Anna Mghwira avuliwa uenyekiti ACT-Wazalendo, Yeremia Maganja akaimu uwenyekiti

Wanasiasa wa bongo bana!! Nisaidieni kwa anayejua/anaeweza nataka kwenda kuishi Canada nitulizane huko kwanza miaka ishirini ndipo nipige simu bongo
 
Ha ha amepata kigugumizi kuzungumzia hilo la kupewa ilani ya kijani., nilitamani ZZK ndie angekua mzungumzaji wa hili suala
 
Chama cha ACT-Wazalendo leo kimetangaza kumuondoa Anna Mghwira kwenye nafasi ya uenyekiti wa chama hicho.

KUHUSU MRITHI WA MGHWIRA: Chama cha ACT-Wazalendo leo kimemtangaza Yeremia Maganja kuwa Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho hadi uchaguzi utakapoitishwa.
Dili hilo. Jiulize why zito amesafiri. Kama chadema tu
 
Kuteuliwa kwa watu wawili hakumaanishi kwamba wanaweza kushika nchi, inawezekana hao wawili ndio walioonekana wana uwezo katika hao wengine waliobaki, ila kama nchi inaongozwa na watu wawili basi hoja ya ACT inasimama, ila mpaka sasa bado mnasafari ndefu.
 
Halafu wamebanana sana kwa nini wanapoongea wasipeane nafasi kidogo au lazima wakusanyike pamoja na kuchungulia mic wote
 
Wakati Anna anateuliwa alikuwa nji za nje... Kamati kuu inakaa na kutoa tamko, Kiongozi Mkuu wa Chama yuko nji za nje...

What a coincidence.. Hahhaha
 
Kwahiyo mama aliposikia uteuzi tu, akabadili tiketi faster na kurudi zake bongo. Hakuna kusubiri ni kuwahi tu.
 
Wanasiasa wa bongo bana!! Nisaidieni kwa anayejua/anaeweza nataka kwenda kuishi Canada nitulizane huko kwanza miaka ishirini ndipo nipige simu bongo
kwani ukiishi nchini lazima ufanye siasa?

huko canada kuna vigodoro?

huko kuna simba na yanga?

huko kuna wazee wa ngwasuma na twanga pepeta?

Tunahitaji kampani yako braza
 
Eti Anamwigulu sijui Anna nani kwa kuteuliwa na Rais kuwa RC inaonyesha kuwa ACT ipo tayari kuongoza nchi.

Kha yani Hawa ACT sijui wanaubongo wa mdudu gani. Huyo bibi na kuzunguka nchi nzima alipata sijui kura 500 alafu Leo wanajitoa ufahamu.

Nazani sasa ni zamu ya Mwigamba kuteuliwa nafasi ya Mtendaji Kata ili na yeye aseme yupo tayari kuongoza jimbo
 
Nchi hii haiwezi kukombolewa mikononi mwa chama cha makabahila kupitia mtu/watu wasiojiweza kiuchumi. Maskini akirushiwa mfupa lazma mate yamtoke na abadili njia.
Wapinzani wajijenge vizuri kiuchumi na wagombea wawewatu wasiyo na njaa at least!! Mtu kaajiriwa anategemea kamshahara cha ajira Leo mnamteua kugombea urais!! Poor you...
huyu alikuwa anatafuta kazi kupitia chamachake na tunajua wakowengi,bora angepewa kazi nyingine sio ukuu wa mkoa kazi inayotumika kwasasa kukomoa na kuporomosha jitihada za upinzani.
 
Hakika dhambi na laana ya usaliti ishaanza kuwala wasaliti mchana kweupee pe,tulisha sema awali ACT ni CCM B.Leo CCM A na viongozi wao wameshindwa kuvunga wanaumbuka waziwazi.

Hakika hapa ndiyo utaamini ya kuwa Mungu yupo na UHAI, angalia Le Propese le TUMBO anavyoteseka naye eti M/Kiti wa M/Kiti wa vyama vya siasa le Mutungi le wasaliti.

Angalia Baby Josephine laana ilivyo mfanya hadi leo anaficha uso wake kuogopa na kuona aibu yakuwa dunia inamzomea.

My Take: Huu ni mwanzo tu mengi yanakuja....zaidi Le Goli la Mkono le Nape...na bado..
Heri siku nyingine ukaficha upumbavu wako kuliko kuja kujiaibisha kwa haya uliyoandika.
 
ACT inajikosha tu lakini kuna walakini mkubwa katika haya yanayoendelea,alivyoteuliwa KITILA mlijitetea ni muajiriwa wa serikali sasa kateuliwa mwenyekiti wa chama ambaye inambidi aachie nafasi yake ya uenyekiti akatumikie ilani ya CCM bado tu mnatetea?Halafu kwa Rais kufanya uteuzi wa kiongozi wa chama bila kuwapa taarifa kabla hiyo ni dharau kubwa sana kwa chama sijui kwa muhusika labda alishawasiliana nae lakini kwa chama rais anateua bila ya kuwapa taarifa inamaana amewadharau na ana nia ya kuwavuruga tu au kuna kazi mlimfanyia na sasa haya ni malipo yake.chukulia mfano wa kilichotokea,tarifa imetolewa na ikulu kuwa mwenyekiti wa ACT ameteuliwa ZITTO akasema hawajawasiliana na mwenyekiti wao kwasababu yuko nje ya nchi,kabla hawajakaa kikao cha kutafakari na kutoa maamuzi kuhusiana na uteuzi tayari mwenyekiti wao keshawahi ikulu kuapishwa na sasa hivi yuko kazini mkoani kwake!mnasema rais amevunja mwiko wa kuteuwa wapinzani lakini sidhani kama ACT walikuwa wapinzani lakini sikuzote ukijikombakomba unapata malipo yako.
 
Back
Top Bottom