Amir Jamal aliyekuwa Waziri wa Fedha

Hivi Mobutu Sesseseko alizikwa wapi? si alikuwa ni Mzaire huyu Mzee?
 
Wanabodi,

Binadamu yeyote ni mbinafsi by nature, na level ya ubinafsi inategemea mazingira mtu aliyokulia pia. Mjadala huu unavyoendelea tunaona mitazamo binafsi. Kila mmoja wetu leo hii, akiwa na nafasi bora serikalini, wazo la kwanza litakuwa binafsi ya huyo mtu, wengine binafsi zao huziweka "pending" kusikilizia jamii inayomzunguka itasema nini juu ya nafasi aliyojaliwa. (huyo si mchoyo hana roho ya korosho but still ana ubinafsi ambapo akipata mwanya tu atatimiza malengo ya ubinafsi), wa pili ni kuna mbinafsi na mwenye choyo huyu hasikii wala haambiwi!!, kwa kifupi wote hawa ni hatari, cha muhimu ni kuwa MAKINI na kila mmoja wetu anayepata nafasi bora serikalini, kwani kila mmoja wetu ana ajenda yake ya siri ambayo ni UBINAFSI.

Mjadala huu hautaishia kwa Marehemu A.Jamal tu, bali utaendelea kwa akina
1. Al-Noor Kassam
2. Col.Kinana
3. Rugumyamheto
4. Ntukamaazina
5. Rage
6. Marehemu Bryson
7. YUSUPH MANJI (dealer/agent wa biashara za serikali)....for NEXT TOPIC
8. Z Meghji, Rostam nk nk nk na sasa Salim A Salim

Ni kweli inauma sana kuona kuna vijana wengi sana wamepitia education system yetu BURE wakati huo wakijiita waTZ, halafu baadaye wametukimbia kurudi nchini mwao. But the question is, Je serikali yetu imeweza ku-absorb watu wake wwote waliowasomesha?? NO, kwa hiyo hao hawana tofauti na waTZ (wasomi) walio nje kwa hivi sasa, kwani walipata opportunity (coincidentally wengine nchi zao za asili) na kuzitumia.

Kupima uzawa wa mtu ni NEXT TO IMPOSSIBLE, kuna wazawa wengi tu wameiuza nchi kwenye madeni meeengi sana kwenye mikataba ya hovyo.

JKN naamini aliwatumia akina Jamal, Kassam na wengine kwakuwa hakuwa na watu, na kwa kuwa hawa jamaa walikuwa very loyal kwake basi aliendelea nao.

Nchi yetu ina uhuru wa kimawazo na kiitikadi pia. Hatuwezi kuiga Kenya au Uganda pasipo na kuwa na sababu za msingi, kwani tuna uhuru wa kujiendesha na kujiamulia mambo yetu wenyewe. Kama CCM mwaka jana wangemsimamisha SAS leo hii, tungekuwa tunazungumza mengine hapa.

Waafrika tujiheshimu kwa kulinda maslahi yetu kutokana na rasilimali zetu(and not otherwise), sio kuuza kila rasilimali yetu kwa faida ya wachache huku wananchi wetu wanaendelea na shida

Wanabodi tuendelee kuweka/kuandika mikakakati ya kulinda na kuinua maslahi yetu, uhuru wetu na uchumi wetu wa Taifa TANZANIA, hayo mengine yanahitaji mikakati ya UDHIBITI tu.
 
Washikaji, huu mjadala unafurahisha. Watanzania tujifunze kutofautisha kati ya sura, tabasamu, rangi, na mawazo yaliyo kichwani mwa mtu au itikadi na asili ya mtu. Bill Clinton na Bintie Condoleza Rice wote ni Wamarekani wa kuzaliwa. Tofauti Clinton ni mtishi na bi Rice ni mweusi. Wote wawili walishika nyazifa tofauti. Wamarekani weusi wangefurahia sana kupata mwenzao katika madaraka ya juu ya serikali ambaye ni Rice. Bahati mbaya, wamarekani weusi wanampenda sana Clinton kuliko wanavyompenda Rice mweusi mwenzao. Hata ukawaweka katika nafasi ya kugombea uraisi wa watu weusi peke yao wa marekani, Clinton na umarekani weupe wake atamshinda Rice umarekani weusi wake miongoni mwa wamarekani weusi, siyo kwa sababu ya utofauti katika umaarufu wao, bali kwa sababu ya utofauti katika itikadi na sera wanazozisimamia. Wote ni wamarekani wa kuzaliwa.

Joe Slovo alizaliwa Lithunia na wazazi wake walihamia Afrika kusini akiwa na umri wa miaka nane. Hakuwa mweusi, lakini alipata uraia wa Afrika kusini. Aliusumbua utawala wa makaburu kuzidi viongozi wengi unaowaona sasa hivi wanagombania madaraka. In fact, yeye ndiye aliyebuni mfumo wa utawala ambao ulikuja kukubaliwa kabla ya uchaguzi huru wa Afrika kusini. Kabla hajafa, alikuwa waziri wa mambo ya nyumba katika serikali ya Mandela. Aliendeleza itikadi yake ndani ya utawala serikali ya umoja. Hata baada ya weusi kuchukuwa madaraka, alionya na kusema "haitakuwa na maana kama weusi watashika madaraka wakati wazungu bado wana nguvu za uchumi".

