Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 189
Katika awamu ya tatu ya utawala wa Tanzania chini ya Rais Benjamin Willium Mkapa, mkewa, Anna, alikuja na dhana (Taasisi) ya kuwaletea maendeleo wanawake aliyoiita Fursa Sawa kwa Wote. Baada ya kuingia awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, mkewe naye, Salma, amekuja na dhana (Taasisi) iitwajo Wanawake na Maendeleo (WAMA). Sina kumbukumbu kama Wake za Marais wa awamu ya kwanza na ya pili nao walianzisha Taasisi za aina hiyo. Je wadau hii inaashiria nini katika awamu hizi mbili na zinazokuja?