Anayemiliki mabasi ya Kilimanjaro ni Tajiri wa ajabu kweli kweli

Hivi hiyo biz Ugumu wake uko wapi,? Kwenye kutowa huduma? Au kwenye service ya magari? Au kwenye kulipa mishahara maworker?! ..Yani sijaelewa ugumu wa hii biz ya mabasi iko wapi..

Maana kwa route moja tu gari inaweza ingiza hata 1.2+M Sasa hasara inatokea wapi hapo wakuu?
 
Biashara ya ma bus inatakiwa iendeshwe kama anavyoendesha Klm ndo maana muhuni yupo kwenye game kitambo na bado analeta G7 mpya namba D
Ukikurupuka unafilisika chap tu , Darlux kaingia na wenge leo Yuko chali na michina yake ila muhuni klm xprss anakomaa na marcopolo gari zenye maisha marefu anazifanyia maborsho ya Mara kwa Mara na huduma bora ndo maana ana survive yupo kwenye game Hadi leo.

Biashara ya bus ni pasua kichwa kama huna roho ngumu huwezi kuifanya inaweza kukufilisi chap tu ukajikuta umetajirisha maajent na makondakta, kwahiyo unatakiwa ujue unae mshauri anaijua hiyo biashara vilivyo hawezi kuwekeza pesa nyingi kuliko faida anayopata huko ni kuchoma hela, wachoma hela wote sahivi wako chali japo waliingia na michina ya kisasa
Anataka kumfananisha mwenzie na watakatisha pesa, Bongo hii usishindane na biashara ya mwenzako, Amwache afanye kwa pace yake.
 
Labda yakichoka ndo anayapeleka ruti zingine
Biashara siri kaa na ujinga wako na biashara ni huria

Ukitaka kushindana na kilimanjaro express sio kesi kanunue mabasi yako most current kaweke route anaenda kilimanjaro sio kesi uone mziki wake na hayo mabasi yako most current tuone nani ataendelea ku survive sokoni soko la bus transportation
 
M
Biashara siri kaa na ujinga wako na biashara ni huria

Ukitaka kushindana na kilimanjaro express sio kesi kanunue mabasi yako most current kaweke route anaenda kilimanjaro sio kesi uone mziki wake na hayo mabasi yako most current tuone nani ataendelea ku survive sokoni soko la bus transportation
Mbona una hasira sana
RELAX😎
 
Loyal customers siyo royal customers
Sawa cha msingi umeelewa

Kilimanjaro brand ni brand kubwa hata awe ni mabasi mabovu vipi ana customer base kubwa very loyal to him

New entrant kupenya na kujenga brand sokoni ufikie brand ya kilimanjaro Express itakuchukua Miaka na gharama kubwa mno

Kwanza hata kabla kufikia utakuwa umefilisika kwa kukosa loyal customers
 
Anataka kumfananisha mwenzie na watakatisha pesa, Bongo hii usishindane na biashara ya mwenzako, Amwache afanye kwa pace yake.
Biashara ya bus ni ngumu sana ukinunua bus ya million 300 anaeanza kula hela ni wapiga debe kila stand,ajent kila stand,dereva, traffic kabla yako alaf gari ikiharibika wote huwaoni msala ni wako
Bado wamiliki wa mabus barabarani wanakutana na vikwazo vingi sana maana safari zao ni mchana tu na ni lazima zifike kituo kilichopangwa huko barabarani unamwagwa hela siyo mchezo bila hivyo kazi haifanyiki.
 
Ngoja niseme ivi haya magari nlisha achaga kupanda mda mrefu sana achilia mbali mwendo wao wa kobe tulisha wahi haribikiwa na gari korogwe nakumbuka tulifika arusha saa tano usiku ni miaka 6 imepita toka kipindi hicho sikuwahi panda tena
 
Uko sahihi sumry alikuwa na mabasi 80 brand ya kisasa aliuza yote kukimbia ushindani akaenda kulima sumbawanga

Akina Kilimanjaro aliwakuta akaondoka kwenye biashara na mabasi yake Classic akina Kilimanjaro bado wanaenda

Anayebisha aingie YouTube a search kwa kuandika milionea Sumry amsikie mwenyewe alichoongea kuhusu hiyo biashara ya mabasi
mh,cjui kama ni kweli au la,mi nilisikia kipindi cha nyuma,plate namba za gari na pikipiki zilikuwa zinafanana,kwa hiyo matajiri wa mabasi walikuwa wanasajili mabasi kwa plate namba za pikipiki,mambo yalivyokuja kubumbuluka,makesi na mafaini ya hatari juu,ilikuwa biashara ngumu sana.
 
Hii kampuni nimewaungisha sana lakini kwa sasa nataka kuwakimbia.

Tajiri ana mabasi ambayo yana namba A yapo barabarani yamechakaa.

Hata ile ajali ya Mbeya, juzi inasemekana uchakavu wa gari nao ni chanzo kikubwa.

Tajiri hanunui gari mpya anavizia wenzake wafilisike or magari yao yachoke kisha anayanunua kwa bei rahisi kisha anayapeleka gereji yake anayachomelea na kuyapiga rangi kisha anayaweka barabarani anayaita luxury.

Mfano ni zile gari za Dar Lux kazinunua kazipiga rangi kisha akaweka engine za Scania , akazileta barabarani ila cha kushangaza yale magari yana AC juu ila ukipanda ni joto kwa kwenda mbele hamna AC mule ni janja janja.

Magari ya Kilimanjaro baadhi yameshachoka, mengine hadi ndani kuna harufu ya uvundo lakini mmiliki anajidani anatoa huduma za kisasa.

Ni muda muafaka kwa wamiliki wa hii kampuni wakiona ubahili kununua Scania mpya basi wamgeukie mchina la sivyo hii kampuni tutaikimbia soon.

Angalia matajiri wengine kama Nacharo na Sauli. Sauli alianza na gari chache juzi kanunua Marco polo mpya kaweka barabarani.

Juzi Nacharo ya Tanga baada ya kucheza na mchina kwa kipindi kifupi juzi kanunua gari mpya za marcopolo scania kweka barabarani.

Na siku hizi makampuni ya kuunda mabasi kama una kampuni kubwa unachukua magari na unalipa kwa awamu sijui anakwama wapi.
kapicha bas
 
Sawa cha msingi umeelewa

Kilimanjaro brand ni brand kubwa hata awe ni mabasi mabovu vipi ana customer base kubwa very loyal to him

New entrant kupenya na kujenga brand sokoni ufikie brand ya kilimanjaro Express itakuchukua Miaka na gharama kubwa mno

Kwanza hata kabla kufikia utakuwa umefilisika kwa kukosa loyal customers
Watu wanadhani kuwa na gar mpya umemaliza kuna ishu ya loyal customers
Leta gari mpya utajaza na yeye mwenye mkweche anajaza vile vile mpaka uje kumfikia umeisha
 
Back
Top Bottom