Marehemu Kambona alipotoka London aliwataja Jamal, Kawawa, na Nyerere kuwa wana fedha nyingi nchi za nje. Nyerere hakujitetea yeye, bali alimponda Kambona kwa kuwapakazia watu safi. Hata katika maombolezo ya kifo chake hapa Dar es salaam, Nyerere alisema Jamal ndiye aliyekuwa anatoa fedha wakati wa harakati za ukombozi. Alikiri kuwa ndiye aliyemlipia nauli kwenda kuhutubia umoja wa mataifa ili nchi yetu iweze kutoka mikononi mwa wazungu kwa wakati huo.

Nchi yetu ni masikini sana. Tuache kujenga utamaduni wa kibaguzi. Tuwapime viongozi wetu kwa itikadi wanazozisimamia badala ya sura na rangi zao. Mtanzania ni mtanzania tu hata awe anafanana na Kobe, Kindi, au Kuchakulo. Makaburu wa afrika kusini ni raia wa hiyo nchi. Wengi wamezaliwa pale. Kuna weusi waliozaliwa katika kambi za wakimbizi pale morogoro lakini ni raia wa Afrika Kusini. Makaburu walipingwa na dunia nzima sio kwa sababu ya wekundu wao. Ni raia wa Afrika kusini. Dunia ilikuwa inapinga ugonjwa wa sera za kibaguzi.

Watu wasio na sera hasa wale wasiopenda kujidhughulisha, wanatabia ya kupenda kugawa watu. Kikwete amekuwa kiongozi katika sehemu kubwa ya umri wa maisha yake. wakati anagombea uraisi, kambi yake ilitakiwa iwe na mengi sana ya kutueleza kutokana na uchapaji kazi wake "detailed". Badala yake tuliambulia Cheap shot-an unfair or malicious attack on Salim. Watanzania wote tukaacha kujenga utamaduni wa kuwahoji wagombea wetu, badala yake tukanunua utamaduni wa kijinga. Sasa tunalalamika kwamba anakimbia maswali. Tumeshindwa kumuuliza maswali wakati anagombea uraisi tunataka kumuuliza leo ameshakuwa raisi? ebo!

Hivi kweli kuna mtanzania leo hii anadhani (sio anafikiri), kuwa raisi wa nchi yetu ni mtanzania? labda kwa sura na rangi mnazozitaka. Itikadi na Sera anazozitekeleza Kikwete na aliyepita Mkapa hazitokani na matakwa ya watanzania na haziwanufaishi watanzania. Kipindi cha Mkapa tumetawaliwa na makaburu, Kikwete kuna akina Sinclair. Wale ndiyo wanaweza kumkalisha raisi chini na wakamuuliza maswali na asikimbie. Mtanzania ukaulize maswali? thubutu.

Nakubaliana na fikiraduni. Ubaguzi ni ugonjwa na wala sio kitu cha kujivunia. Tuache kuwachagua "Mamluki" eti kwa sababu ni wenzetu, yaani wanafanana na sisi hata kama mawazo na mioyo yao vinatofautiana na vyetu. Hawa ni machangu doa wa IMF, World Bank na wahuni wengine. Hivi leo hii tunadhani kuwa Raisi wa sasa wa Iraq anayefanana na watu wa Iraq ndiye anayeiongoza Iraq? Watu wa Iraq wanaweza kujivunia kuwa yule kibaraka wa Marekani ameondoka na sasa tumempata Rais ambaye ni miraq?

Wanaodhani kwamba Marekani haitakuwa na Raisi mweusi wakafikiri tena. Hizi nchi zimeendelea. Taratibu watu wanaonekana kuacha old fashioned prejudices. Americans have no friends, they have interests. Mtu yeyote anayeweza kusimamia interests zao atawaongoza. Kuna wabaguzi marekani ambao hawataisha. Wapo wazungu wanopenda Mbwa kuliko wanavyompenda mtu mweusi. Mzungu wa sasa hivi amefikia mahala ambapo kama kuna wagombea uraisi wawili, mmoja ni mzungu na mwingine ni mweusi, na akaona kuwa yule mzungu akichaguliwa anaweza kumnyanganya mbwa wake, ila mweusi anataka kutetea urafiki wa mbwa na binadamu. Kuna mawili. Mzungu anaweza asiende kupiga kura kwa sababu ya ubaguzi juu ya mweusi au anaweza kwenda kumchagua mweusi kwa sababu ya mapenzi yake aliyonayo juu ya mbwa kuliko ya mtu mweusi (interest). Hivi ndivyo mweusi atakuwa raisi wa Marekani.

Powel hakuwa kipenzi cha Bush na marafiki zake (conservatives) kwa sababu ya itikadi zake. Mwanzoni Bush alitaka kumtumia kama kibaraka "a die" -nauli ya kuingilia Ikulu. Katika kipindi chake cha uwaziri, ni mara nyingi alikuwa anamwambia Bush "hapana". Rice ni mtu wa ndiyo mpaka mwisho. Ni kipenzi cha maconservatives sio kwa sababu ya rangi yake, bali kwa sababu ya kulinda maslahi yao full stop.

Watanzania tuache kujenga utamaduni wa kibaguzi. Ubaguzi hauna mipaka. Hii siyo historia ya Kyoma, bali ni historia ya maisha ya binadamu. Tukianza kuamua chaguzi zetu kibaguzibaguzi, basi mstakabali wa nchi yetu utaamuliwa kikabila, kidini, na ujinga mwingine unaofanana na huo.

