Angalizo: Wanaoweka matangazo ya kutafuta Kazi

Aisee kweli kbsaaaaaaaa tena hasa mabinti jmn.

Wanapotafuta kazi na wakahitajika kwenda kuonana na huyo mtu, ki ukweli ushauri wangu wasijiamini kuptiliza kwa maisha ya sasa....maisha ambayo kila mtu ana shida ya pesa...na wengine wananjia zao za kupata pesa.

Soo kina dada chonde chonde, mnapotafta kazi sehemu kama hizi kwa watu usioowajua ni hatari sana.
 
Thanks very much for giving us that education. Finding a job is not as easy as we think, but good introduction and explanations can really help. We have to be careful though! May God bless you.
 
thumb20.jpg


Salaam!

Ni muda sasa humu Jukwaani kumekuwa na mabandiko ya watu mbalimbali wakiomba kazi, zile za ujuzi mahususi na zile za jumla.

Baadhi ya wanaoandika wamekuwa wakitaja sifa zao, wengine wakitaja kwa upana na wengine kwa ufupi sana na wakati mwingine bila taarifa zozote zitakazomwezesha mwajiri kupata fununu za mtu anayetaka kumuajiri.

Kama ambavyo wanaoweka matangazo ya kazi waliaswa hapa: ZINGATIA-Mnaoweka matangazo ya kazi humu nadhani ni wakati wa wanaoweka matangazo ya kusaka kazi pia tukazingatia vigezo kadha wa kadha.

Walau tangazo la kutafuta kazi liwe na vitu vifuatavyo:


  • Wasifu, kwa kuwa kanuni za JF zinalinda haki ya faragha, utambulisho uhusishe wasifu mwingine ISIPOKUWA majina. Mathalani, mwombaji anaweza kusema kuwa yeye ni kijana mwenye umri wa miaka XX anayepatikana eneo XY.
  • Elimu, hii inasaidia mtu ambaye anaomba kazi kuweka wazi elimu aliyonayo, iwe ya jumla au ya utaalamu mahususi. Waajiri au wenye kujua fursa za ajira wangependa kujua elimu aliyonayo mhitaji ili wamsaidie iwezekanavyo.
  • Uzoefu. Hiki ni kigezo kinachompa sifa za ziada mwombaji. Ni vema kusema kama umewahi kufanya kazi, semina ama kuhudhuria mafunzo fulani maalumu kwani itaongeza ushindani wa mwombaji.
  • Mapendeleo. Kutaja elimu na uzoefu pekee hakutoshi, ni vema muombaji/mhitaji akaweka wazi kazi, eneo, mazingira ya kazi ambayo anayapendelea pamoja na vitu vingine vya ziada. Kuandika kwa ujumla sana hupelekea wasio na nia njema kujibu kwa kejeli na dhihaka. Kuwa mahususi na kazi itakiwayo kutapunguza majibu mengi yasiyofaa kwa mwombaji.
  • Andiko lisiwe na nia ya kuvuta sana usikivu. Maandiko yenye uelekeo wa kulia-lia, kutangaza kuwa maisha ni magumu na hujui ufanyaje hakurahisishi harakati za kupata kazi. Watu wenye nia mbaya wanaweza kutumia uhitaji huo uliopitiliza kwa manufaa yao kiuchumi (utapeli) na hata kingono (hasa kwa mabinti).

Nawatakieni kila lililo jema katika harakati za kusaka ajira!


asante
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom