Analysis ya sherehe za miaka 35 ya ccm

Jamco_Za

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
1,330
195
Jamani angalie TBC1 hao wanaadhimisha miaka 35 viatu vibovu namna hiyo, shame on you CCM, mmenunua Tshirt kwanini hamkununua Suruali na Viatu hata yebo yebo kuficha aibu yenu.
 
hahahaha watu choka mbaya,cjui wamewakodi kutoka wapi!sungusungu hata fimbo inamshinda kubeba
 
halafu wamesombwa na malori katika barabara zenye mahandaki....sishangai kuwa katika hali hiyo!
 
Hebu badilisha heading yako! Unataka TBC waoneshe nin wakati hiyo ndio hali halis ya Mtanzani?
 
Mimi nadhani wamefanya vizuri kwani wamedhirisha kuwa maisha bora kwa kila mtanzania bado hayajapatikana na hakuna dalili ya kupatikana maana ni "malofa"
 
Maisha bora yanawezekana CCM ikiondolewa kabla ya uchaguzi mkuu, vinginevyo.....
 
Hebu badilisha heading yako! Unataka TBC waoneshe nin wakati hiyo ndio hali halis ya Mtanzani?
Walitakiwa wapige picha kwa juujuu, sasa wao wamekosea wakapiga mpaka suruali na viatu!
 
magamba bwana wanalaana sana yani hao sungusungu kupewa hizo tshirt ndo wameliza kabisa shame on them magamba
 
Hakuna marefu yasiyo na mwisho na mwisho! Hata ccm ina mwisho tuongeze bidii ya elimu ya uraia.
 
tabia hii ya kusomba walalahoi kutoka vijiji vya mbali kuja kujaza uwanja itawagharim sana magamba. hivi chadema huwa hawana siku ya kuzaliwa kwa chama chao? natamani siku hiyo iwepo rasmi ili magamba waone jinsi gani wananchi wanavyokuja wenyewe bila kurubuniwa!
 
RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kina hatari ya kuanguka vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ikiwa hali mbaya inayoendelea katika nchi haitarekebishwa.

Kauli hiyo ya kwanza ya aina yake, aliitoa saa chache tu baada ya kutamba kwamba CCM ina uhakika wa kurudisha nafasi zote za uongozi tangu za vitongoji hadi ubunge zilizonyakuliwa na upinzani katika uchaguzi mkuu uliyopita.

Akipokea maandamano ya matembezi ya wana CCM katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5 asubuhi, Kikwete aliwahakikishia waandamanaji hao kuwa chama hicho kimejizatiti kikamilifu na kina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, katika hotuba yake ndefu katika Uwanja wa CCM Kirumba majira ya mchana, Kikwete aligeuka na kukiri kuwa vyama vya upinzani sasa vina nguvu kubwa nchini inayotishia kukishinda chama hicho tawala katika uchaguzi mkuu ujao.

Kikwete alisema hali ya sasa ndani ya chama hicho haiwezi kuleta na kutetea ushindi wake katika chaguzi zijazo ikiwa viongozi wa juu wa CCM hawatachukua hatua za haraka za kuondoa misuguano mikubwa iliyopo.

Kuhusu kujivua gamba

Rais Kikwete katika hilo alisema, "Hivi karibuni nikiwa na NEC hapo Dodoma, nilitumia kauli ‘Nyoka Kujivua Gamba'. Usemi huo ulienezwa tofauti kabisa. Kimsingi tulipitisha maazimio mengi, lakini wenzetu wameona azimio moja tu la kujivua gamba.

Alisema hoja ya kujivua gamba iliyopitishwa na NEC mwaka jana si ya hovyo, hivyo kiongozi na mwanachama yeyote ndani ya CCM anayeuona uamuzi huo ni wa hovyo, basi yeye ndiye wa hovyo mbele ya jamii.

"Haiwezekani tukaendelea kuwa na watu wa hovyo, lazima chama kijipange na kujiweka sawa ili kisipoteze sifa kwa jamii," alisema Mwenyekiti huyo wa CCM, ambaye alipokea wanachama wapya wapatao 1,847.

Alikiri kuwa ajenda ya watu kujivua gamba imegonga mwamba na kuwatupia mzigo wanachama wake kuwawajibisha viongozi hao na wale wanaowaona hawaendani na maadili wala sera za chama hicho tawala.