Maswala ya nani kazikwa wapi sidhani kama yanasaidia kutatua matatizo tuliyonayo. Kama kuzikwa ni kipimo cha uzalendo, basi Mobutu Seseseko angezikwa Zaire ambako aliwaongoza wazaire kwa miaka yote ile. Au Kabulu Botha akifa asizikwe Afrika Kusini. Tuache mawazo ya kizamani. Hakuna mahusiano yoyote kati ya kutatua matatizo ya watu na sehemu unapozikwa. Dunia sasa hivi ni kisiwa. Walioiongoza Tanzania miaka kumi iliyopita hawako Tanzania. Hata wakifa hawatazikwa Tanzania.
 
Duh! Kyoma wala sina la kuongeza.

Hawa hawa walishasema kuwa kabila kubwa hakuna kupewa urais, yaani Mchaga, msukuma, mnyakyusa,wanyamwezi na wahaya hakuna kuwa rais TZ. na hili lipo na watu wanalifahamu.

Hiyo tumeinyamazia, ila ndo hayohayo uliyoongelea. Tatizo hawa washkaji hawajaishi Rwanda na Burundi au Somalia, wanaangalia magazeti na TV tu!! Jamani jiwekeni ktk nafasi ya hizo nchi mtaelewa kuwa UBAGUZI ni mmbaya sana.....

Mungu awasaidie muwe na Moyo wa UPENDO wa dhati.

FD
 
Fikiraduni,

Nasisitiza kuwa walioiongoza Tanzania miaka kumi iliyopita wakifa hawatazikwa Tanzania. Sisi tutabakia na misukule tuniita "maraisi wastaafu". These people have no hearts. Leo tunajiongopea kuwa tumemchagua Kikwete tena kwa kura nyingi.

Waliomchagua Kikwete ni wale waliotembeza yale mamilioni ya fedha ili kununua watu. Wale ndiyo wanaoongoza nchi. Wale ndiyo wanaoweza kumuuliza maswali. Wale ndiyo wanaomuandalia mazingira ya kwenda Nasdaq. Wakati wa uchaguzi tulikubali kupewa fedha na sisi tukaenda kununua Kimpumu, Ulanzi, Uraka, Kipasula, Komoni, Mnazi, Gongo, Mbege, Pingu, Lubisi, Kayoga, Wanzuki, Mataputapu, Kangala, Kyindi, Kwete, Mnanasi, Tembo, koroba, na Dengelua. Pale ndipo tulikuwa tunauza nchi. Now we are sober and trying to come up with the so called "questions" to "beloved our president". Si mzawa! rangi yetu! anameremeta, "akanana".

Hivi tunafikiri Balozi Daraja ndiye alimuwekea kapeti jekundu Kikwete kwenda Nasdaq? Kwenye soko la watu tunaowaita wabaguzi? Wanaowachukia weusi wao wa New Orleans, lakini wanatupenda sisi weusi wa Tanzania na Mheshimiwa wetu Raisi Kikwete? Wanataka kuja kutuendeleza sisi kabla ya weusi wa nchini mwao! Cha kufurahisha ni kuwa tunajivunia jinsi Raisi wetu anavyong'ata kimombo kwenye TV za Marekani MSNBC. Tukitaka kumuuliza maswali ya kiswahili pale DC anatukimbia. Mimi nilidhani Raisi ni mzalendo mwenzetu.

Waliompeleka Nasdq ndiyo wanaoiongoza nchi yetu. Wamekwisha pewa hati miliki ya ardhi yetu yenye madini tele. Wale ndiyo wanataka Kikwete awahakikishie maswahiba wao ambao ni mabepari na makupe waje kununua vile ambavyo wenzao waliowahi wamewekeza "kama akina Karl Peter". Hao ndiyo wana haki ya kumuuliza Raisi maswali na akajibu.
Hakuna mtu anakuja kuwekeza nyumbani. Wanakuja kuchuma na kuondoka. Mazingira mazuri anayoyaelezea Kikwete pale Nasdq ni yapi?

Hivi kweli Compaq/HP wanaweza kujenga kiwanda cha Computer kikubwa bongo kama wafanyavyo China, Indonesia na India? Si tuna cheap labor? What about Education? Mazingira mazuri ya uwekezaji ni kuwapa watu wenu elimu ya maana na kuweka infrastructure. Watu waliwengi hawana elimu. Bado ni gharama kusafirisha mizigo kutoka Mwanza to Dar kuliko kutoka Japan to Dar. Hayo ndiyo mazingira mazuri ya wawekezaji kuja kutunufaisha sisi watanzania. Katika nchi za watu wenye akili timamu, hakuna njia yoyote ambayo Kikwete angechukuwa Uraisi bila kufafanua kwa kinagaubaga bila miyeyusho suala la IPTL. Juzi katika hotuba yake kwa wananchi anasema suala la umeme ni kikwazo kikubwa kwa nchi yetu. Are you real saying?

Sisi tumetoka kwenye ulevi wa mataputapu na kuweka masuala yote nyeti pembeni na kuanza kujichimbia makaburi ya ubaguzi mpaka leo baada ya uchaguzi. Watu wanaoona mbali wamemuita Salim huko Dafar. Anatakiwa kukaa chini kufikiri na kusuluhisha matatizo ambayo sisi tunayapalilia. Hagombei tena uraisi, na wala sio waziri. Matatizo yote tuliyokuwa nayo bado tumefunikwa na ukungu mzito wa majadiliano ya ubaguzi. Kama unavyoona majadiliano ya ubaguzi yanaendelea, hata matokeo yake yanatabia ya kumea na kuchukuwa nafasi ya vitu vya msingi. Ubaguzi maana yake hakuna sifa. Ni mwenzetu basi.

