Arusha kumekucha

Makamuzi

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
1,155
263
Ile habari ya mgomo wa toyo na vifodi arusha umeanza hali ni mbaya wanafunzi wameshindwa kwenda shule,Polisi wanazunguka mji mzima kuzuia uwezekano wa kutokea vurugu, lakini kuna kila hali uwezekano wa vurugu ni mkubwa sana.
 
Nimepitia barabara ya clock tower, daladala zipo za kuhesabu. Frends corner - unga ltd daladala zipo nyingi kidogo.
 
mpilio mandamano tafadhali tujuzane please mda wa kuanza na wapi au sio
 
Inaonekana mgomo upo ila haujafanikiwa sana, daladala zipo chache kuliko kawaida.
 
ile habari ya mgomo wa toyo na vifodi arusha umeanza hali ni mbaya wanafunzi wameshindwa kwenda shule,Polisi wanazunguka mji mzima kuzuia uwezekano wa kutokea vurugu,lakini kuna kila hali uwezekano wa vurugu ni mkubwa sana.
 
jamani hii serikali gani ambayo haisomi hata arama za nyakati sasa tizama watoto washule wanakosa masomo kwa sababu ya mtu mmoja anajiita Zuberi kwa kufanya kazi ya Mkama wa CCM. Mungu wangu nakuomba utuepushe na hii Bengazi ya Tanzania
 
Mkuu mimi nimeona wanafunzi wengi eneo la Sabena lakini hiyo nimeiona ni hali ya kawaida kwani hata usafiri ukiwepo ni kawaida ya wanufunzi kuzagaa vituoni kwa kuwa madereva wa daladala wanaona hasara kuwachukua kipindi cha asubuhi. Kwa jinsi hali nilivyoiona hakutakuwa na vurugu.
 
Mkuu, ina maana wanafunzi peke yao ndo wamekosa usafiri?
Watu wazima waendao makazini wao wamepanda nini?
 
Mkuu, ina maana wanafunzi peke yao ndo wamekosa usafiri?
Watu wazima waendao makazini wao wamepanda nini?
Birigita hali ya usafiri siyo mbaya, ni hao wanafunzi waliozagaa tena ni eneo moja na ukichunguza ni kila siku mida ya asubuhi kutokana na shida ya usafiri utawakuta wamejazana kituoni. Hadi saizi hakuna tukio lisilo la kawaida la kushitusha.
 
nawapa pole sn wanafunzi waliokosa shule na wafanyakazi walioshindwa kwenda kazini VUMILIENI TU MANA TUKO KWENYE MCHAKATO WA KULIKOMBOA TAIFA.
 
nawapa pole sn wanafunzi waliokosa shule na wafanyakazi walioshindwa kwenda kazini VUMILIENI TU MANA TUKO KWENYE MCHAKATO WA KULIKOMBOA TAIFA.

lol..angel, wewe upo ofisini tu unapigwa na kiyoyozi unasema kuwa upo kwenye mchakato?
 
Back
Top Bottom