Arusha: Jeshi la Polisi lamtia mbaroni mtuhumiwa anayedaiwa kumuua Beatrice Minja

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,347
5,571
Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji ya Beatrice James Minja ambayo aliyafanya huko Tarekea Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjro Tarehe 12.11.2023 na mtuhumiwa aliyefanya aliyefanya tukio hilo kukimbia.

Akitoa taarifa hiyo leo kwa vyombo vya Habari Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa baada ya taarifa hizo kufika Jeshi la Polisi lilianza mara moja uchunguzi kumtafuta aliyefanya tukio hilo ambapo mapema leo Disemba 31.12.2023 Jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Mtuhumiwa Lukas Paul Tarimo.

SACP Misime amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa mafichoni huko Kijiji cha Jema kata ya Olondonyosambu Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha.

Aidha amebainisha kuwa baada ya Mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na Mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuuwa wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.

Pia Msemaj wa Jeshi hilo amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na Jeshi la Polisi kitendo kilichopelekea mtuhumiwa wa mauaji kukamatwa huku akiwaomba wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi.

=====

Stori ya Beatrice Minja kuchomwa visu iliandikwa na Malisa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii baada ya kuwa kijana aliyemchoma visu kuendelea na maisha yake kama kawaida bila kuchukuliwa hatua yoyote huku beatrice akipigania uhai wake akiwa anauguzwa na wanawe. Beatrice alifariki dunia tar 27/12/2023 baada ya kukaa siku 42 ICU katika hospitali ya KCMC bila mtuhumiwa huyo kukamatwa.

"Beatrice James Minja (47) mkazi wa Tarakea, Rombo anapigania maisha yake kitandani. Alijeruhiwa kwa kuchomwa visu 25 na Bw. Paul Tarimo ambaye anadaiwa ni mfanyakazi wa Prof. Adolf Mkenda, Mbunge wa Rombo na Waziri wa elimu.

"Beatrice na Paul walikuwa kwenye mahusiano lakini Paul akawa anamtesa kwa vipigo vya mara kwa mara. Amewahi kumpiga mpaka mimba ikatoka. Beatrice alitafuta suluhu kwa muda mrefu bila mafanikio. Hatimaye akaamua kuondoka na kwenda kuanza maisha yake.

"Kabla ya kuondoka Tarimo alimpora Beatrice kiasi cha 10M ambazo zilikuwa mtaji wa biashara pamoja na pesa za ujenzi wa nyumba ya mama yake. Beatrice aliripoti polisi lakini Tarimo hakuwahi kuitwa kuhojiwa.

"Beatrice alipoondoka kwa Tarimo aliacha baadhi ya mali ikiwemo nguruwe wakubwa 6 na vitoto 11. Baada ya Beatrice kuondoka Tarimo alienda kwenye banda na kukatakata nguruwe wote pamoja na vitoto. Bado polisi hawakufanya lolote.

"Tarehe 13/11/2023 saa 12 jioni Beatrice akiwa na akina mama wengine wawili, walishambuliwa na Tarimo, ambaye alimkwida Beatrice na kumchoma jumla ya visu 25 maeneo mbalimbali ya mwili wake.

"Alikimbizwa hospitali ya Huruma lakini alipewa rufaa kwenda KCMC. Tayari ameshafanyiwa operation kubwa 2 za tumbo, na ameshonwa jumla ya majeraha ya nje zaidi ya 20. Kwa sasa yupo ICU. Yupo kwenye mstari mwembamba kati ya kifo na uzima. Wakati huohuo Tarimo anaendelea na shughuli zake kama vile hakuna kilichotokea.

"Beatrice ana watoto wawili ambao aliwazaa kabla hajakutana na Tarimo. Mmoja yupo chuo kikuu UDSM mwaka wa 3 na mwingine yupo darasa la 5. Katika hali ya kushangaza Tarimo amesema atawasaka watoto hao na kuwaua. Watoto hao wameripoti kutishiwa maisha kwenye kituo cha polisi Tarakea lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

"#MyTake:


"Polisi kwanini mnasita kuchukua hatua dhidi ya Bw.Paul Tarimo? Mtu anachomwa visu 25 hadharani na mtuhumiwa anatamba mtaani? Lini mmekua "Goigoi" kiasi cha kuogopa watuhumiwa? Mnataka Beatrice afe ili mseme mlikosa ushahidi wa kumkamata Tarimo? OCD Rombo hivi Beatrice angekua mwanao, huyo Tarimo angekua uraiani hadi sasa? IGP Wambura tafadhali shughulika na OCD Rombo na askari wake maana wanafanya jeshi la polisi litukanwe unnecesarily!" - Aliandika Malisa


Mtoto wa Beatrice akiomba msaada wa mtuhumiwa kukamatwa wakati mama yake akiwa ICU, akisema waliripoti tukio hilo polisi lakini hawakupata msaada stahiki, akiliomba jeshi la polisi kuhakikisha mtuhumiwa huyo anakamatwa kwani ni tishio kwa maisha yao lakini pia bili ya hospitali ilikuwa imefikia milioni 9 na wahawana namna ya kulipa deni hilo​
===

Majonzi yatawala baada ya Beatrice kufariki dunia Disemba 27, 2023


====
Kwa muendelezo zaidi wa sakata hili pia soma:

- Aliyemchoma Mwanamke visu 25 na kumsababisha Kifo afariki dunia akiwa chini ya ulinzi

- Utata Sakata la mauaji ya Beatrice Minja: Kwanini serikali imehamishia mwili wa Paul KCMC wakati uchunguzi ungeweza kufanyika hospitali aliyofia?

