Anyweshwa maji ya betri na vibaka

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Mustafa huko wilayan Kondoa amelazwa katika hospitali ya wilaya baada ya kukutana na VIBAKA ambao walipomsimamisha walimpora vitu na kunywesha kinachosadikiwa kuwa ni maji ya betri au tindikali.

Daktari mmoja amethibitisha hilo na kusema kuwa kwa sasa Mustafa ana vidonda mdomoni na tumboni pia anakoroma tu hata kusema hawez (hali ambayo inazidi kubadilika) kadri muda unavyokwenda.

source: KURUNZI LA REDIO IMAAN
 
Daah.......kuna watu wana roho mbaya, bora ukutane na simba kuliko wao!
 
lazima kuna kisa kakifanya ambacho kipo sawa au zaidi ya kunyweshwa maji ya betri.Matukio kama hayo huwa ni Visasi .
 
kuna vitu hapo wake za watu sumu pia vya watu haviendi bure
 
pole sana Mustafa. Hao redio iman hovyo kabisa wanafumbia macho matukio kibao hili wamelipaisha kwa sababu muathirika ni MUSTAFA. Shame on you redio nini sijui!!!
 
ambaye hayajamfika ya vibaka ndo huwa anasema usichukue sheria mkononi, lakini wakishakuliza afu ukakuta kibaka anashughulikiwa unaweza ukaomba wakuachie ili amfaidi vizuri
 
ambaye hayajamfika ya vibaka ndo huwa anasema usichukue sheria mkononi, lakini wakishakuliza afu ukakuta kibaka anashughulikiwa unaweza ukaomba wakuachie ili amfaidi vizuri

unalosema ni kweli kabisa Baba V. but nashangaa sana hivi utu hakuna kabisa ama ni nini? kweli unamnywesha mwenzio tindikali??? kama umesha mwibia basi mwache aende zake kwa amani.
 
Last edited by a moderator:
uwiiii! jamani binadamu kweli tumefikia hapa? yaani nakubaliana na sweetlady kwa mantiki hii. na ni bora wangemwua kabisa ingempunguzia matatizo kuliko kumsababishia haya ya kansa na matatizo ya maini na figo na utumbo kuoza jamani.
 
Inashangaza sana gfsonwin......binadamu wa siku hizi hawana ubinadamu kabisa......yaani kama simba!
 
Last edited by a moderator:
Inashangaza sana gfsonwin......binadamu wa siku hizi hawana ubinadamu kabisa......yaani kama simba!
sijui tutaish vipi aisee, na namna hii japo Mungu aliumba dunia kama sehem nzuri ya watu kufurahia kuish lakin dunia hii imekuwa sio mahali pa furaha bali hofu.
 
Back
Top Bottom