Alisema maamuzi ya kujivua gamba hayakulilenga kundi ama watu fulani ndani ya CCM, bali linawahusu wanachama wote wanaojitambua kwamba si waaminifu kujiondoa wenyewe ndani ya chama kwa kuachia nyadhifa za kiuongozi.

"Wito wa kujivua gamba haujapewa mwitikio mzuri. Tumetupa mpira huo kwa wanachama kuwawajibisha viongozi hao, maana tunawafahamu. Sasa kazi kwetu sote," alisema Rais Kikwete.

Akwepa kuzungumzia mgogoro wa madaktari

Katika hali ya kushangaza, Rais Kikwete alishindwa kabisa kugusia suala zima la mgogoro wa madaktari ambao umelitikisa taifa kwa wiki mbili sasa, akisema atatafuta muda wa kulizungumzia sakata hilo.

Maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walishikwa na butwaa baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake bila kugusia jambo hilo.

Watu wengi walisikika wakilalamika na kushutumju vikali hali hiyo, huku mmoja wa watu waliokuwa uwanjani hapo alisikika akidai kuwa serikali ya CCM imejimaliza yenyewe.

Katiba mpya

Rais Kikwete aliwapongeza wabunge wa CCM kwa uamuzi wao wa kuitetea Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mpya 2011, na kwamba muswaada huo umeshawasilishwa tena bungeni, hivyo ataunda tume ya kukusanya maoni kwa Watanzania ambapo aliwaomba wana CCM kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao, maana muwamba ngoma huvutia kwake.

"Hili la Katiba mpya tumechukua mapendekezo ya vyama vya upinzani, kikiwemo CCM ambacho nacho kimetoa mapendekezo manane. Nawashukuru sana wabunge wa CCM katika hili, lakini wana CCM jitokezeni kwa wingi kutoa maoni yenu maana muwamba ngoma huvutia kwake."

Waandamanaji wasombwa kwa malori

Katika kile kilichoonekana kuwa nguvu ya CCM imepotea mjini Mwanza, chama hicho kililazimika kukodisha mabasi na malori maalumu tangu juzi kwa ajili ya kuwasomba watu wa kuhudhuria sherehe hiyo kutoka maeneo kadhaa ya ndani na nje ya Mwanza.

Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya watu waliohudhuria walikiri kuletwa kwa magari kutoka katika wilaya kadhaa za mkoa huo na wengine wakitoka mikoa jirani na Mwanza.

Pia katika juhudi za kupata watu wengi uwanjani hapo CCM inadaiwa kuwakodi vijana wengi wasio na kazi maalumu jijini hapa kwa kuwalipa ujira kidogo na kuwapatia fulana, kapelo za chama na chakula.

Imani za ushirikina zajitokeza

Wakati Rais Kikwete akiingia uwanjani hapo, kulijitokeza dalili za uwepo wa vitu vilivyoashiria nguvu za ushirikina, jambo lililoonekana kuwashtua wasaidizi wake wa Usalama wa Taifa.

Wasaidizi wake waliona chupa mbili zilizokuwa zimejazwa vitu vilivyodaiwa kuwa ni dawa za kishirikina, kisha mmoja wao akaipiga teke chupa moja.

Chupa hizo mbili za maji zenye ujazo wa lita moja na nusu, ziliwekwa upande wa kulia na kushoto wa zulia alilotandikiwa Rais kupita kwenda kwenda meza kuu.

Kinana ajuta

MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema kitendo cha kuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Jakaya Kikwete katika kipindi cha uchaguzi mwaka 2010, kimekuwa kitanzi kwake.

Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifunga maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama hicho, yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Buguruni.

Kwa mujibu wa Kinana, wananchi na wana-CCM wamekuwa wakitumia umeneja wake kumpatia kero nyingi ili azitolee majibu au kumpelekea Rais Kikwete.

Alisema katika ziara yake ya siku 10 mkoa wa Dar es Salaam, amekuwa akipokea kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Hata hivyo, alisema anatarajia kuziwasilisha kero zao kwenye Kamati Maalumu ili zijadiliwe.

Hali hiyo ilitokana na wakazi wengi wa mjini kuonekana kukisusia chama hicho na hivyo viongozi wake wakajawa na hofu ya kupata idadi ndogo ya mashiriki.

