Arusha: Lema arudishwa mahabusu, kesi yaahirishwa tena

Yaani hakimu anafahamu kuwa wale wanaozuiwa nje ya mahakama wamekwenda kusikiliza kesi ya Lema na hivyo kutoa amri? Labda uwasilishaji ndio mgumu, Napata shida kufahamu hakimu anapata wapi mamlaka ya mambo yanayotokea nje ya korti yake. Kama kuna jambo linalotokea ndani ya korti yake hapo sawa. Nje ya korti? Sijui labda! Mwenye kufahamukwa hakika hakimu aliamuru nini tafadhali anijuze.
Lol....sasa kwani hiyo ndoto ya lema aliota ndani ya court?! Kama mambo yanayotokea nje ya court hayamuhusu hakimu, I'm sure hata hii ya lema haitomuhusu
 
Mhimili mmoja unateua wakuu wa mihimili yote iliyobaki, halafu mnasema mihimili yote Sawa! Acheni siasa, serikali imeeenda sana chini. Jpm alikuwa sahihi
kuwateua si kigezo yakuwaingilia ktk maamuzi yao.viongoz waliopita mbona hawajaingilia,why awamu hi?kwnn ni hi awamu inataka mambo ya kibabe babe kila idara?kuna kitu c bure na mda ni mwalimu mzuri
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna watu wanamvimbisha kichwa Lema wakati mwenzao mambo yake yanamuhatibikia. Tafakari, hizi ni zama zingine brothers!
 
Bado Wakili Kibatala anafafanua hoja anamponda wakili wa serikali.
Mabishano makali ya Kisheria yanaendelea kati ya mawakili wa Lema na wakili wa Serikali.
Kesi ya jinai no 440, 441 inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema imearishwa hadi Tarehe 22-11-2016 siku ya jumanne
Hivyo basi Mh Mbunge kurudishwa tena Magereza


Hii ni Silaha iliyowashinda hata Makaburu SA. Muhimu mhutumiwa kujua kuwa Gereza ni siyo Kaburi.
 
Kuna uhuru wa kumtusi mtu?
kumbuka huyo meya hakumuita Sokwe ila amemfananisha na sokwe.
Lema ana uhuru kwanza kama mbunge. na duniani kote hakuna uhuru unaovunja heshima ya mtu mwengine. kila uhuru lazima uwe na mipaka ndio maana zikawekwa sheria.
Lema anapambana na sheria za nchi alizoshiriki kuzitunga.


Usiweke akili rehani. Kinachozungumzwa ni issue ya haki ya kupewa dhamana na siyo masuala ya Kesi ya Msingi.
 
Mihimili mitatu hakunaga tena Tanzania
TRUE...kwa ndugai wameingiliwa na mdudu mtu maamuzi yote lazima yatoke kwa wazee wa magogoni kupitia agent wao huku kwa mahakama nayo wamezibiti cjui tutapumulia wapi
 
Acha kumsikiliza huyu dikteta uchwara. Ndani ya katiba ya nchi hakuna popote pale ilipoandikwa mhimili unaoteua wakuu wa mihimili iliyobaki basi huo ndiyo wenye nguvu. Acha kukurupuka.

Mhimili mmoja unateua wakuu wa mihimili yote iliyobaki, halafu mnasema mihimili yote Sawa! Acheni siasa, serikali imeeenda sana chini. Jpm alikuwa sahihi
 
Maelezo yapo biased sana.Muda wote umeeleza namna Kibatala "alivyomponda" wakili wa serikali GHAFLA ukarukia kwenye "mabishano makali ya kisheria yanaendelea" halafu unasema kesi imeahirishwa.
Kwenye hayo mabishano makali ya kisheria wakili wa serikali alisemaje?????
Tukifahamu hayo ndio tunaweza kuona kama Lema anaonewa ama la.
 
Kuna watu wanamvimbisha kichwa Lema wakati mwenzao mambo yake yanamuhatibikia. Tafakari, hizi ni zama zingine brothers!
hebu acha kuandika kila linalokujia akilini! Tukikuuliza uwataje unaweza kutupatia majina yao?
 
