Arusha: Aliyemuua mwanaye kwa kugomea Jando ahukumiwa Kunyongwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watuhumiwa watatu wakazi wa mkoani Arusha akiwemo baba aliyemuua mwanaye wa kidato cha pili baada ya kugomea jando.

Hukumu hizo zimetolewa leo Jumatano Februari 15, 2023 baada ya watuhumiwa hao kutiwa hatiani na mahakama hiyo katika kesi za mauaji zilizokuwa zikiwakabili.

Hukumu hizo zimetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, aliyekasimiwa mamlaka ya ziada, Marry Mrio.

Katika hukumu hizo Hakimu Mrio, amesema upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha pasipo shaka washitakiwa hao wametenda makosa hayo ya mauaji ambayo kwa mujibu wa sheria adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa.

Waliopewa adhabu hiyo ni Jonas Mollel (58) aliyemuua mtoto wake wa kumzaa Mosses Jonas (16), Paul Laizer aliyemuua mke wake Ndomononi Sianga na Abubakar Said aliyemuua Luciana Antony.

Katika kesi iliyokuwa inamkabili Mollel, ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Juni 8, 2018 alimuua kwa kumkata na panga mtoto wake aliyekuwa na umri wa miaka 16, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili.

Amesema katika ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo mtuhumiwa alidaiwa kumuua mtoto wake baada ya mtoto huyo kukataa kwenda kufanyiwa jando nyumbani kwa baba yake baada ya baba yake kutengana na mama yake.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu huyo amesema kutokana na ushahidi wa mazingira na maelezo ya onyo yaliyotolewa polisi na mtuhumiwa huyo mahakama imeona upande wa Jamhuri umethibitisha pasipo shaka shtaka hilo na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

"Ushahidi wa mazingira ulionyesha mshitakiwa alimchukua mtoto ili akaage kwa mdhamini wa ubatizo kwa ajili ya kutahiriwa. Tangu siku hiyo alipomchukua mtoto hakurudi na alipoulizwa alisema hajui na alimjibu mkewe kuwa kumchukua mtoto ilikuwa nu geresha na ataua mmoja baada ya mwingine," amesema.

"Baadaye mtoto alikutwa amekufa kwa kukatwa shingo na Mahakama ilijiuliza ushahidi wa mazingira uliotolewa na mashahidi wa Jamhuri uliweza kuthibitisha kuwa mshitakiwa alimuua mtoto wake, na umeonyesha alikuwa na nia ovu na alijipanga kuua hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa la mauaji ya mtoto," amesema.

Wakili wa Serikali, Neema Mbwana aliieleza mahakama kuwa hawana kumbukumbu za kijinai za mshtakiwa huyo ila wanaomba mahakama itoe adhabu kama ilivyoanishwa kwenye sheria na iwe funzo kwa wengine wanaojichukulia sheria mkononi.

Naye wakili wa utetezi Fauzia Mustapha aliiomba mahakama ipunguze adhabu ikizungatia ni kosa la kwanza kwa mshitakiwa ambaye amekaa mahabusu katika Gereza Kuu la Kisongo kwa miaka mitano tangu akamatwe na ana watoto wanne wanaomtegemea.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili Hakimu huyo amesema katika utoaji wa adhabu wanakuwa wamefungwa mikono na sheria na katika kosa la mauaji adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa, hivyo mahakama hiyo kutamka mtuhumiwa huyo anahukumiwa kunyongwa hadi kufa.

Katika kesi nyingine ya mauaji namba 64/2020 Paul alishtakiwa kwa kosa la kumuua mke wake Februari 2, 2020 wilayani Longido mkoa wa Arusha.

Kesi namba 73/2020 iliyokuwa ikimkabili Said, mahakama hiyo ilimtia hatiani kwa kosa la mauaji ya Luciana Machi 9, 2019 ambapo mahakama hiyo ilieleza kupitia ushahidi ulitolewa na jamhuri marehemu alikufa kifo kisichokuwa cha kawaida ambacho kilisababishwa na kukosa hewa kwa kunyongwa kwenye shingo.

Alisema kupitia ushahidi wa jamhuri ikiwemo wa daktari ulionyesha marehemu alifariki kwa kukosa hewa huku katika maelezo ya onyo ya mshitakiwa huyo akieleza jinsi alivyomnyonga shingo marehemu.

"Mahakama inaangalia sheria katika utoaji haki,hata ukiwa na huruma kiasi gani huwezi kukiuka taratibu za sheria zilizowekwa,hivyo mahakama hii inatamka adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa mashitakiwa," ameeleza Hakimu.

MWANANCHI
 
Yaani baba aue mtoto ajili ya kukataa kukatwa mkono wa sweta?.
Ikizingatia hakimu ni mwanamke hapa anaingiwa na hali ya kuona mfumo dume na anamuona aliyeuwawa ni kama mwanaye.
 
Ngoja wakae huko miaka kumi tu.
Matokeo ya ujinga na kukosa maarifa

Watajua duniani hapa uzembe kidogo na maisha yote na matambo yote yanapotea mazima...
 
Back
Top Bottom