Majimbo ya Mwanza ambayo chama hicho kiliyapoteza kwa CHADEMA katika uchaguzi mkuu uliopita ni Nyamagana linaloongozwa na Ezekiel Wenje, Ilemela lililo chini ya Highness Kiwia na Ukerewe, linaloongozwa na Salvatory Machemli

Source: Tanzania Daima JK ahofia CCM kuanguka 2015
 
RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kina hatari ya kuanguka vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ikiwa hali mbaya inayoendelea katika nchi haitarekebishwa.

Kauli hiyo ya kwanza ya aina yake, aliitoa saa chache tu baada ya kutamba kwamba CCM ina uhakika wa kurudisha nafasi zote za uongozi tangu za vitongoji hadi ubunge zilizonyakuliwa na upinzani katika uchaguzi mkuu uliyopita.

Akipokea maandamano ya matembezi ya wana CCM katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5 asubuhi, Kikwete aliwahakikishia waandamanaji hao kuwa chama hicho kimejizatiti kikamilifu na kina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, katika hotuba yake ndefu katika Uwanja wa CCM Kirumba majira ya mchana, Kikwete aligeuka na kukiri kuwa vyama vya upinzani sasa vina nguvu kubwa nchini inayotishia kukishinda chama hicho tawala katika uchaguzi mkuu ujao.

Kikwete alisema hali ya sasa ndani ya chama hicho haiwezi kuleta na kutetea ushindi wake katika chaguzi zijazo ikiwa viongozi wa juu wa CCM hawatachukua hatua za haraka za kuondoa misuguano mikubwa iliyopo.

Maoni yangu

Kwanza namshkuru Rais kwa kuwa muwazi na kukiri kwa kinywa chake kuwa chama hicho kipo dhohofulihali na kama hakijajipanga upya, ushindi wa 2015 utakuwa ni ndoto. Nionavyo mimi Rais amechelewa sana kuitoa hii kauli, mimi nadhan ilibdi aitoe 2009, ila haina mbaya. Vyama vya upinzani hususani, CHADEMA. Jipangeni, zidisheni mashambulizi hasa maeneo ya vijijini ili kuwapanga wananchi mkao wa ushindi. Kamwe msije mkalewa sifa kuwa mpo vizuri.

Rai yangu kwa uongozi wa CDM chonde jamani pelekeni elimu vijijini,tutumieni miaka miwili hii kuwafikia wananchi wa vijijini. Mkitokea huko 2914/15 itakuwa ni too late. Mimi nipo tayari kujiunga kwenye huo msalagambo wa kwenda vijijini kueneza habari njema hasa huko maeneo ya kwetu. Aidha, kama fedha haitoshi fanyeni fundraising campaigns wanachama tuchangie. Suala la kuhimiza michango huwa halina mwisho, ni suala endelevu. Chama kisipo himiza na kukumbusha wanachama ni rahisi kwa mwanachama kusahau mwisho wa siku shughuli zinalala. Chadema tuna mtaji mkubwa sana wa wanachama wanaopenda kuona chama kinasonga mbele. Nashauri tumieni fursa hiyo. Wana CDM wenzangu nini kifanyike ili tuzidi kujidhatiti na kujipanga kwa ushindi 2015???

Source Tanzania Daima 06/02/2012
 
JK ahofia CCM kuanguka 2015
• Awashukia viongozi wenzake kwa undumilakuwili

na Mwandishi wetu

amka2.gif
RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kina hatari ya kuanguka vibaya katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, ikiwa hali mbaya inayoendelea katika nchi haitarekebishwa.
Kauli hiyo ya kwanza ya aina yake, aliitoa saa chache tu baada ya kutamba kwamba CCM ina uhakika wa kurudisha nafasi zote za uongozi tangu za vitongoji hadi ubunge zilizonyakuliwa na upinzani katika uchaguzi mkuu uliyopita.
Akipokea maandamano ya matembezi ya wana CCM katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5 asubuhi, Kikwete aliwahakikishia waandamanaji hao kuwa chama hicho kimejizatiti kikamilifu na kina uhakika wa kushinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao.
Hata hivyo, katika hotuba yake ndefu katika Uwanja wa CCM Kirumba majira ya mchana, Kikwete aligeuka na kukiri kuwa vyama vya upinzani sasa vina nguvu kubwa nchini inayotishia kukishinda chama hicho tawala katika uchaguzi mkuu ujao.
Kikwete alisema hali ya sasa ndani ya chama hicho haiwezi kuleta na kutetea ushindi wake katika chaguzi zijazo ikiwa viongozi wa juu wa CCM hawatachukua hatua za haraka za kuondoa misuguano mikubwa iliyopo.
Kuhusu kujivua gamba

