Amri ya Mahakama Kuu iliyofanya VIP Engineering kulipwa Fedha zake

Hukumu ya mahakama iko wapi hapo? Hakuna hukumu ya mahakama hapo, bali makubaliano ya two parties ambayo yaesajiliwa na mahakama kupata nguvu za kisheria.
Hakuna hukumu ambayo huwa haina submissions, arguments za two parties, argument ya mahakama na decision.

Inabidi urudi darasani kusoma sheria na kuelewa maana na nguvu ya Consent Settlement Order. Kwa faida yako hiyo ni amri iliyotokana na usuluhishi wa mahakama. Isome vizuri Amri hiyo na ujue maana yake!
 
Mahakama iliamuru VIP alipwe pesa zake zilikotoka si suala la VIP kwani yenyewe ilitakiwa ilipwe pesa zake kwa mujibu wa mkataba na hata muda wa malipo na kodi vyote vimetajwa katika Amri hiyo. Na hiyo ndiyo amri ya Mahakama na siku zote hakuna anayeizungumzia Amri hii na watu wanaaminishwa kuwa VIP kashiriki katika ukwapuaji wa fedha hizo! Aibu mbona aibu!

kinachonishangaza watu wanadai fedha zirudishwe lakini hawataji kuwa first entity kupokea fedha ilikuwa TRA! sisikii wakisema TRA irudishe pesa, kamishna wa TRA akamatwe, afilisiwe...n.k, wanakwenda straight to Tibaijuka!
 
Soma hukumu Mahakama na usichanganye mambo. Hakuna neno escrow katika uamuzi huo. Wakuulizwa ni PAP hizo pesa ilizipata wapi na si VIP!

Jibu swali nililokuuliza. Nimekuuliza hivi: mahakama iliamua kuwa VIP ilipwe pesa zake na PAP na kwamba malipo yatoke kwenye account ya Escrow?

Halafu nani kakwambia kuwa hiyo ni hukumu? Hiyo uliyoweka hapo ni matokeo ya mediation iliyofanywa kati ya VIP na PAP kwa msaada wa mahakama. Order yenyewe inasema wazi kabisa, wewe unadanganya ni hukumu.

Usitake kuwadanganya watu hapa. Hiyo siyo hukumu aka judgment bali consent settlement order. Kasome kwanza ujue maana yake au muulize aliyekupa hiyo order akupe ufafanuzi wa kisheria.

Judgment na consent settlement order ni vitu viwili kabisa. Tofauti na judgment, consent settlement order ni makubaliano ya pande mbili bila kukubali kosa.

Hapa pande zote mbili zinaingia katika makubaliano na mahakama ina-supervise makubaliano hayo kwa kutoa hiyo consent settlement order.

Judgment inam-bind kila mtu lakini consent settlement order inawa-bind waliokubaliana yaani VIP na PAP. Hata heading ya hiyo document haisemi kuwa Judgment bali ni Consent Settlement Order. And probably ndo maana hiyo consent settlement Order ilikuwa disposed without involving the other parties.

Sasa wewe unataka tuwe-bound na makubaliano binafisi kati VIP na PAP kisa tuu yalikuwa supervised na mahakama. It is merely a consent order ambayo PAP na VIP wamekubaliana jinsi watakavyolipana.

Hakuna sehemu order inasema kuwa mahakama imeamuru PAP imlipe VIP, bali wao wenyewe ndo wamekubaliana chini ya uangalizi wa mahakama walipane kivipi.

Kwa hiyo, kulikuwa hakuna haja ya PAC ku-refer hayo makubaliano binafisi kati ya VIP na PAP.

Nenda kajipange upya urudi, vingenevyo hii consent settlement order ilitakiwa kuwa confidential kati ya wahusika (VIP na PAP), but thank you anyway kwa kutupa hints jinsi huu mchezo ulivyochezwa.

cc Kimbunga

Ndugu, wewe ni Mwanasheria Rugemeleza Nshala?

