Anaapa kukilinda chama cha kijani

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Feb 13, 2013
1,796
1,350
Tuko kwenye msiba jamaa kafiwa na mkewe aliyefariki akijifungua kwa kutokwa na damu nyingi na kukosa huduma kwa wakati kwa kutokuwa na vitendea kazi hospitalini. Mwaka jana marehemu mkewe alipoteza kichanga kwa ukosefu wa dawa hospitalini. Tonaongea siasa, cha ajabu anashabikia CCM mpaka machungu ya kufiwa anayasahau.

Tuko na Baba yake mstaafu, muda tu alikuwa analalamika mafao anazungushwa mwaka wa saba, tunamsikitikia lakini bado anaona CCM kwamba ndiyo suluhisho lake. Inasikitisha sana.

Kaka wa marehemu, shemeji ya jamaa yangu ni Askari Polisi mwaka wa 21, analalamika ameshindwa kusomesha watoto kipato kidogo, mikopo hapati, vyeo vinapanda kwa kujuana. Mpaka leo hata kibanda cha nyasi kijijini kwao tabu. Cha ajabu anasema CCM ndiyo wanafaa kuongoza sio wapinzani, mpaka leo hajashtuka na wanategemea ukombozi.

Wadogo zake wawili wanalia sana kwa kusikitika kuondoka kwa shemeji yao ambaye amekuwa akiwalea kama mama yao. Walifaulu darasa la saba ingawa hawajui kusoma na kuandika, matokeo yake hata sekondari waliyochaguliwa kwenda wanaogopa kwenda kwa kutokuwa na mahitaji ya shule na kuogopa aibu kwani wanajua fika hawataelewa kitu.

Mjomba wake marehemu ni mwanajeshi, yeye anashangaa wanavyotaka kutumiwa kuibakisha CCM madarakani ingali kama yeye ameichoka na ameapa kufuata sheria inavyomtaka, pasipo kufanya kinyume na kiapo chake cha kazi.

Anaungwa mkono na dada yake Jamaa aliyekuja kumzika wifi yake na kuwashangaa wanaoshabikia CCM ambayo walikaa viongozi wa awamu tatu kwa pamoja kwa maana ya miaka 30 kutoa ahadi zile zile ambazo hazitekelezeki, bado wapigie CCM kura miaka mingine 10 kwa maisha yale yale tena kwa kuendelea kupata misiba zaidi wakati viongozi ambao ni wale wale na familia zao wanatibiwa nje, watoto wao wanasoma Nje na wanataka waendelee kuzalisha vizazi ambavyo vitaendelea kuwa tegemezi kwao na familia zao.

Amewaomba wabadirike hata kwa kuwajaribu wapinzani tuone wataleta mabadiliko gani. Vile vile siku ccm ikitoka madarakani nguvu zinaamia kwa wananchi kama kutatokea chama chochote kuingia madarakani na kushindwa kuwahudumia wananchi wanakitoa. Hapo ndipo tutakuwa na viongozi wawajibikaji kwa wananchi, lakini kwa mfumo huu huu tutazikana saana hata kwa vifo vinavyo hepukika.

Nikaona jamaa akalia sana kwa uchungu wa kuondokewa na mkewe kana kwamba ndiyo kapata habari wakati huo. Maskini kwa sauti ya masikitiko akakumbuka mstari mmoja kwenye Biblia usemao " watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa".

Mara kwa sauti moja wakasikika wakisema kweli mabadiliko yanahitajika na kuanzia hapo hawataki kusikia neno CCM. Ananukuliwa akisema "tutafute mabadiliko kwa amani ingawa sasa naona kabisa wale watakao Fanya yasiwezekane kwa amani hayata hepukika kivinginevyo".

Kwa pamoja tutafute MABADILIKO, tuondoe UONGOZI WA KUPOKEZANA pasipo MAFANIKIO.

Ukitafakari sana mtu anayeshabikia sana CCM ni mtu tegemezi na wale ambao wana position fulani kwenye serikali na taasisi zake. Bila kusahau wanao kaa kwa shemeji zao na wapiga mizinga wasiopenda kufanya kazi kwa maana ukiingia utawala mpya watalazimika kufanya kazi na bila kusahau mamarioo.

Tafakari kwa kina utaliona hili.
 
Stori nzuri.nadhani uombe tu contacts za shigongo tukuunganishe sio kuongea tu kama mbweha
 
Wenye akili wataelewa wavivu wakufikiria watazomea nakysema hovyo. Hii ni hali halisi katika picha
 
Back
Top Bottom