Mfano mdogo tunaouona ni wa vyombo vya habari vya IPP - Mengi na Habari Corporation - Ulimwengu. Mwenzetu ni mtusi ati! Ulimwengu alimpigia Kampeni Mkapa sio kwa sababu aliona ni bora kuliko watanzania wote, bali kwa sababu kati ya wagombea waliokuwepo wakati huo, aliona yeye ndiye anafaa kuwa Raisi. Chombo chake Rai na Mtanzania wakati huo, havikukiuka maadili ya uandishi wa habari. Hawakuchanganya maoni yao na habari. Walivitofautisha hivi vitu viwili.

Front pages za Mtanzania na Rai, hata Dimba la michezo kwa wakati huo 1995, yalitoa haki sawa bila kushabikia mgombea yeyote. Yaliandika kile kilichoonekana. Habari yoyote katika magazeti hayo ilijibu maswali matano ya msingi ya uandishi wa habari-what happened? when it happened? where it happened? why it happened? and finaly, who was involved?. Kama zilivyo kanuni za uandishi wa habari, walitenga kurasa za makala tena zikiongozwa na Rai ya Ulimwengu mwenyewe na wakati mwingine hata Tahariri zao zilikuwa zinampigia kampeni Mkapa.

Ulipokuwa ukisoma gazeti, ulikuwa unajua fika kuwa haya ni maoni ya mhariri yaliyokuwa na sehemu yake, haya ni maoni ya mmiliki Ulimwengu-Rai katika ukurasa wake, haya ni maoni ya wasomaji sehemu yake, na hii ni habari ambayo ndani yake hakuna maoni ya mtu. Hata mwandishi wa habari hakuona haya kuweka jina lake. Vyama vyote vilitendewa haki sawa ya kuandika habari za wagombewa wao bila kupenyeza maoni ya kuwaponda ndani ya hiyo habari. Uchaguzi ulipoisha, Vyombo vya habari vya Ulimwengu kama kuna mtu alivifuatilia kwa makini, vikaanza kazi yake ya kuikosoa Serikali.

Havikuwa na simile hata kidogo. Wajinga walianza kunungunika kuwa mbona Ulimwengu anamgeuka Mkapa. Hapana! huo ndiyo uzalendo. Akaanza kupinga rushwa, ufisadi, mauwaji ya Zanzibar na vitisho vya serikali kwa wananchi kutumia vyombo vya dola. Wizi wa mchana, na utetezi wa wanyonge. Huko sio kumgeuka Mkapa. Alikuwa anamsaidia mtu aliyempigia kampeni. Leo hii tunamwita Ulimwengu Mnyarwanda. Toka lini Myarwanda anatetea uhai wa maisha ya Mzanzibar au muislam pale mwembe chai?

Angalia vyombo vya IPP, hakuna ubaya kumpigia kampeni Kikwete. Tofauti yao na Ulimwengu, ni kuweka maadili ya uandishi pembeni. Wanawalisha matapishi wana nchi. Leo wanakwambia Lowassa ni mchapa kazi pale wizara ya maji. Kesho wanasema wizara ya maji ilikuwa sokomoko. Raisi alivyokuwa anahutubia ugenini akaulizwa swali na akili zikaruka kwa haraka utafikiri mwandishi alikuwa kwenye kichwa cha Raisi. Ukisoma habari unajiuliza kama kweli hayo ni maoni au ni habari?

Kwa kifupi ni rahisi kugundua kuwa IPP wanatetea interest zao na Habari walikuwa wanatetea interests za taifa. Hata sasa hivi, Ulimwengu alikuwa anampigia kampeni Salim. Lakini baada ya Kikwete kushinda, hampingi Kikwete. Anampa moyo kikwete kwa kumulika sehemu zilizokwisha oza. Hiyo ndiyo kazi ya uandishi. Huu ndiyo uzalendo. I don't give a damn kama Ulimwengu ni Mtanzania mwenye asili ya kinyarwanda, na Mengi ni Mtanzania Mzawa. Nchi yetu watu hawajasoma kwa wingi kuweza kuchambua habari. wanameza tu na kuchanganyikiwa. Of course, media shouldn't tell us what to think, but what to think about! lakini sisi wapiga mungi tunatambua hayo? Mengi akitekenywa kidogo anakimbilia uzawa, lakini amini, vyombo vyake haviisaidii Serikali ya Kikwete na hata havitusaidii sisi wananchi.

Kaangalie ka Chiluba na mawazo yanayolingana urefu wake. Watu wanasema Tanzania ni maskini. Kameiacha Zambia katika ufukara. a way below povert line. Majuto huja baada ya mjukuu. Wazambia wanajuta na hawawezi kumrudisha Kaunda. Hata hivyo, watamrudisha vipi wakati wamekwisha jazwa ujinga wa majadiliano ya kuwa Kaunda siyo Raia. Sisi ndiyo mambo hayo tunakumbatia sasa
 
Hivi Kyoma huyu Salim alikosa msaada wakati wa Wahutu na Watusi leo anawezaje kuwa msaada wa Darfur ? Je kama nikisema kaitwa kule kwa sababu wanao waua waafrika wenzetu ni waarabu wenzake wewe utasema ndiyo akili hiyo ???
 
