Argentina And Hijab

Hivi mtu akiwa uchi, ukamwambia kuwa yupo uchi, ni kuto kumuheshimu?

Inategemea na mtu huyo anaamini vp dhana ya kuwa uchi. Hata hivyo ni kutokumheshimu na kumvunjia uhuru wake kama mwanadamu kumkatalia mtu kuvaa apendavyo. Kama yeye kafurahishwa kuwa uchi wewe kinakuuma nini? Mna matatizo sana nyie. Mnapenda kutendewa wema lakini nyie hamuoni kuwatendea wema wengine ni haki yao pia. Acheni double standard. Leo unafurahi watu kuruhusiwa kuvaa hijab Argentina lakini hutaki watu waingie maka na madina na kuvaa watakavyo! lol
 
Ndivyo ukristo unavyo fundish hivyo, kuwa watu waachiwe watembee uchi kama wanyama.... Kaazi kweli kweli.
 
Ndo serikali zinazotawaliwa na watu wenye akili ukienda saudia hakuna uhuru wa kuabudu kama upo umebanwa sana!

Ni lazima ufahamu na uheshimu nafasi za Saudi Arabia (Macca, Madina na karibu Saudi nzima) na Jeruselem (Bait-al-Maqdis or Al-Qudus) katika uislamu, kinyume na hivyo basi labda hufahamu na huna heshima na sehemu takatifu za dini mbalimabli na sio uislamu tu. Muislamu gani umemsikia anadai aruhusiwe ku-practice uislamu ndani ya Vatican, Cantebury au Taj Mahal?

Tofautisha hizo na Argentina au Tanzania. Hizo ni sehemu takatifu na dini nyengine isiyokuwa ya hapo ni marufuku. Vile vile kuingia bila ya ruhusa (kiujanja kwa madhumuni ya kueneza dini nyengine) ni kosa kubwa, ila unaweza kukaribishwa na kuwekewa sehemu maalumu ya kufanyia ibada zako kwa ihsani ya mwenyeji, sio ufanye utakavyo tu kama utakavyoweza kufanya unapokuwa mgeni sehemu nyengine kama Tanzania katika jiji la Dar es Salaam au Arusha.

Ardhi yote ya Hijaz ni takatifu (Macca na Madina ni dhahiri kwa kila mtu) lakini sehemu nyengine vilivile ni muhimu katika historia ya uislamu, ijapokuwa watu hawazifahamu sana, kuna makaburi ya masahaha na mashahidi, kuna misikiti waliojenga masahaba, kuna sehemu ambazo mapigano (battles) na makubaliano (truces, agreements na undestandings) ambazo zilikuwa ni "turning points" katika historia ya uislamu, yalifanyika chini ya maelekezo/mwongozo wa Mtume Muhammad (SAW) mwenyewe akiwa bado yupo, hivyo zinakuwa sehemu za kumbukumbu-hai ya Sunna za Mtume. Sijui unafahamu kidogo.

Angalau katika hili ufalme wa Saudi haujaweza kuenda kabisaaaaa kinyume dhidi ya uislamu, licha ya kukaribisha majeshi ya kikafiri katika ardhi ile eti kuleta ulinzi sehemu hizo kumbe vile ni kuupa ulinzi ufalme walioupandikiza pale.

Fahamu na heshimu hilo
 
Back
Top Bottom