Anataka nianze kuishi nae kabla ya ndoa, hivi ndoto yangu yakuvaa shela itatimia kweli?

Si kuna mmoja alikuja kulia humu kaposwa kila kitu ila jamaa kaingia mitini miaka sijui mingapi unaweza kuta kuna mtu wake anamsubilia siku akiwa tayari huyo anayeyuka kama barafu
 
Kaa ukijua kuwa kutolewa mahari plus kutambulishwa sio kufunga ndoa, pili ndoa hailazimishwi na inavyoonekana mwenzio anataka kukuridhisha tu kwa kutoa mahari ila hayuko tayari kuoa
Hilo nalo neno
 
Huyo sio muoaji, anataka akufanye Single Mother
Bahati mbaya hata huyo mume ana watoto wawili kwa mama tofauti, halafu anataka amzalie kama alivyowazalisha wengine wawili na bado dada yetu anaomba ushauri! Sijui anataka ushauri gani wakati ana macho.

Nimekumbuka wimbo "bubu ataka kusema " wa Sikinde wakisema "mwenye mapenzi haoni, ingawa macho anayo! "

Vv
 
Hapo ndipo wadada mnapokosea umri ukisogea tu unaamua kiwa cheap hata kama ulijitunza kwa muda wote,umri wako ukusaidie kuamua kwa busara una uhakika gani kama hao aliozaa nao hakutumia mbinu hiyohiyo?mahari sio ndoa wala kutoa mahari hakuhalilishi kuwa mke,dini zote zina taratibu zake za ndoa kama hujazifuata hizo bado hujaingia kwenye ndoa hata kama mahari imetolewa uwe na msimamo wako na huyo mwanaume atalazimika kufunga ndoa ila ukiishi nae imekula kwako utatiwa mimba na ndoa itakuwa ikipigwa kalenda kila siku.
 
Ni upofu tu wa akili zetu ndoa sio maisha ya furaha kwa kuwa wanawake hutaka ndoa tu basi baada ya hapo sisi wanaume hurudi tena kutafuta wake woman vs wife ndio issue sasa wewe muache tu huyo na usijute na umri wako.
 
Back
Top Bottom