Mwanzoni sikuelewa kwa nini umeuliza hili swali.

Ila baada ya kusoma hiyo document ndo nikaelewa kwa sababu kama aliyeanzisha hii thread ni mwanasheria, then atakuwa ni "mwanasheria asiye msomi", just in case kama huwa kuna the so-called "mwanasheria msomi".

cc Nyani Ngabu.
 
Unaweza kuelezea uharamu wa fedha alizolipwa Ruge? Au sumu ya kina Zitto na wahuni wenzake imekuingia sana?
labda nami nikujibu kwa swali hili, ruge alilipwa pesa hiyo na nani? Na je huyo aliyelipa hiyo pesa alitoa wapi? Msidhani kwamba watanzania wa siku hizi ni walewale wa mwaka 47. Naomba jibu hayo maswali halafu kisha nitaendelea.
 
mkuu kuna ishu nyingine naomba nikuulize, nilisoma kuwa PAP walimpa Rugemalira advance ya $7mil before PAP kuchukua IPTL(na escrow account). Is this true?

Walilipa $7.5milioni na wakataka kutokomea na Rugemalira akawafungulia kesi ya kudai kutekelezwa kwa mkataba mnamo tarehe 8 Januari 2014 ambayo ndiyo ilisababisha Amri hii ya maridhiano. Rugemalira alikataa kutapeliwa na akapigania haki zake leo hii anaitwa kila aina ya tusi kana kwamba mtu kukataa kutapeliwa ni kosa kubwa!
 
Uharamu wake ni upi wakati mahakama imeamua alipwe fedha zake na PAP na ndivyo ilivyofanywa? Je ndugu yangu umesoma Amri ya Mahakama Kuu na kuielewa au unaamua kuwa mbishi kama mshipa?
kiujumla sijaisoma hiyo amri, lakini naomba wewe utusaidie hapa, je rugemalila alilipwa na PAP hiyo pesa sawa! Je PAP hiyo pesa unafahamu alikoitoa? Pesa aliyopewa ruge ni haramu kwa sababu Haikupaswa kutoka Bot na kupewa PAP/IPTL. Kama mahakama iliamuru ruge apewe pesa ambayo haikustahili kutoka bado ni haramu.
 
Ndugu Rugemeleza, swali langu ni moja tu. Unaweza kuniambia ni kifungu kipi kilichosema kuwa Singa singa achukue hela iliyokuwa kwenye Account ya Tegeta Escrow ili atumie kulipia manunuzi ya hisa 3 za VIP Engineering. Kama ukishindwa kunielewesha, basi hata wewe ni mpotoshaji mkubwa kwa maslahi yako binafsi.
 
Hukumu ya mahakama iko wapi hapo? Hakuna hukumu ya mahakama hapo, bali makubaliano ya two parties ambayo yaesajiliwa na mahakama kupata nguvu za kisheria.
Hakuna hukumu ambayo huwa haina submissions, arguments za two parties, argument ya mahakama na decision.

Hahahahahaa.

Na wewe umeshtukia eh?

Jamaa anataka kuwajaza ujinga Watanzania.

Akajipange upya.
 
Sasa kama uliiona kwanini mkaamua kupindisha ukweli na kuwahukumu wasiohusika na kuwaacha wezi huru? Aibu kwako wewe uliyekufa dhamira.
haa haa, naona mmeamua kutetea wezi wa upande mmoja! Wale waliogawana pesa mkombozi benki nao ni wezi, wale waliochukua stanbic kwenye sandarus pia ni wezi. Hatuwezi tetea wezi waliowekewa kwenye akaunti zao pale mkombozi benki kamwe. Wizi ni wizi tu.
 
