Anayejua kuhifadhi maji ya mvua

Lwakalisa

Member
Feb 26, 2013
27
12
Jambo wadau,

Naomba kwa mwenye kujua, nimekuwa nikikinga maji ya mvua ila yakikaa baada ya muda huwa yanakawaida ya kuteleza. Nifanye nini ili yakae muda mrefu ukichukulia hali ya upatikanaji wa maji ni íssue.
 
jambo wadau. naomba kwa mwenye kujua. nimekuwa nikikinga maji ya mvua ila yakikaa baada ya muda huwa yanakawaida ya kuteleza. nifanye nini iliyakae muda mrefu ukichukulia hali ya upatikanaji wa maji ni íssue.

Pole sana mkuu, hilo limewakuta wengi. Wengine maji yao huwa yananuka!

Mimi mara nyingi hasa ninapokuwa na wageni wachache kwangu, natumia maji ya mvua toka kipindi kimoja cha masika mpaka kingine bila shida ya maji hayo kunuka wala kuteleza ingawa si mtaalam wa maji.

Shida ya maji ama kunuka au kuteleza hutokea kama unaruhusu maji yakaingiwa na mwanga wa jua mara kwa mara na kwa muda mrefu. Pia jitahidi kudhibiti matakataka mengi toka nje yasiingie katika tank la maji yako; hii itakusaidia kutofanya usafi wa tank mara kwa mara. Kufanya usafi wa tank ni kajishughuli kanako sumbua kiasi fulani.

Ili kuzuia mwanga usiingie katika tank la maji yako, tengeneza mfumo wa kuingiza maji katika tank kupitia chamber maalum, mahali ambapo utaweza kudhibiti matakataka mengine(kuchuja). Na maji hayo yatoe kwa bomba au pump bila kufungua fungua tundu kuu la kupita wakati unafanya usafi wa tank.

Nakukaribisha kama una maswali, uliza.
 
weka chumvi kidogo, kama dumu la lita 20 weka chumvi nusu kijiko cha chai.
 
Mr.Mbilinyi nataka kujua huduma za kupima maji(nitrate) zikoje gharama,sehemu gani? mi nipo MORO
 
Niliwahi kusikia watu wakiongelea wakisema kuwa unaweka chlorite kidogo - ile dawa ya madoa sina uhakika ni kwa kipimo gani sasa sijui kama ni kweli ama la
 
mr.mbilinyi nataka kujua huduma za kupima maji(nitrate) zikoje gharama,sehemu gani? Mi nipo moro

nenda sokoine university of agriculture, idara ya soil science kuna maabara zilizoenda shule..
 
Back
Top Bottom