Ari ya utendaji kazi ya TAKUKURU

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Hivi ari ya kutenda kazi katika kura za maoni za CCM inaonesha mpasuko katika CCM? Au wanatumiwa na kundi fulani la CCM? Je, kwenye kuwapata marais - Zenji na Tanzania hakukuwa na rushwa? Hivi tabia hii ya wadogo si ya wakubwa pia? JK hakutaka kumwadhibu Dk. Hosea wakati wa Richmond saga ili aje kumsaidia hivi sasa? Je, baada ya uchaguzi wataendelea na ari hii? Je, sasa wanauwezo wa kukukamata vigogo? Je, wanaweza kutusaidia sasa kuhusu Kagoda? Au haya ni matunda ya Hosea kupata PhD? Hivi rushwa haiwezi kupitishiwa benki kwenye akaunti ya mpokea rushwa? Hivi kuhaidiwa uongozi sio rushwa? Hao vigogo Hosea aliosema watafikishwa mahakamani hivi karibuni mbona bado?
 
hapa yanaandaliwa mazingira wananchi waiamini TUTAKUKURUKA(TAKUKURU) ili waweze kuitumia kuiba kura langu jicho tutaona
 
Usidanganyike TAKUKURU ni mafisadi namba mmoja. Watakukamata kama hujawapa rushwa. Nashukuru Mungu niliwahi kuwa nao japo kwa mda mfupi...kuna siku tulikuwa training pale Morogoro chuo cha TANESCO, Hosea alikuwa akitoa lecture alisema kitu mpaka nikatishika na kukosa interest nao na hatimaye nilijiondokea. Anasema, "hapa ndo mnaanza kazi, miaka miwili tu unakuta mtu gari mpya! Unajiuliza huyu kijana na kamshahara haka hili gari kapata wapi!". Wakati huo yy alikuwa mkurugenzi wa upelelezi, nikajua kwa kuwa alijua hilo tatizo, basi watatafuta jinsi ya kuliondoa...wapi bwana. Niliokuwa nao wakati huo.....baadhi ni matajiri wa kutisha! Hivi ulishawahi kusikia wamekamatana kwa rushwa?

SINA IMANI NA TAKUKURU. Period!
 
Morali unonyeshwa wakati huu wa uchaguzi, ni wa kutengeza mazingira ya kuvuna zaidi...watu watawahonga zaidi kuogopa kukamatwa.
 
Usidanganyike TAKUKURU ni mafisadi namba mmoja. Watakukamata kama hujawapa rushwa. Nashukuru Mungu niliwahi kuwa nao japo kwa mda mfupi...kuna siku tulikuwa training pale Morogoro chuo cha TANESCO, Hosea alikuwa akitoa lecture alisema kitu mpaka nikatishika na kukosa interest nao na hatimaye nilijiondokea. Anasema, "hapa ndo mnaanza kazi, miaka miwili tu unakuta mtu gari mpya! Unajiuliza huyu kijana na kamshahara haka hili gari kapata wapi!". Wakati huo yy alikuwa mkurugenzi wa upelelezi, nikajua kwa kuwa alijua hilo tatizo, basi watatafuta jinsi ya kuliondoa...wapi bwana. Niliokuwa nao wakati huo.....baadhi ni matajiri wa kutisha! Hivi ulishawahi kusikia wamekamatana kwa rushwa?

SINA IMANI NA TAKUKURU. Period!

Twaambiwa, kamwe tusimpe mbu kazi ya kutibu malaria tukatarajia kutokomeza ugonjwa huo. Pia twaambiwa ardhi haikomolewi kwa kuikanyaga kiaina. Aliye hai na marehemu wote wanaitegemea ardhi sawia. Hivi unaweza kucheza muziki unaotokana na makelele ya mbu masikioni mwako?
 
Kwenye uchaguzi wengi wa wapinzani watakamatwa tena kwa kubambikiziwa, nna wasiwasi hata na mgombea urais tishio la CCM akaletewa kashkash ya nguvu na (TAKUKURU). Kumbuka hakuna jambo ambalo CCM wanalifanya kwa dhamira safi.
 
Nao ni kipindi chao cha kuvuna waacheni wavune!!

Tena bila aibu wanasema wazi wazi, uchaguzi ndo wakati wa kuanzisha miradi ya kujenga nyumba!!!

Ari hiyo ni uongo mtupu, ukiangalia yaliyotokea kilimanjaro utelewa!!! Eti wanasema kumshusha cheo yule kamanda haihusiani na mumkamata DC, ya mama Sita naye kichekesho tupou; ati aliitiwa mgonjwa!!! Eti wa kumsindikiza alikuwa katibu mwenezi.... Hao hao wanamuandalia mazingira atoke... utaona.

Makamba naye anasema "watakao thibitika" tutawaengua. Swali ni nania anathibitisha kuhusika..... changanya na yako utelewa.:biggrin:
 
Mimi nimefikiri mambo mawili. Kwanza TAKUKURU si taasisi ya CCM. CCM, kama taasisi, ilipaswa kuwa na vyombo vyake vya kushughulikia mambo ya namna hii. Sasa yaelekea hakuna na kama vipo basi ni kanyaboya. Kwa hiyo Dr Slaa anapaswa kulisemea hili, kwamba CCM kutumia TAKUKURU kama sehemu yake ni kuonyesha udhaifu wa hali ya juu ya chama hicho. Makamba na Kikwete hawana uwezo wa kutambua hili.

Pili, kwa vile TAKUKURU sio sehemu ya CCM haiwezi kupambana na rushwa humo. TAKUKURU imeshindwa kupeleka wezi wote wa EPA mahakamani itawezaje kupambana na rushwa katika siasa za CCM, ambako hukuna msamiati 'kuwajibika'? Kamati ya Maadili ya CCM ina shughuli gani kama TAKUKURU ndio inafanya kazi yake?

Mwisho, hii yote ni kiini macho tu. Baada ya uchaguzi watatuambia 'unaona CCM ni safi hata TAKUKURU haikukamata mtu na yote mliyoyasikia ilikuwa ni mikikimikiki ya uchaguzi tu. Hapakuwa na ushahidi ndio maana hakuna aliyeshtakiwa mahakamani!' Sasa hivi jamaa wako laundry wanafua CCM - baada ya hapo ni safi - hata TAKUKURU watathibisha. Wameiga staili ya Mh Lowassa kuwaagiza TAKUKURU wachunguze mkataba wa Richmond, waliyofuata ni historia.
 
Back
Top Bottom