Tunachosema ni kwamba regardless ya convincing arguments za wenzetu kuhusu Jamal kuzikwa Canada, bado sio ustaarabu kwa kiongozi wa kufikia mpaka uwaziri kuzikwa nje ya nchi yako, something is not right,

Ndio respect kwamba mzee alilitumikia taifa letu with all he had, lakini kuzikwa nje ya nchi yetu hilo bado haliingii akilini as wabongo!, Tatizo sio Jamal kuzikwa nje, tatizo ni kiongozi wetu mwenye asili ya kihindi kuzikwa nje it all about the symbolism it represent, I mean it does not make a sense at all!

Mbona Sterling alizkiwa bongo na yeye alikuwa muingereza mbongo! Hawa kina Rice na Powell they have nothing to do na hii issue, kwanza hata wao wanabaguliwa huko jamani, tunajua kuwa mzee Powell alipokuwa waziri ni mzungu Armittage ndiye aliyekuwa na uamuzi wa mwisho kule State Dept, na sasa hivi ni kina Chenney na Rumsifield ndio wenye uamuzi wa mwisho hawa wamewekwa tu kuweka political balance, tofauti na akina Jamal ambao walikuwa ni mawaziri wa kweli with all the power,

I mean ninaelewa points za mzee Jasusi on this issue lakini guys somebody anahitaji kuja hapa ku-explain more of what happened?
 
Mugishangwe,

Naona kidogo mwenzangu UAFRIAKA wako mzito sana, una kitu fulani nje ya swala zima pamoja na kwamba wewe ndiye uliyeanzisha mada hii.

Kwanza swala la Jamal nimekuulizeni kwa nini hamkuchukua maiti TZ maanake Jamal kesha kufa hana sauti tena, na wewe kama mwanzilishi wa hii mada hukufahamu kabisa Jamal kazikwa wapi bila maelezo ya Mkira. Na hesabu kubwa ya watanzania hatukufahamu kabisa wala haikuwa hoja. Uliona wapi hiyo?

Hapa inaonyesha wazi sisi wenyewe ndio wabaguzi yaani taifa zima kiongozi wetu kafariki wala hatuna habari!..Na sijui kama unaelewa ujumbe maalum ulikwenda kuzika ama kudai maiti huko Canada. Hili swali peke yake halina jibu.

Pili,
Swala la Salim, nadhani namwelewa vizuri Mzee Es kwa maelezo ya msimamo wake. Isipokuwa katiba yetu ndio inamruhusu Salim na waarabu ama wahindi kupigania urais Tanzania kama nafasi hiyo inavyotolewa USA kwa weusi lakini wapo wazungu wanakataa kabisa mweusi kuwa kiongozi wa Marekani kwa sababu nzito zinazoambatana na asili ya uzawa..Inabidi mtu ufahamu msimamo wa huyo mzungu (kama alivyo Mzee ES) na sio wale wanaodai tu nigger hawezi kutawala - msimamo wako.

Kwa mantiki hii sioni kabisa unaposimama wewe zaidi ya chuki isiyokuwa na mpango kwa Jamal na Salim...utanisamehe lakini, kwani haya yametokana na maelezo yako mwenyewe.

Swala la Darfur, mshikaji liache kama lilivyo kwa sababu hao akina Salim likes ndio wanaokufa leo hii kwa sababu tu wanapingana na utawala wa Kartoum. Na wanajeshi wa jeshi la Sudan asilimia 90% ni weusi kama wewe na mimi na ndio wanaoangusha mabumu kama tulivyokuwa tukiuana South Africa na Rhodesia..Usiyachanganye maswala haya na yale ya kusini mwa Sudan ambako siasa ni dini sio rangi.

Acheni jamani mmemfuata Jamal hali makosa ni yetu sasa hivi Salim wakati tunafahamu katiba inaruhusu na Salim anazo kila haki na quality kuliko viongozi kibao..au sababu kubwa Mkapa na wenzake fedha zao wanapeleka Swiss badala ya UAE.
 
Mugishagwe,

Hakuna Waarabu wanaowaua waafrika wenzetu huko Dafar. Labda tunatofautiana katika suala zima la uelewa wa Uarabu ni nini na Uafrika ni nini. Kinachotokea kule ni waafrika wenzetu wanauana wenyewe kwa wenyewe kwa misingi ya potofu ya kibaguzi. Kumbuka kinachogombewa ni madaraka/mlo, hivyo, ubaguzi unapandikizwa kama chombo cha kuwarahisishia kazi. Hakuna mwarabu aliyewaua waafrika wenzetu Rwanda na Burundi au Ethiopia ambako hakuna makabila mengi kama ilivyo Tanzania. Kinachoua watu huko ni misingi ya kibaguzi waliyoiweka na kuipandikiza. Nakubaliana na wewe kuwa hiyo siyo akili. Ni kufilisika kwa akili.

Kumbuka ubaguzi hauanzi na mauaji. Mauaji ni matokeo ya ubaguzi. Roma haikujengwa kwa siku moja. Dafar wana historia yao, walianza taratibu kama tunavyoanza sisi mpaka wakafikia hapa walipo.

Salim alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa OAU, kulikuwa na utaratibu wa OAU wa kutokuingilia masuala ya ndani ya mipaka ya nchi.

Wakati wa sherehe za kumpongeza Salim kwa kuchaguliwa kwake hapa Mnazi mmoja, aliwaelezea wananchi jukumu kubwa lililo kuwa mbele ya OAU chini ya uongozi wake. Ilikuwa kuhakikisha wanaondoa utawala wa kibeberu na kuhakikisha nchi zote za Afrika zinakuwa huru. Hivi ndivyo tunapima rekodi za ufanyaji kazi wa viongozi wetu na wala siyo soga.