Rais Kikwete katika hilo alisema, “Hivi karibuni nikiwa na NEC hapo Dodoma, nilitumia kauli ‘Nyoka Kujivua Gamba’. Usemi huo ulienezwa tofauti kabisa. Kimsingi tulipitisha maazimio mengi, lakini wenzetu wameona azimio moja tu la kujivua gamba.
Alisema hoja ya kujivua gamba iliyopitishwa na NEC mwaka jana si ya hovyo, hivyo kiongozi na mwanachama yeyote ndani ya CCM anayeuona uamuzi huo ni wa hovyo, basi yeye ndiye wa hovyo mbele ya jamii.
“Haiwezekani tukaendelea kuwa na watu wa hovyo, lazima chama kijipange na kujiweka sawa ili kisipoteze sifa kwa jamii,” alisema Mwenyekiti huyo wa CCM, ambaye alipokea wanachama wapya wapatao 1,847.
Alikiri kuwa ajenda ya watu kujivua gamba imegonga mwamba na kuwatupia mzigo wanachama wake kuwawajibisha viongozi hao na wale wanaowaona hawaendani na maadili wala sera za chama hicho tawala.
Alisema maamuzi ya kujivua gamba hayakulilenga kundi ama watu fulani ndani ya CCM, bali linawahusu wanachama wote wanaojitambua kwamba si waaminifu kujiondoa wenyewe ndani ya chama kwa kuachia nyadhifa za kiuongozi.
“Wito wa kujivua gamba haujapewa mwitikio mzuri. Tumetupa mpira huo kwa wanachama kuwawajibisha viongozi hao, maana tunawafahamu. Sasa kazi kwetu sote,” alisema Rais Kikwete.
Akwepa kuzungumzia mgogoro wa madaktari

Katika hali ya kushangaza, Rais Kikwete alishindwa kabisa kugusia suala zima la mgogoro wa madaktari ambao umelitikisa taifa kwa wiki mbili sasa, akisema atatafuta muda wa kulizungumzia sakata hilo.
Maelfu ya wananchi waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walishikwa na butwaa baada ya Kikwete kumaliza hotuba yake bila kugusia jambo hilo.
Watu wengi walisikika wakilalamika na kushutumju vikali hali hiyo, huku mmoja wa watu waliokuwa uwanjani hapo alisikika akidai kuwa serikali ya CCM imejimaliza yenyewe.
Katiba mpya

Rais Kikwete aliwapongeza wabunge wa CCM kwa uamuzi wao wa kuitetea Sheria ya Mabadiliko ya Katiba mpya 2011, na kwamba muswaada huo umeshawasilishwa tena bungeni, hivyo ataunda tume ya kukusanya maoni kwa Watanzania ambapo aliwaomba wana CCM kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao, maana muwamba ngoma huvutia kwake.
“Hili la Katiba mpya tumechukua mapendekezo ya vyama vya upinzani, kikiwemo CCM ambacho nacho kimetoa mapendekezo manane. Nawashukuru sana wabunge wa CCM katika hili, lakini wana CCM jitokezeni kwa wingi kutoa maoni yenu maana muwamba ngoma huvutia kwake.”
Waandamanaji wasombwa kwa malori
Katika kile kilichoonekana kuwa nguvu ya CCM imepotea mjini Mwanza, chama hicho kililazimika kukodisha mabasi na malori maalumu tangu juzi kwa ajili ya kuwasomba watu wa kuhudhuria sherehe hiyo kutoka maeneo kadhaa ya ndani na nje ya Mwanza.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya watu waliohudhuria walikiri kuletwa kwa magari kutoka katika wilaya kadhaa za mkoa huo na wengine wakitoka mikoa jirani na Mwanza.
Pia katika juhudi za kupata watu wengi uwanjani hapo CCM inadaiwa kuwakodi vijana wengi wasio na kazi maalumu jijini hapa kwa kuwalipa ujira kidogo na kuwapatia fulana, kapelo za chama na chakula.
Imani za ushirikina zajitokeza