Ila mimi nashindwa kuwaelewa watu humu ndani,kwa Lema kukamatwa na kunyimwa dhamana sio jambo la haki lakini watu wanafurahi na kushabikia hiki swala.Kama hupendi chama cha mtu usijenge chuki mpaka ukamchukia mtu,hii hali sio nzuri kabisa.Watu tutofautiane kwenye sera na kujinadi lakini sio tufurahie haki na sheria kupinduliwa hivi.Kwasababu what goes around comes around.Kama leo hii chama tawala kikiwa kinavunja sheria kwa makusidi kwakuwa dora wao ndio wanaimiliki,unategemea siku yoyote wakishika nchi chama cha upinzani wataweza kufata haki na sheria?au watataka kulipiza mabaya yote waliokuwa wanafanyiwa ili kuonyesha nawao walikuwa pia wanaumia.Sasa tukifika hapo ndio unaposikia vita na mapigano ya sisi kwa sisi yanaanza.Ushauri tu jamani tufate utawala wa sheria hata kama chama cha upimzani kikiingia madarakani siku yoyote waweze kulithi na kuishi kwenye uongozi uliokuwa umeachwa vizuri.Usimuonee mtu kwakuwa hamfanani mawazo,bali msikilize kisha mjibizane tu kwa hoja,kisha wengi tunawapa kwakuwa ndio demockrasia.Ila tusitukanane na kuchukiana kwasababu ya vyema vyetu.Tumeambiwa uchaguzi uchaguzi umeshaisha na sasa tufanye tu kazi ,sasa mkatae mkubali Lema ndio mbunge wa Arusha sasahivi na serikali yote ya arusha ipo mikononi mwao ,lakini mbona hawaachiwi wafanye kazi kila siku inakuwa shida tu,ukienda kwenye almashauri napo ni mvutano kwanini inakuwa hivyo?Kwasababu tumeanzisha vyama vingi sasa kuwa chama tofauti na CCM isiwe kama umefanya kosa kubwa hapa nchini.Katiba imeruhusu watu kuwa huru lakini viongozi hawataki kutii Katiba.Ni mtazamo tu na maoni yangu,watu umsichue kama negative ni uhuru wa kutoa mawazo tu.
 
Acha kumsikiliza huyu dikteta uchwara. Ndani ya katiba ya nchi hakuna popote pale ilipoandikwa mhimili unaoteua wakuu wa mihimili iliyobaki basi huo ndiyo wenye nguvu. Acha kukurupuka.

Mkuu ni kweli mhimili unaoteua wakuu wa mihimili iliyobaki sio wana nguvu dhid ya mihimili mingine.

Lakin kiuhalisia kama mtu anaweza kukuteua na kukutengua huoni kama inakuwa unafanya kazi chini yake na hasa katika nchi zilizojaa uoga kama yetu

Aliyeteuliwa ana hofu na kibarua chake akienda kinyume na matakwa ya aliyemteua

Watu kama aliyekuwa mwanasheria mkuu wa zanzibar ni wachache sana.Watu wenye kusimamia kile wanachokiamin na ukweli
 
Mimi nilisema hivi vyeo vinavyotafutwa na mahakim na majaji na mapolisi kupitia migongo ya wanasiasa wapinzani ni shida tupu,mtu unajua kabisa huyu ni mbunge hawezi kukimbia lakini kwakuwa unatafuta cheo upandishwe kwa kutumia mgongo wa wengine ni shida na alaaniwe atafutaye cheo kwa kukandamiza haki za watu,majaji ndiyo maana yalikula rushwa ya Escrow.
 
Acha kumsikiliza huyu dikteta uchwara. Ndani ya katiba ya nchi hakuna popote pale ilipoandikwa mhimili unaoteua wakuu wa mihimili iliyobaki basi huo ndiyo wenye nguvu. Acha kukurupuka.
Teh teh vipi umerudi nchini?
 
22-17=5 days akiwa nondo. Safi sana. Siku hiyo isikilizwe kidogo, hafu iahirishwe miezi mitatu. Hadi ajifunze kitu
 
Back
Top Bottom