Apata kipigo kutoka kwa watoto wake

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MWANAUME aliyetambulika kwa jina moja la Faridi [59] mkazi wa Gongolamboto jijini Dar es Salaam, amekutwa na kadhia nyingine ya kupewa kipigo kutoka kwa watoto wake kutokana na tabia za kumnyanyasa mke wake.

MWanaume huyu alinusurika adhabu mahakamani kwa mke wake kwenda kufuta kesi kutokana na kumuonea huruma mume wake aliozaa nae watoto na kuishi nae kwa muda mrefu.

Huu ni muendelezo wa habari iliyoandikwa katika mtandao huu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ampeleka mumewe polisi.

Awali Faridi aliweza kufikishwa kituo cha polisi na mke wake kutokana na tabia ya zake chafu ikiwemo na kumpiga mara kwa mara na watoto wao kutoa idhini aweze kumfikisha kituo cha polisi.

Ilidaiwa mwanaume huyo alikuwa akihitaji kuoa mke wa pili na amlete katika nyumba aliyojenga na mke huyo kitendo ambacho mke wake Bi FAtma [50] alikuwa hakiafiki na kumfanyia visa kila kukicha ili aweze kuondoka katika nyumba hiyo alete mke mwingine

Juzi majira ya jioni ilidaiwa kuwa, Farid aliweza kufika nyumbani kwake akiwa na mwanamke mwingine anayekadiriiwa kuwa na miaka kati ya 30 hadi 32 kwa minajili ya kuja kuwatambulisha watoto wake akiwemo na mke wake kuwa ni mama yao mwingine ambae anatarajia kufunga nae ndoa

Imedaiwa kuwa mara baada ya kufanya utambulisho huo watoto wake waliingia ndani na kuweka bunge la muda kuhusiana na kitendo alichofanya baba yao na kufika maamuzi ya kuwaadabisha wote wawili huku wengine wakiwa na mawazo wamfukuze mama huyo na wengine wakidai watakuwa wanamuonea huyo mwanamke na kufikia maamuzi ya kumuadabisha baba yao

Imedaiwa kuwa mtoto wake wa kiume ambaye alipigiwa simu kwa kuwa anaishi karibu na nyumbani hapo alifika nyumbani hapo na kuanza kufanya vurugu kwa baba huyo na hatimaye watoto wake wengine wawili wa kike wakaingilia ugomvi huo na kujikuta wakimpa kichapo baba yao huku wakilia kwa machungu kuonewa kwa mama yao

Habari hii ni ndefu itaendelea tena
 
Mkasa mkubwa!. Kusema kweli kitendo cha watoto kumpiga mzazi wao kinasikitisha sana, na katika hali ya kawaida kingeonekana kuwa ni laana kwa watoto.
Lakini vile vile kwa mume kumpiga mke wake ni tendo ambalo halipaswi kuwachwa lipite bure bure. Kwa upande mmoja, kutokana na malezi tuliyopewa, nawahisi watoto ni wakosa kwa kumpiga baba yao. Kwa upande wa pili, nahisi ni stahiki yake kwani alipitilisha mipaka. Kwa kuwa mama alikuwa hawezi kujitetea, watoto wake ndio watetezi wake. Pengine angalau itakuwa fundisho kuwa mwanamke hapigwi!
 
hivi kwa kawaida watoto wanatakiwa waamulie au waingilie kati kumsaidia mama kwa kumpa kipigo baba!
Mkasa mkubwa!. Kusema kweli kitendo cha watoto kumpiga mzazi wao kinasikitisha sana, na katika hali ya kawaida kingeonekana kuwa ni laana kwa watoto.
Lakini vile vile kwa mume kumpiga mke wake ni tendo ambalo halipaswi kuwachwa lipite bure bure. Kwa upande mmoja, kutokana na malezi tuliyopewa, nawahisi watoto ni wakosa kwa kumpiga baba yao. Kwa upande wa pili, nahisi ni stahiki yake kwani alipitilisha mipaka. Kwa kuwa mama alikuwa hawezi kujitetea, watoto wake ndio watetezi wake. Pengine angalau itakuwa fundisho kuwa mwanamke hapigwi!
 
ukiona imefikia hatua hiyo lazima ujue kwamba watoto wameshachoka.
siwalaumu na natoa pongezi zangu za dhati kwa watoto hawa.
 
Back
Top Bottom