1. tunarudi pale pale uharamu unaosema wewe ni kuwa PAP sio mmiliki halali wa IPTL, sasa ikiwa ni hivyo nani ni mmiliki halali wa IPTL? Standard chartered not so?
2. Assuming fedha zimekwapuliwa na PAP asiye mmiliki halali, je Rugemalira ana kosa gani kwa kuuza hisa zake? kuna uchunguzi wowote umefanyika kubaini kuwa thamani za hisa zake ilikuwa inflated kutakatisha fedha? Au kuna utata katika hisa za Rugemalira ndani ya IPTL as well? Nini hoja hasa ya Rugemalira kuwa mkosaji katika hili? Hivi assuming Sethi angenunua kiwanja, tungemuandama aliyeuza kiwanja au tungeshikilia kiwanja?

Mimi sio mwanasheria, ni MTZ tu wa kawaida ninayefuatilia sakata hili kama wengine. Ninachojua mimi, IPTL ilikuwa na wenyewe wa Malaysia (Nilikuwa mmoja wa waliopinga uwekezaji huu kuwa ni wa kinyonyaji na ulikuwa na mizengwe mingi sana ulipoanzishwa. Hata wahisani wetu wakati ule waliupinga na kuonyesha, kimahesabu, kwa nini hautoi "thamani kwa fedha"). Hii kampuni ililuwa ni Mechmar (kama nitakuwa sahihi..). Mbona jina lake limepotea kwa sasa? Huyu Ruge anajua ukweli kwani yeye alikuwa ndiye mwekezaji mzawa walioshirikiana na Mechmar kuanzisha IPTL. Ilikuwaje Mechmar kuhamisha hisa kwenda PAP ndio matatizo. Kwa hiyo, wewe, kama ni mwanasheria wa Ruge au ndiye mwenyewe, unatuhangaisha tu hapa. Tafuta au tueleze ilikuwaje umiliki wa IPTL kuhama hama bila yeye kujua na kuja kudai haki yake baadaye.
 
Inabidi urudi darasani kusoma sheria na kuelewa maana na nguvu ya Consent Settlement Order. Kwa faida yako hiyo ni amri iliyotokana na usuluhishi wa mahakama. Isome vizuri Amri hiyo na ujue maana yake!
Kwa hiyo hiyo ni hukumu? Kwa hiyo maana ya consent settlement order ni hukumu? Huoni hayo ni makubaliano ya pande mbili. Huelewi kitu kakz
 
Ndugu yangu,

Ninachukia wale wanaotuona WaTZ ni wajinga miaka 53 baada ya Uhuru. Mbona unazungumzia matawi na husemi mizizi? Msingi wa yote haya ni kuwa PAP ni kampuni feki. Pia PAP na IPTL ni mtu huyo huyo kama makaratasi yanavyoonyesha, ingawa kisheria, IPTL ilishafilisika na kwa mujibu wa sheria za kimataifa, Standard Chartered (Hong Kong) ndiyo inayohitajika kuwakilisha matakwa ya IPTL (mdeni sugu aliyeshindwa kulipa deni). Accordingly, mauzo ya share za IPTL to PAP ni kiinimacho.

  • Kwa maelezo hayo, hata hiyo kesi iliyoamuliwa na jaji huyo haikutakiwa kuwepo. Tunaweza kuhisi kuwa malipo yaliyofanywa kwa majaji kutoka Mkombozi Bank ni hongo (Unless unatuambia walifanya kazi gani ya VIP au IPTL ili kuhalalisha malipo makubwa kiasi kile)
  • Katika kesi hiyo, VIP na IPTL wanawashitaki PAP na serikali. Kwa hiyo mkono wa kulia unaushitaki mkono wa kushoto kwa kuunyang'anya donge bila fidia??????
  • Kwa uelewa wangu, mawaziri na wengine waliopo kwenye orodha ya malipo hawawajibishwi kwa kupokea pesa bali kwa kushindwa:

