa kweli umasikini ni shiidaa kubwa sana.
Akina mama vikundi vya ajabu ajabu mara vikoba saccos uchwara ni janga katika jamii full stress.
 
Hio mitoto jela inaihusu daah nimeumia sana imemuangamiza mno mdogo wao
 
ifike mahala tuwe sasa jamhuri ianze kuhukumu hata wale wanaoshindwa malezi ya watoto na ikifikia hatua hiyo Serikali inawanyang'anya watoto na kwenda kuwalea kusikojulikana na kuwafunga wazazi maisha au kuwanyonga kabisa.

Mijinga ya namna hii ndio inaleta matatizo yasiyoisha kwenye jamii na kuifanya jamii kupambana na mikwamo kila uchwao.
 
Hao watoto huenda waliwaona wazazi wao wananyanduana.
Inasikitisha kwa kweli umasikini ni shiidaa kubwa sana.
Akina mama vikundi vya ajabu ajabu mara vikoba saccos uchwara ni janga katika jamii full stress.
Hao wala sio kwamba hawajui wanachokifanya,miaka 17 kama anasoma ni form three huko,itakuwa wanatumia makitu yao yale ya Arusha,wapewe kibano na kifungo washenzi sana
 
Miaka 17 na 15 sio watoto na wala kwa kigezo cha wazazi kutokuwepo hao watoto hawana ubinadamu inapaswa wait we either kwenye vyombo vya sheria/ustawi wakanywe
 
Kuna story nilisoma sehemu, matokeo yake alichapwa viboko kadhaa Basi mbakaji alikuwa na umri miaka 17, wakati Kuna magereza ya watoto.
 
Watu kama hawa pamoja na umri wao ni kuwafunga kwenye nguzo na kuwapiga risasi hadharani..huu ni ukatili wa kiwango cha lami.
 
Back
Top Bottom