April '09 Bomb Blasts in Dar (Mbagala) and responses

Kuna watu wamesma kuwa kwa nini naibu waziri atoetaaRifa na wakati wataalamu wa jeshi wapo.ningependa kuwaambia hio taarifa kwa uelewa wangu huwa hazitoki kichwani kwa waziri bali anatumiwa na jeshi kuitoa na yeye anakuwa na dhamana tu ya kuwasilishana kwa wananchi

Kama taarifa ya waziri imetoka jeshini kwanini watofautiane? Waziri anasema mambo shwari,mnadhimu mkuu wa jeshi anasema kuna uwezekano wa kutokea milipuko zaidi tena ya kwenda mbali zaidi...
 
Duh kwakweli nawapa pole waathirika wa hili janga la mabomu. Kwa maoni yangu there is a message in this 'issue', kwa tunaofuatilia mambo tutakumbuka last week kuna wanaJF walionya kwamba kuna jambo moja la hatari litatokea this week kwakuwa wafisadi walikuwa wanajipanga kuhusu ishu flani...haya sasa yameanza mabomu,sijui nini kitafuata. STAY TUNED!

Ndugu yangu tuambiane mafisadi wanajitayarisha na nini? tujitayarishe kukimbia? i hope hawajapiga mabomu makusudi ili kumtisha watu na serikari?
 
Kuna watu wamesma kuwa kwa nini naibu waziri atoetaaRifa na wakati wataalamu wa jeshi wapo.ningependa kuwaambia hio taarifa kwa uelewa wangu huwa hazitoki kichwani kwa waziri bali anatumiwa na jeshi kuitoa na yeye anakuwa na dhamana tu ya kuwasilishana kwa wananchi

Nchimbi,
Ni wazi kuwa wananchi hivi sasa hawana imani na serikali ya JK hasa mawaziri wake na wengine wote walioteuliwa kiajabu ajabu bila sifa.
 
Kama taarifa ya waziri imetoka jeshini kwanini watofautiane? Waziri anasema mambo shwari,mnadhimu mkuu wa jeshi anasema kuna uwezekano wa kutokea milipuko zaidi tena ya kwenda mbali zaidi...

Hao ni Waziri na Mnadhimu wa Jeshi wanatofautiana, halafu kuna kamishna wa operesheni wa Polisi, yeye kasema hakutakuwa na madhara makubwa kwa mali na maisha ya binadamu. Akaulizwa mbona washa kufa, akadai ni mapema mno kusema lolote. Hujui kitu halafu unasema hakuna madhara.

Yani hakuna central comand, hakuna msemaji wa serikali. Waziri anafyatua, Jeshi linaongea wanavyojua wao, Polisi wanafyatua kivyao....
 
Kama taarifa ya waziri imetoka jeshini kwanini watofautiane? Waziri anasema mambo shwari,mnadhimu mkuu wa jeshi anasema kuna uwezekano wa kutokea milipuko zaidi tena ya kwenda mbali zaidi...
Mimi sioni tofauti ya habari hizo kwa maana ukiambiwa hali ni shwari haina maana kuwa hali imetengemaa.kwa kuwa ukweli ni kuwa shwari kwa maana kuwa hakuna mabomu yanayolipuka tena....lakini pia ujue kuwa hizi taarifa mbili yani za waziri na mnadhimu mkuu hazikuchukuliwa muda mmoja japo wamezitoa wakati mmoja na huu ni uzembe wa waandishi wetu.Hizi taarifa zilikuwa zimepishana muda wa masaa matatu.hivyo zote ni sahihi kwa wakati ziliotolewa ila moja sio sahihi kwa wakati zilipotangazwa
 
Mkuu unajicontradict...
 
Nchimbi,
Ni wazi kuwa wananchi hivi sasa hawana imani na serikali ya JK hasa mawaziri wake na wengine wote walioteuliwa kiajabu ajabu bila sifa.
Kwanza hakuna mtu alieteuliwa kiajabu na wala hakuna mbunge wa ajabu kwa kuwa mawaziri wote ni wateule wa kutoka miongoni mwa wabunge ambao ni wawakilishi halali wa wananchi wa Tanzania...kama ni kweli wananchi wanashangaa uteuzi wa wabunge wao kuwa mawaziri basi ni wazi kuwa rais nae ana haki ya kuwashangaa hao wananchi kwa kumchagulia wabunge wasiofaa na hatimaye yeye kujikuta hana choice zaidi ya kuwateua hao
 
Rais mwenyewe hafai, halafu ukitaka kusema wananchi wa Tanzania hawawi manipulated katika chaguzi za Tanzania utakuwa si mkweli. watu wote wenye uelewa wanajua CCM imeiba hela za EPA kupigia kampeni, sasa hapo kuna uhalali gani?

