Ndugu zangu,
AFRIKA kuna mambo! Kuna picha niliyotundika jana bloguni; mjengwa.blogspot.com iliyozua mjadala mkubwa kuhusiana na matumizi ya Serikali na hususan matumizi ya viongozi waandamizi wa Serikali. Ni ni picha inayomwonyesha balozi wa Sweden nchini Tanzania, Lennart Hjalmaker alipokuwa safarini kuelekea Sweden akitokea Dar es Salaam.
Balozi huyo alionekana akiwa kwenye economy class. Nikaandika, kuwa katika nchi zetu hizi, katika ndege hiyo hiyo, yaweza kabisa kukawa na Waziri wa Serikali au hata Balozi wetu nje ya nchi ambaye amepanda Business Class yenye gharama kubwa huku anayechangia asilimia 40 ya bajeti yetu amepanda economy class. Naam. Nimeona kuwa huu ni mjadala wenye tija kwa nchi yetu na hususan katika kipindi hiki cha bajeti. Wengine mnasemaje?
Maggid,
Sweden,
Juni 11, 2011
http://mjengwa.blogspot.com