TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 13,768
- 21,253
Hii ni picha juu ni ya jamaa yetu (mwafrika) mwanaume anayenyongwa kwa kutumia kifaa cha kunyongea kiitwacho garrote.
Picha chini ni garrote inavyoonekana kwa karibu sana, usigukilie kifaa kilivyo au maumivu yake yanakuwaje ila ni vipi binadamu aliunda kifaa hiki ili kitumike kutoa adhabu kwa mwenzake.
Garrote ni kifaa cha kutekelezea mauaji hayo ambacho kimeandikwa kilitumika katika karne ya kwanza BC huko Roma.
Aliyehukumiwa alitakiwa kukaa na kufungwa na chuma shingoni mwake kabla ya mnyongaji kugeuza au kuzungusha skrubu ambayo kinadharia ingepasua ubongo wake, na kumuua papo hapo, ila hii ilipitia shingoni na kumtoboa hadi upande wa pili wa shingo.
Mateso haya ambayo mwafrika aliyapata kutokana na uenda kukaidi au kwenda kinyume na matakwa ya bosi wake kwa miaka hiyo, ilidhihilisha unyanywasaji mkubwa wa binadamu kwa karne hiyo.
Japo leo hakuna njia kama hiyo bado mwafrika anapitia changamoto kubwa sana.