  • Kushindwa ku-declare payments kama inavyotakiwa na tume ya maadili (wakiwa viongozi wa kitaifa)
  • Kushindwa kueleza kazi gani wamefanya ya VIP na kustahili kupewa malipo hayo (Unaomba mchango wa kusaidia shule unapewa pesa za kujenga shule nyingine mpya mbili, halafu unataka kutuambia ni "kamchango" kama vile ametoa laki mbili)
  • Kwa nini wote walioko kwenye orodha wana uhusiano na sekta ya nishati (katika nyakati tofauti) na walishika nyadhifa za juu serikalini
  • Mbona sioni ushahidi wa mgogoro wa TANESCO na IPTL kutatuliwa kabla ya PAP/IPTL kuchota fedhaza Escrow. Tuonyeshe kwanza ushahidi wa usuluhishi wa hili tatizo lililosababisha kufunguliwa account ya Escrow kabla ya utetezi wako huo. (Hii hatua ndiyo ingeonyesha kipi ni cha serikali na kipi ni cha IPTL na kufunga mjadala!
  • Ushahidi wowote wa mahakama katika jambo hili una mashaka ya kuaminika kwa kuwa kuna harufu ya rushwa kwenye mhimili huu.
  • Utatusaidia sana kama ungeshusha orodha ya wote waliopokea fedha kutoka StanBic ili nao tuwashughulikie kisheria. Hata kama ni Raisi kwani sisi wananchi tunajua ya kufanya kama kutakuwa na kiburi cha watawala.
Naomba sana, sana, sana msitufanye waTanzania ni wajinga. Wewe na wahusika wengine (Mawaziri, majaji, wabunge, maaskofu, na wengineo wote waliohusika kwenye mchakato wa kuzitoa na waliopokea pesa za Escrow) mnyamaze na sisi tuangalie serikali itafanya nini na ninyi nyote. kama kutakuwa na hatua za kisharia, mkajitetee mahakamani (Sijui mahakama ipi kwani ningekuwa mimi ningeomba international courts kwani internal courts zimeshakuwa compromised).

Ahsante sana

nimependa post yako.crugemereza unamtetea apa?ungekuja na orodha ya waliopata mgao stanbic apa ungeonekana shujaa. kwa upuuz huu na mween n rugemereza nakutakia xmas mbaya na mween nakutakua xmas njema ili tuanze mwaka mpya kwa kushughulikia awa wezi
 
Inabidi urudi darasani kusoma sheria na kuelewa maana na nguvu ya Consent Settlement Order. Kwa faida yako hiyo ni amri iliyotokana na usuluhishi wa mahakama. Isome vizuri Amri hiyo na ujue maana yake!

Wewe umesema ni hukumu. Refer maandiko yako ya nyuma.
 
Jibu swali nililokuuliza. Nimekuuliza hivi: mahakama iliamua kuwa VIP ilipwe pesa zake na PAP na kwamba malipo yatoke kwenye account ya Escrow?

Halafu nani kakwambia kuwa hiyo ni hukumu? Hiyo uliyoweka hapo ni matokeo ya mediation iliyofanywa kati ya VIP na PAP kwa msaada wa mahakama. Order yenyewe inasema wazi kabisa, wewe unadanganya ni hukumu.

Usitake kuwadanganya watu hapa. Hiyo siyo hukumu aka judgment bali consent settlement order. Kasome kwanza ujue maana yake au muulize aliyekupa hiyo order akupe ufafanuzi wa kisheria.

Judgment na consent settlement order ni vitu viwili kabisa. Tofauti na judgment, consent settlement order ni makubaliano ya pande mbili bila kukubali kosa.

Hapa pande zote mbili zinaingia katika makubaliano na mahakama ina-supervise makubaliano hayo kwa kutoa hiyo consent settlement order.

Judgment inam-bind kila mtu lakini consent settlement order inawa-bind waliokubaliana yaani VIP na PAP. Hata heading ya hiyo document haisemi kuwa Judgment bali ni Consent Settlement Order. And probably ndo maana hiyo consent settlement Order ilikuwa disposed without involving the other parties.

Sasa wewe unataka tuwe-bound na makubaliano binafisi kati VIP na PAP kisa tuu yalikuwa supervised na mahakama. It is merely a consent order ambayo PAP na VIP wamekubaliana jinsi watakavyolipana.