Upande wa Rwanda, usiangalie wakati wa kipindi cha mauaji toka April to July 1994. Ukifuatilia vizuri suala la Rwanda, utagundua kuwa yalikuwepo maongezi ya muda mrefu kati ya kikundi cha Kagame na Serikali. Kinala aliyekuwa nyuma ya juhudi za maongezi alikuwa Salim. Heshima ya jina la Arusha haipo kwenye ramani ya dunia ya sasa kwa sababu ya hali ya hewa yake. Ni kwa sababu ya vichwa vya watu ambao ni watanzania waliokuwa wanafanya juhudi za dhati kusimamisha mapigano kati ya Kagame na Serikali.

Salimu ndiye aliyeishawishi Serikali ya Mwinyi kuwa msuruhishi. Mikutano yote ya wakati huo kama ulikuwa unaifuatilia, Salimu ndiye aliyekuwa mwongeaji mkuu. January 1994, Serikali ya Rwanda na kikundi cha Kagame walikuwa wamefikia makubaliano ya kugawana madaraka. Hata hivyo, Raisi wa Rwanda Habyarimana hakuwa mkweli kwenye majadiliano. Hakuwa tayari kwa dhati ya moyo wake kugawana madaraka na kikundi cha Kagame.

Kwa siri, akaanzisha kikundi cha kuwateketeza watusi kilichoitwa Interahamwe. Wahutu wanaamini kuwa watusi siyo asili ya Rwanda. Walianza kuua mmoja baada mwingine. Kama zilivyo serikali za kiafrika kukumbatiana. Mtu wa kwanza kupiga kelele kuwa serikali ya Tanzania chini ya Mwinyi ilikuwa haiko makini katika kusimamia maamuzi ya maongezi alikuwa ni Salim. Alilalamika kwenye vyombo vya habari kuwa serikali ya Rwanda inacheza rafu na ilikuwa imeanza mpango wa siri wa kuwaua watusi wasiyo na hatia. Aliamua kumfuata kifimbo cheza Butiama.

Nyerere yeye hakuwa na lugha za kuchombeza kama za Salim. Aliitisha mkutano wa waandishi wa habari Butiama na kutamka wazi kuwa Serikali yetu inakumbatia wauaji. Haya yote yameandikwa kwenye magazeti yetu ya hapa nchini toka mwaka 1993 na 1994. Labda Mugishagwe umekaa nje muda mrefu. Kama uko hapa nyumbani, basi usomi magazeti. Kitendo hicho kilimfanya Mtikila promptly without delay, akamwita Nyerere mtusi na siyo mtanzania. Akamsifia mwinyi kwa kumkumbatia Habyarimana.

Hicho ndicho kilikuwa chanzo cha Nyerere kuambiwa ana asili ya kitusi na siyo Mtanzania. Anatetea watu ambao nia yao ilikuwa kutawala eneo zima la Afrika ya Mashariki. Inawezekana Mugishagwe huwezi kununua hiyo propaganda ya Mtikila lakini kuna watu wengi walio na chuki binafsi na Nyerere au wanaowachukia watu kutoka Mara waliinunua.

Machi 1994 Kagame naye akaanza kuhamaki na kuweka karamu chini. Alishika tena mtutu wa bunduki na kuanza mapigano yaliyokuwa yamesimama. Alihojiwa na vyombo vya habari wakati huo na akasema alikuwa anawakomboa watu wake waliokuwa wanaanza kuuawa. Uliitishwa mkutano Arusha katika kipindi hicho cha machafuko ambao ulihudhuliwa na Habyarimana pamoja na Cyprien Ntaryamira Raisi wa Burundi. Salimu mwenyewe alikuwepo katika huo mkutano.

Tarehe 6 April 1994 wakati wanarudi nyumbani, ndege yao ikatunguliwa. Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa watu kufa kama mainzi. OAU haikuwa na jeshi la dharura. Walikuwa wamewekeza mawazo yao kwenye majadiliano. Walihaa kutafuta misaada ya wanajeshi kutoka umoja wa mataifa. Wamarekani walikuwa wa kwanza kupinga. (no interest in Rwanda).

Mauaji yalivyopamba moto, wabeljiji waliondoa maaskari wao baada ya vifo vya askari wao sita. Askari waliobaki walikuwa ni kutoka katika baadhi ya nchi chache za Afrika zikiongozwa na Algeria ambao kwa tafsiri zetu potofu ni waarabu. Sisi Tanzania ambako ni majirani na waafrika wenzetu, hatukuwa na askari hata mmoja Rwanda. Mimi narudia kuwa ubaguzi ni ugonjwa. Mugishagwe, naomba Physical address yako nikutumie Documentary ya The ghost of Rwanda-DVD. Siyo movie. Utawaona akina Kagame, Habyarimana, na walioua na walionusurika. Wote wanaohojiwa na hata historia fupi ya Rwanda. Achana na Hotel Rwanda movie.

Waliookoa maisha ya waafrika wenzetu kule Rwanda, siyo sisi waafrika wenzao. Tulikuwa tumelala usingizi. Watu wa kukumbukwa ni wale waliokuwa mstari wa mbele kukatisha kwenye mapanga na majabia ili kubeba na kutibu majeruhi. Kuficha watu wasiuwawe. Utakuja kushangaa ukiona watu hao kuwa ni wale tunao waita wazungu wabaguzi, askari tunao waita waarabu wa Algeria ambao kwa kanuni yetu humu ukumbini siyo wazalendo. Leo hii tunadhubutu bila haya kusema kuwa waafrika wenzetu wanauawa.

Wanaosema kuwa Salim alikataliwa na CCM kwa sababu ya uarabu wake wanatupotosha au hawajuhi. Hivi watanzania tuna uwezo wa kumchagua mtu tunaye mtaka kuwa Raisi. Toka lini? eti salim tulimkataa kwa sababu ya uarabu wake! lo! Hivi CCM wangempitisha sisi tungemkataa? Waliomkataa Salim ni kikundi cha watu ambao wamekuwa wakiitawala nchi toka tupate uhuru. Tusijibalaguze kuwa tunaweza kutoa maamuzi. Watanzania wa kawaida hawajawa na uwezo huo.

Salim alikataliwa kwa sababu ya sifa zake za uongozi na siyo kwa sababu ya uarabu wake. Sisi raia wa kawaida tunapewa mada tu ya kuzungusha akili yetu. Ebu jiulize kidogo! Viongozi wetu ni walewale toka tupate uhuru. Kundi hilo la Viongozi waliowengi ndani ya CCM, labda asilimia 85 wakiongozwa na Mkapa ndiyo waliuza mashirika yetu bure, hapa unaongelea mikasa ya IPTL, Ndege ya Raisi, Rada, NBC, Nyumba za Serikali, TTCL, Netgroup, Loliondo na Chavda, kununua nyumba ya ubalozi Italy kwa njia za udanganyifu, Kupitisha sheria za kuhararisha uchaguzi kwa njia ya rushwa-yaani kununua kura kama unanunua embe dodo, na ufisadi mwingi ambao tunaweza kuorodhesha mpaka kesho. Jemedari mkuu anayewasimamia walaji wote hawa ni Benjamin Mkapa.

Swali langu ni kwamba hao viongozi, wamekaa kikao na kuangalia mustakabali wa nchi yetu. Wakasema hii mikataba hewa, rushwa, na ufisadi inabidi vikomeshwe-kama alivyosema Kikwete kwenye hotuba yake ya kiini macho bungeni, na hata kama alivyo kiri Kingunge najuzi tu. Wakaendelea kusema kuwa tunamtaka kiongozi shupavu/madhubuti wa kusimama kidete na kuvunja mikataba yote hii alafu kuhkikisha waliokiuka taratibu wanafikishwa katika vyombo vya sheria kama zifanyavyo nchi nyingine.

majina mawili yako mezani, yaani Kikwete na Salim. Well, hata Mwandosa pia. Wakasema nani anafaa. Wakaanza panga kwa Salim kuwa huyu bwana ni mwarabu. Tukimpa nchi hana uzalendo. Ataiuza kwa waarabu wenzake. Kikwete anafaa. Huyu kijana anaweza kupangua mikataba yote na kuwafikisha mahakamani waliohusika. Waliohusika ni hakina nani? Mkapa, anna Mkapa, na viongozi asilimia 65 ya wanaopiga kura za kumpitisha mgobea urahisi. Huyo mwingine naye kibaka tu. Hivi ndivyo walivyomkataa Salim and you want me to buy that.

Hata siku moja mwizi hachukiwi na mwizi mwenzake. Mtu ambaye siyo mwizi anachukiwa na wezi. Walijua kuwa Salimu akiingia majamboz yao yote waliyoyafanya yanakwenda mrama. Waswahili wa pwani hujuana kwa vilemba. Hakuna njia yoyote unayoweza kumshawishi mtu wa kawaida kuwa kikundi cha wezi kinamchagua askari wa kutokomeza wizi. guys! you must be kidding! Mambo ya regan kuwa na Faili la Salim ni soga tu.

Nimeeleza mwanzoni kuwa Americans have no friends, They have interests. Salim wasn't serving their interests. Eti nani? Koffi Annan? jamani si kibaraka tu au Mugishagwe unaonaje? Marekani na utajiri wake wameshindwa kuishawishi dunia kukubaliana na kitendo cha uvamizi wao kwa Iraq. Tanzania na umaskini wetu, tuliishawishi OAU, UN na dunia kwa ujumla kukubaliana na kitendo cha kuivamia Uganda na kusimika mamluki pale akina Obote, Binaisa na Yusufu Lule. Tulikuwa na Raisi mzuri lakini alikuwa na timu nzuri sana.

Salimu anajulikana kwa kutokuwa na ukabila, udini, na mzaha katika uongozi. Amekaa pale Ethiopia kuiongoza OAU na siyo kuleta ushikaji wa kuwajaza wapemba, na wabongo. Nafasi zilishikwa na wataalamu kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika. Hakuwa na upendeleo na nchi yoyote ikiwemo Tanzania. Pale hakwenda kuongoza Tanzania. Nitajie mtu hata mmoja ambaye alikuwa ni mbabaishaji katika teuzi zake za OAU. Nakumbuka kuna tume ya kuchunguza haki za binadamu chini ya OAU iliyomtoa kijasho kamuzu Banda, ilikuwa na majaji sita waliobobea kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Kutoka Tanzania alikuwa ni Jaji kisanga. Fatilia ni mtu wa aina gani.

Kuna mbongo ambaye alikuwa mfanya kazi wa Salim, alileta mtafaluku pale Ethiopia na akatiwa ndani. Wabongo walilaani, lakini huyu jamaa hana undugu, ukabila, wala mzaa. CCM wanajua hivyo. Ndiyo maana Ben alihakikisha anagonga msumali wa mwisho kwenye kaburi isije ikatokea hata bahati mbaya akashinda. Alibadirisha hata utaratibu uliyompa yeye Uraisi. Tofauti na Kikwete anayewekewa vyombo vya habari na wanaokula bila kunawa nchini mwetu, Salim akija Marekani vyombo vya habari vinamkimbilia kusikia anatema chehce gani? hata juzi alikuwa anahojiwa na C-span ya huko Marekani.