Mawaziri wanaenda kununua vyeti Almeida na kwenye diploma mills kebe kebe ilimradi waitwe Dr. tu, kuna integrity hapa?

Watu wame stoop low mpaka kum photoshop Salim katika a nasty propaganda campaign, kuna ustaarabu hapo?

Hii ni karma kwa Kikwete kuhusu wizi wake alioufanya, hatuombei mabaya lakini kama hamna uongozi lazima mambo yataenda alijojo tu.

Gari halina dereva utategemeaje lisiache njia?
 
Tena wachovu wenye kujibandika 'Qualifications' ambazo hawana!!!!
Nadhani hapa tunatoka nje ya mada lakini swala la kubandika qualification ni jambo lenye kuhitaji mjadala mrefu sana.Kwa kuwa nachojua mimi ni kuwa ata wahitimu wetu wa udsm kuna vyuo haviwakubali kwa masters kwa kuwa wanakiona chuo chetu bora kabisa ambacho ata mimi nimekisoma kuwa ni substandard.....wao nao wanasema kuwa ni za kubandika..proffessor wetu wa magonjwa ya moyo muhimbili aruhusiwi wala kumtibu mgonjwa wa BP india.
 
Hello Members

Napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole wahanga wote wa mlipuko huu wa mabomu mbagala kwani it very sad and painfull to see people are suffering kwa uzembe wa watu wachache kwani hadi sasa hawajatumbia kama the areas are safe.Shame on them for those who cause this mess
 
Kwanza pole waanga wote wa hili janga. Pili, mpaka sasa hivi ni hatua zipi zimechukuliwa na serikali kuanzia kusimamia usalama na mali za raia? Yule waziri aliyeenda kutembelea Segerea ametoa tamko gani kuhusu usalama na mali za raia?
 
Nimesema shwari haina maana kuwa ni tengemavu.pili nimesema kuwa waandishi wamerusha hewani habari kwa pamoja yani taarifa ya Mnadhimu na waziri lakini kimsingi hizi taarifa mbili zilitoka kwa tofauti ya masaa 3
 
Hii si mara ya kwanza Ghala la silaha kulipuliwa.Miaka ya Nyuma Mafinga JKT ghala la silaha lilipuka pia.sijui ilikua ni ajali au ni kuficha wizi.Ajali?!!!? Ndiyo inawezekana.Lakini.Nasikia harufu ya Ufisadi..Ukiuza silaha na risasi kwa majambazi,Ukiuza silaha na mabomu nchi jirani wapiganako vita,Ukinunua silaha hewa,Unabakiwa na kazi moja tu.Choma moto Ghala la silaha kukata ngebe na kuua so.Kila mtu anakula kutokea mezani pake...Nasikia harufu kali ya Ufisadi hapa.
 
great...now an opportunity arises for a no bid contract to a "friend" to buy the weapons again...classic
 
Nchimbi mwenyewe kumbe anafyatua hayuko hata Dar kwenyewe.

Ammo Explodes at Tanzania Dump Site, 3 Killed

By THE ASSOCIATED PRESS
Published: April 29, 2009

ARUSHA, Tanzania (AP) -- Huge explosions rocked an ammunition dump at an army camp in Tanzania's commercial capital Wednesday, killing three people and injuring more than 150, officials said.

Dr Sylvia Mamkwe, a doctor at Temeke Municipal, said it had received the three fatalities, and state-run Tanzania Broadcasting Corp., citing police on the site, gave the injury total.

Police spokesman Mohamed Mhina said the blasts lasted for about two hours and fires were still burning two hours after that. Local media reports said houses around the military base were on fire.

Local schools have called parents to come pick up their children. The blast rattled windows in houses 37 miles (60 kilometers) away, said resident Kate Esmail.

William Nchimbi, the deputy defense minister, said bombs, bullets and other ammunition exploded in an armory at the Bagala Army Camp in the coastal city of Dar es Salaam.

''We have formed a team to assess the source and the loss incurred,''
Nchimbi told journalists in the northeastern town of Arusha, where he was attending a regional leaders' meeting. He did not take any questions.

Ammunition dumps in Tanzania are volatile and easily ignited. The Bagala Army Camp is surrounded by civilian homes but is far from downtown Dar es Salaam.
 
Amiri Jeshi Mkuu yuko wapi? Au kama kawaida yake kwa mara nyingine tena 'hahusiki'? Je, walioumia katika janga hili wameshaenda kupewa pole na kiongozi yeyote wa juu wa Serikali na kuambiwa Serikali itawasaidiaje kama kuna ambao hawana mahali pa kuishi kutokana na janga hili? Naona wale waliokuwa wanapiga kelele kwamba ni "Kikwete tu 2010" idadi yao itazidi kupungua maana ushahidi unazidi kungezeka kwamba nchi haina uongozi kabisa.
 
Back
Top Bottom