Anayeifahamu COASCO.... taarifa zake please.

MoneyMaker

Member
Jul 1, 2012
18
6
Wapendwa wanaJF,

Salamu.

Nimeitwa kwenye usaili COASCO wa Assistant Auditor. Ila kwa sasa ninafanya kazi sekta binafsi. Si ifahamu vizuri COASCO. Wakati naomba kazi nilikuwa sina kazi na ilikuwa mwezi wa tatu. So, kwa mdau yoyote anayefahamu COASCO ikiwemo malipo yao, naomba anijuze. Utakua umenisaidia kufanya maamuzi sahihi aidha kuondoka huku niliko au kubaki na kupunguza ushindani kwa wasailiwa wengine.

Ni hayo tu wanabodi.

Nawasilisha.
 
Kwa hiyo jamaa aliekupigia simu hakukuambia ofisi zinapatikana wapi? yaani hata code number ya simu iliyotumika hukuifahamu, Tangazo la kazi nalo halikuandika? wabongo tuache uvivu wa ku google, haya link hiyo http://www.ilo.org/public/english/employment/ent/coop/africa/download/coasco.pdf

Mr Suggestion, asante kwa link yako. Ila, sio kwamba sifahamu wanapatikana wapi. Ninachomaanisha hapa ni utaratibu wa kazi zao na malipo yao yakoje ili niweze kufanya maaumuzi ya aidha kuattend usaili Dodoma au laa hivyo kupunguza ushindani kwa wengine. So, kama unafahamu utaribu wao wa malipo na kazi, nijuze please.
 
MoneyMaker kama wewe ni professional basi unajua thamani yako ni ipi, mimi nikienda kwenye usaili wowote ule nitasema nipeni kiasi fulani zaidi ya hapo sikubaliani na hiyo ajira yao, wewe kwa sasa labda uulizie life ya Dodoma ikoje, namaanisha msosi, nyumba, matibabu na starehe garama zake kwa hapo mkoani zikoje, ndio utakuwa na wakati mzuri wa kuomba kiasi fulani cha mshahara.

Sina detail zaidi ya hizo mkuu
 
Asante Mkuu kwa ushirikiano wako.
Ubarikiwe.
 
naona wameita watu 417 kwa nafasi 11 is it fair kweli? jamaa bwana wanakatisha tamaa kinoma, anyaway nendeni mkajaribu
 
wakuu wametoa wapi hayo majina naomba kujuzwa jamani mm ni momoja ya watu waliomba au waliwapigia simu
 
kaka coasco ni shirikisho la ukaguzi la vyama vya ushirika,kazi yao ni kukagua vyama vya ushirika,sina uhakika na malipo yao ila kuna maslahi mazuri,nishafanya nao kazi walikuja kukagua vyama vyetu,mie ni afisa ushirika.

Asante Adolph kwa taarifa. Pamoja Mkuu.
 
naona wameita watu 417 kwa nafasi 11 is it fair kweli? jamaa bwana wanakatisha tamaa kinoma, anyaway nendeni mkajaribu

Yaani, we acha tu. Ndo maana najaribu kufahamu malipo yao ili niweze kufanya maamuzi sahihi. Si ajabu wametuita wengi ili kutoa lawama ilhali wana watu wao wamewaandaa tayari. A'way, ndo maisha yenyewe Mkuu Qulfayaqul.
 
duh hata mie nimeitwa, lkn mambo haya ni kama ya udom, watu 400 af wanataka 11 , rushwa lazma itembee
 
hawana tofautii na nssf watu 5000 wameitwa interview wamechukua 70 wanaowajua wao wote shenzi zao
 
kama una C.P.A kijana utalipwa take home kuanzia 1.5m,kama hauna take home inarange kati ya 800k hadi 1.2m,kila la kheri mkuu,hawa jamaa wana mipango mizuri hasa kama una C.P.A,nasikia wameingia mkataba na internatinal Organization fln i guess UN watakuwa wanawakagua hivyo watakaobahatika watasafiri sana nje ya nchi kupiga mzigo wa ukaguzi
 
Mkuu steveachi, asante kwa info. lakini mi nilisikia NAO (National Audit Office) kwa Utoh ndio walioingia mkataba na international organization, kumbe ni COASCO? Duh. kazi ipo. Ubarikiwe.
 
kama una C.P.A kijana utalipwa take home kuanzia 1.5m,kama hauna take home inarange kati ya 800k hadi 1.2m,kila la kheri mkuu,hawa jamaa wana mipango mizuri hasa kama una C.P.A,nasikia wameingia mkataba na internatinal Organization fln i guess UN watakuwa wanawakagua hivyo watakaobahatika watasafiri sana nje ya nchi kupiga mzigo wa ukaguzi

Usijichanganye National Audit na COASCO ni taasisi mbili tofauti steveachi
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli Mkuu Ndachuwa, mi nilisikia NAO kwa Utoh ndo waloingia mkataba na International organisation, sio COASCO. Mkuu steveachi, tunaomba ufafanuzi kidogo mkuu. Ubarikiwe.
 
Wapendwa wanaJF,

Salamu.

Nimeitwa kwenye usaili COASCO wa Assistant Auditor. Ila kwa sasa ninafanya kazi sekta binafsi. Si ifahamu vizuri COASCO. Wakati naomba kazi nilikuwa sina kazi na ilikuwa mwezi wa tatu. So, kwa mdau yoyote anayefahamu COASCO ikiwemo malipo yao, naomba anijuze. Utakua umenisaidia kufanya maamuzi sahihi aidha kuondoka huku niliko au kubaki na kupunguza ushindani kwa wasailiwa wengine.

Ni hayo tu wanabodi.

Nawasilisha.

Ni kama Auditing firm ila inajishughulisha na vyama vya ushirika tu especially SACCOS
 
COASCO - Kazi yao kubwa ni kubwa ni kukagua hesabu za vyama vya Ushirika. Ni taasisi ya umma na inafuata taratibu zote za Serikali. So, ukiajiriwa utakuwa mtumishi wa umma.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom