Arumeru Mashariki: Mwenyekiti wa CCM ahamia CHADEMA

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,272
Mwenyekiti wa CCM wa Serikali ya Kitongoji cha Madukani,eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni, Godzed Minja, juzi amerudisha kadi ya CCM na kujiunga na CHADEMA, wakati makada wa chama hicho wakimnadi Mgombea waoNassari wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kujiunga na CHADEMA, Mwenyekiti huyo Minja, alisema kuwa amefanya uamuzi huo kutokana na kuona CCM haina sera zaidi ya kusambaza matusi na kashfa badala ya kujibu hoja za msingi.

"Mimi naahidi nitakuwa mwana Chadema safi na mwaminifu na sitarudi nyuma katika mapambano haya, CCM imepoteza mwelekeo,'' alisema Minja.

Alisema kuwa atatumia muda wake mwingi kuhakikisha CCM katika Kata ya Mbuguni inapotea kabisa kwa sababu hawana sera za kuwaeleza wananchi juu ya ugumu wamaisha waliyosababisha na kuchangia viongozi wa chama hicho kupata wakati mgumukwa Wananchi.

Naye Mchungaji Israel Natse, akizungumza wakati akimnadi Mgombea wao, Nassarialisema kuwa eneo la Msitu wa Mbogo, Kata ya Mbuguni CCM imekwisha kwa sababu wanachama wengi wamehama chama hicho na kujiungana Chadema, kutokana na sera zao za matusi mbele ya watoto wadogo.

Alisema kuwa wanachama zaidi ya 300 wanasubiri Katibu wa chama hicho Taifa Dk.Slaa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, ili wakabidhi kadi hizo na kukabidhiwa kadiza Chadema mbele yao.

Mwananchi.
 
Ukiendelea kuwa mshabiki,mpenzi au mwanachama wa CCM lazima uwe na sifa zifuatazo...kwanza,lazima uwe una njaa kali,unapenda kulamba miguu ya mafisadi,pili lazima uwe na upungufu mkubwa wa akili aka tahaira...
 
"Mwenyekiti wa CCM wa serikali ya kitongoji" Hakuna nafasi hiyo kwenye CCM niijuayo mimi! Huyo kakupigeni mchanga wa macho, na kama hata nyinyi hamfahamu mfumo(structure) ya CCM basi mna walakin pia!
 
Huyo mwenyekiti kapateje huo ujanja? kweli people's power ni dawa hapa Mwanza jamaa zangu wawili kutoka office ya mkuu wa mkoa walijivua magamba na kuvalishwa magwanda hadharani mbele ya Dr Slaa na umati mkubwa wa wakazi wa Mwanza,ishara ya ukombozi 2015 wa Mtanzania.Arumeru hoye Nassari juu tuko pamoja wazee.
 
"Mwenyekiti wa CCM wa serikali ya kitongoji" Hakuna nafasi hiyo kwenye CCM niijuayo mimi! Huyo kakupigeni mchanga wa macho, na kama hata nyinyi hamfahamu mfumo(structure) ya CCM basi mna walakin pia!

we ndo hujui jinsi wanavyopatikana hao wenyeviti wa vitongoji,alishinda kwenye uchaguzi kupitia ccm vipi bado mgumu kuelewa?
 
Back
Top Bottom