Hakuna sehemu order inasema kuwa mahakama imeamuru PAP imlipe VIP, bali wao wenyewe ndo wamekubaliana chini ya uangalizi wa mahakama walipane kivipi.

Kwa hiyo, kulikuwa hakuna haja ya PAC ku-refer hayo makubaliano binafisi kati ya VIP na PAP.

Nenda kajipange upya urudi, vingenevyo hii consent settlement order ilitakiwa kuwa confidential kati ya wahusika (VIP na PAP), but thank you anyway kwa kutupa hints jinsi huu mchezo ulivyochezwa.

cc Kimbunga

Mwanzoni sikuelewa kwa nini umeuliza hili swali.

Ila baada ya kusoma hiyo document ndo nikaelewa kwa sababu kama aliyeanzisha hii thread ni mwanasheria, then atakuwa ni "mwanasheria asiye msomi", just in case kama huwa kuna the so-called "mwanasheria msomi".

cc Nyani Ngabu.
mkuu thank you for all umemaliza!
 
Mbona kuna kitu kinanichanganya hapo:Rugemarila ana position gani kwenye first applicant company?

kuna issue ya kwamba PAP haikuwa na usajili. Kwa hiyo kila kitu kilichofanyika PAP ikiwemo ni null and void ab initio. PAP haijawahi ku exist as a legal personality. Hili linanichanganya kidogo. Kama PAP haikuwahi kuwa na usajili huko kwao imekuwaje ikasajiliwa hapa nchi? Sheria inataka kampuni ya nje inayokuja kusajiliwa hapa iambatanishe nyaraka za kuonyesha kwamba huko inakotoka imesajiliwa. Je PAP ilileta nyaraka za kughushi ama jamaa zetu wa BRELA nao wamo?
Angalia clause 12. Au point no 12. Ya hukumu!
 
Ndugu Rugemeleza, swali langu ni moja tu. Unaweza kuniambia ni kifungu kipi kilichosema kuwa Singa singa achukue hela iliyokuwa kwenye Account ya Tegeta Escrow ili atumie kulipia manunuzi ya hisa 3 za VIP Engineering. Kama ukishindwa kunielewesha, basi hata wewe ni mpotoshaji mkubwa kwa maslahi yako binafsi.

Hiyo consent settlement order isingeweza kusema hivyo kwa sababu inajumuisha makubaliano yaliyofikiwa kati PAP na VIP na kushughudiwa na mahakama ili yapate nguvu ya kisheria kati PAP na VIP tuu na siyo watu wengine.

Kwa maana nyingine kama hiyo order ingekuwa na kifungu kuwa PAP ichukue fedha kutoka Account ya Escrow kulipia manunuzi ya hisa 3 za VIP, basi hayo yangekuwa ni makubaliano yao wenyewe.
 
Ndugu Rugemeleza, swali langu ni moja tu. Unaweza kuniambia ni kifungu kipi kilichosema kuwa Singa singa achukue hela iliyokuwa kwenye Account ya Tegeta Escrow ili atumie kulipia manunuzi ya hisa 3 za VIP Engineering. Kama ukishindwa kunielewesha, basi hata wewe ni mpotoshaji mkubwa kwa maslahi yako binafsi.
mkuu wametumana kuja kupima upepo hapa jf, ukweli unabaki palepale, pesa aliyopewa ruge ni haramu, japokuwa alilipa kodi.
 
Mleta mada unapaswa uelewe kuwa case iliyozungumziwa hapo ni ya shares walizouziana na haikuhusu kabisa pesa za escrow account ambazo mgogoro wake haukuhusiana kabisa na hisa za VIP na PAP wala IPTL. Escrow ilihusu mgogoro wa namna ya kukokotoa tozo za capacity charge kati ya tanesco na IPTL. Acha kuchanganya madesa. Huko ni kumezeshwa vibaya na kuanza kuongea hadharani pasipo kuelewa msingi wa jambo unaloliongelea. Hii ni hatari sana.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Back
Top Bottom