- Godlisten Malisa akamatwa tena na Jeshi la Polisi na kusafirishwa mkoani Kilimanjaro

- Adolf Mkenda atajwa kuwa chanzo cha Godlisten Malissa kukamatwa tena
 
Huyu ndio msaidizi wa nyumbani wa Waziri ? Mbona kama mlisita sita weer....hadi semaji kuu limeingilia kati hakuna RPC wala RC Mkoa husika ? Kuna deal.hapo kati. RPC amekuwa vompromised na nguvu za Waziri ? Sasa vipi Waziri mwenyewe akitekeleza kitu kama hicho atakamatwa kweli ? Kuna shida mahali, hakuna mtu alue juu ya sheria. Prof Mkenda alichokifanya sio haki kumlinda muuaji kusa madaraka yake ... Waziri
 
Huyu ndio msaidizi wa nyumbani wa Waziri ? Mbona kama mlisita sita weer....hadi semaji kuu limeingilia kati hakuna RPC wala RC Mkoa husika ? Kuna deal.hapo kati .....RPC amekuwa vompromised na nguvu za Waziri ? Sasa vipi Waziri mwenyewe akitekeleza kitu kama hicho atakamatwa kweli ? Kuna shida mahali.....hakuna mtu alue juu ya sheria....Prof Mkenda alichokifanya sio haki....kumlinda muuaji kusa madaraka yake....Waziri
"hadi semaji kuu limeingilia Kati"
 
Huyu ndio msaidizi wa nyumbani wa Waziri ? Mbona kama mlisita sita weer....hadi semaji kuu limeingilia kati hakuna RPC wala RC Mkoa husika ? Kuna deal.hapo kati .....RPC amekuwa vompromised na nguvu za Waziri ? Sasa vipi Waziri mwenyewe akitekeleza kitu kama hicho atakamatwa kweli ? Kuna shida mahali.....hakuna mtu alue juu ya sheria....Prof Mkenda alichokifanya sio haki....kumlinda muuaji kusa madaraka yake....Waziri
hao mawaziri ni watu wadogo sana sana, nafasi za uteuzi hata sio za kupandisha mabega, ona PAULINE GEKUL alivyofyatuliwa amesumbuliwa hadi na vinyangarika kama kina madeleka tu na maelezo polisia amechukuliwa na bila shaka yupo nje kwa dhamana akitakiwa kuhudhuria polisi kwa muda fulani. naashauri polisi ukiona hao viongozi wana tuhuma, nenda tu kakamate waandikwe maelezo na upelelezi uendelee.
 
Jeshi la Polisi nchini, limesema limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa aliyemuua Beatrice James Minja, kwa kumchoma kisu, mnamo Novemba 12, 2023, huko Tarakea wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.
.
Akitoa Taarifa hiyo, leo Disemba 31, 2023, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, SACP David Misime, amesema Mtuhumiwa huyo ambaye jina lake ni Lukas Paul Tarimo, alikamatwa akiwa amejificha katika Kijiji cha Jema, kilichopo Kata ya Olondonyosambu, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, na kwamba alijaribu kujiua kwa kunywa sumu ya kuua wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo na kumkimbiza katika kituo cha afya, ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri.
#ITVUpdates
 
hao mawaziri ni watu wadogo sana sana, nafasi za uteuzi hata sio za kupandisha mabega, ona PAULINE GEKUL alivyofyatuliwa amesumbuliwa hadi na vinyangarika kama kina madeleka tu na maelezo polisia amechukuliwa na bila shaka yupo nje kwa dhamana akitakiwa kuhudhuria polisi kwa muda fulani. naashauri polisi ukiona hao viongozi wana tuhuma, nenda tu kakamate waandikwe maelezo na upelelezi uendelee.
Mkuu wanasiasa wana nguvu kama hujielewi watakusumbua akili yako
 
Kwanza I would like to ask an academic question. Yule mwanamke alichomwa kisu mara 27, ilikuwaje aliendelea kuishi siku 45?
Kwa nini polisi walikuwa wanavuta miguu kwenda kumsaka mtuhumiwa?(Lakini, hapa labda kuna simple explanation)
Huyu Lucas Paul Tarimo ni dini gani? Amewezaje kumchoma mtu kisu mara 27?
 
Aidha amebainisha kuwa baada ya Mtuhumiwa kuhisi atafikiwa na Mkono wa sheria alijaribu kunywa sumu ya kuuwa wadudu lakini Jeshi hilo lilifanikiwa kuwahi sehemu alipo mtuhumiwa huyo na jitihada za kumkimbiza katika kituo cha afya zilifanyika ambapo alipata matibabu na anaendelea vizuri huku akisubili taratibu za kisheria.
Swali kwa jeshi hilohilo
  1. Mbona hamjajitokeza kuzungumzia wale vijana wawili waliopigwa risasi Vingunguti?
  2. Mbona huyu aliyetaka kujiua kwa sumu mmemhangaikia kuokoa maisha yake wakati wale vijana wadogo nao mlikuwa na uwezo wa kunusuru uhai wao wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria sawi na Tarimo?
 
1000006565.jpg
 
Eti mtu unaua unakimbilia oldonyosambu ukidhani serikali inamkono mfupi kiasi hicho,hapo angetakiwa akimbilie Kongo ndani ndani huko ajiunge na waasi.
 
Back
Top Bottom