Wakati Rais Kikwete akiingia uwanjani hapo, kulijitokeza dalili za uwepo wa vitu vilivyoashiria nguvu za ushirikina, jambo lililoonekana kuwashtua wasaidizi wake wa Usalama wa Taifa.
Wasaidizi wake waliona chupa mbili zilizokuwa zimejazwa vitu vilivyodaiwa kuwa ni dawa za kishirikina, kisha mmoja wao akaipiga teke chupa moja.
Chupa hizo mbili za maji zenye ujazo wa lita moja na nusu, ziliwekwa upande wa kulia na kushoto wa zulia alilotandikiwa Rais kupita kwenda kwenda meza kuu.
Kinana ajuta
MJUMBE wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema kitendo cha kuwa Meneja wa Kampeni wa Rais Jakaya Kikwete katika kipindi cha uchaguzi mwaka 2010, kimekuwa kitanzi kwake.
Alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati akifunga maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa chama hicho, yaliyofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Buguruni.
Kwa mujibu wa Kinana, wananchi na wana-CCM wamekuwa wakitumia umeneja wake kumpatia kero nyingi ili azitolee majibu au kumpelekea Rais Kikwete.
Alisema katika ziara yake ya siku 10 mkoa wa Dar es Salaam, amekuwa akipokea kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.
Hata hivyo, alisema anatarajia kuziwasilisha kero zao kwenye Kamati Maalumu ili zijadiliwe.
Hali hiyo ilitokana na wakazi wengi wa mjini kuonekana kukisusia chama hicho na hivyo viongozi wake wakajawa na hofu ya kupata idadi ndogo ya mashiriki.
Majimbo ya Mwanza ambayo chama hicho kiliyapoteza kwa CHADEMA katika uchaguzi mkuu uliopita ni Nyamagana linaloongozwa na Ezekiel Wenje, Ilemela lililo chini ya Highness Kiwia na Ukerewe, linaloongozwa na Salvatory Machemli

Katika sherehe za ccm zilizofanyika leo huko katika viwanja vya ccm kirumba jijini mwanza na kuonyeshwa na star tv zaidi ya watu wanaokaribia 100,000 walihudhuria sherehe hizo (kutokana na vyanzo vya habari humu jamii forum na pia makisio). idadi hii ni kubwa zaidi ya uwezo wa uwanja huo ya kuchukua idadi ya watu isiyozidi 20,000. hivyo basi natarajia kufungua kesi dhidi ya mwenyekiti wa ccm, Nape nnauye na ccm. hii ni kutokana na kuhatarisha usalama wa watu waliohudhuria sherehe hizo kwa kuzidisha idadi ya watu waliohudhuria zaidi ya uwezo wa uwanja huo ambayo ni mara tano ya zaidi ya idadi inayotakiwa jambo ambalo lingeweza kusababisha maafa makubwa ikiwa kuna jambo baya lingetokea. Tukio hili linashabihiana na ajali ya mv spice icelander iliyozidisha idadi ya watu na kupata ajali huko nungwi zanzibar ambapo wamiliki wa meli hiyo wana kesi ya kujibu mahakamani , pia inashabihiana na tukio la mv bukoba. ingawa hakuna jambo baya lililotekea lakini ni lazima tujue kuzidisha idadi ya watu ni kosa kisheria. Nakaribisha maoni/mchango katika kuhakikisha wote waliohusika wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya dola na kupelekwa mahakamani kujibu mashitaka yao.
 
"Wito wa kujivua gamba haujapewa mwitikio mzuri. Tumetupa mpira huo kwa wanachama kuwawajibisha viongozi hao, maana tunawafahamu. Sasa kazi kwetu sote," alisema Rais Kikwete.

Kauli hii ina hatari ya kupewa tafsiri mbaya na umma kiasi cha kuwafanya pengine baadhi yao kutokuwa wavumilivu kusubiria mwaka 2015, ba badala yake kuchukua maamuzi mkononi na kuleta uvunjifu wa amani. Tunaombea hali isifike huko.
 
Back
Top Bottom