Sisi tunabaki kuongopeana kuwa tumemkataa kwa sababu ni mwarabu. Mbona hatumkatazi raisi wetu kutia aibu huko uarabuni kwa kuomba fedha na kupewa elfu kumi. Hata bila haya tunatangaza. Tunaomba fedha ya njaa kwa sababu ya ukame wakati tuna the second largest lake in the World - Victoria, The deepest lake in the World-Tanganyika,

Salim hawezi kuleta maajabu ya kutatua au kuzuia mauaji yanayoletwa na misingi ya chuki. Anachoweza kufanya ni kujaribu kutumia akili kukinga. "Prevention is better than cure". Huwezi kusema unambagua mwarabu alafu wakati huo ukakasirikia mtu anaye mbagua mkatoliki, mhaya, mkurya, au mweusi. Ubaguzi ni ubaguzi tu.
 
Mzee ES,

Nilivyosoma michango ya baadhi ya wachangiaji, nimepata tafsiri kuwa kitendo cha Jamal kuzikwa nje kinaambatana na ukosefu wa Uzalendo, Utaifa na hata inawezekana wakati anafanya kazi, alikuwa anajiimalisha nje aliko zikwa. Mimi ninachosema ni kuwa hakuna mahusiano yoyote kati ya sehemu anapozikwa mtu na uzalendo au utumishi wake kwa nchi husika. Ndiyo maana nikatoa mfano kuwa kama suala la Jamal aliyekuwa waziri kuzikwa Canada linaleta shauku, mbona la Mobutu aliyekuwa Raisi wa nchi kutokuzikwa Zaire alileti mtikisiko?

Katiba ya nchi yetu ina utaratibu wa kuwazika maraisi wastaafu na walioko madarakani endapo watafariki. Hatuna utaratibu wa kuzika mawaziri na viongozi wengine wa juu. Siasa nchini kwetu ni sehemu ya ajira. Ukijiondoa katika ajira mapema, hakuna hata kama ulikuwa waziri, hakuna mpango maalumu wa huduma za afya, na mambo mengine ya msingi. Ndiyo maana watu wanangangania uongozi toka tupate uhuru mpaka leo hii. Hata akina Fundikira, bado wanapigana vipepsi vya ruzuku mpaka leo.

Jamal kama alikuwa na mtoto Canada wa kumtunza na kumpatia huduma muhimu zitokanazo na uzee wake ambazo serikali yetu isingeweza kumpa, angamuacha akafia Bongo? Alipofariki dunia na Serikali yetu haina utaratibu wowote wa kumzika waziri yeyote wa zamani, ulitaka mtoto wake afanye je? Au wewe unapendekeza ingekuwa je?

Kuhusu Powel na Rice mimi nilidhani mchangiaji mmoja aligusia suala la Mmarekani mweusi kutokua Raisi wa Marekani. Nakushauri ufatilie vizuri suala la Armittage. Hakuwa na maamuzi ya mwisho kwa Powel. aliongezwa ili kupunguza makali ya itikadi za Powel. Kumbuka wakati wa Kampeni za 2000, Bush alikuwa anamuhitaji Powel kuliko Powel alivyokuwa anamuhitaji Bush. Powel ana sifa ya kujitegemea kimawazo na alikuwa anaheshimika sana kutokana na vita ya ghuba.

Kambi ya Bush ilitoa leak kuwa Powel angekuwa waziri wa mambo ya kigeni hata kabla ya uchaguzi. Baada ya Bush kushinda, Powel alikuwa ahitajiki. Nani hajuhi kuwa hata Bush mwenyewe siyo anayeendesha nchi, itakuwa Powel? Maamuzi mengi yanafanywa na Cheney pamoja na marafiki zake. Kwa mtu kama Powel, siasa siyo ajira. Kwanza kile cheo kilimzalilisha kuliko kilivyomjenga. Misimamo yake ndani ya majadiliano ya ndani na kuwapinga Chenney pamoja na Ramsifield kulileta tension ndani ya uongozi wa Bush. Lakini walimuhitaji Powel kwa sababu yeye pekee katika uongozi wote, ndiye alikuwa na credibility ya ku-spin, au kuwaelezea wamarekani na dunia nzima nini kinaendelea. Ushahidi alioutoa kuhusu Iraq limekuwa ni doa kubwa katika maisha yake.

Hivyo, Armittage couldn't even tie the shoes of that gentleman. Aliwekwa kupunguza makali. Ni kweli kama unavyosema, uongozi wote wa Bush, wenye maamuzi ya mwisho ni Cheney, Ramsfield, yule Raisi wa sasa wa Bank ya dunia, na marafiki zao wachache. wengine wote waliobaki akiwemo Bush ni ma-spin doctors na watekelezaji. Kinyume na Powel, Rice haitaji mtu kama Armittage, ndiyo maana hayupo.

Hawa watu wawili, ni mifano ya kutufungua macho na kupanua wigo wa majadiliano. Kumbuka watu weusi Marekani wametoka katika historia ya watu weusi watatu ni sawa na binadamu wa kizungu mmoja. Baadae mweusi mmoja akawa sawa na mzungu mmoja. Alafu wakaruhusiwa kupiga kura. Baadae nao wakaanza kugombea uongozi. Mzungu aliyeishi miaka ya arobaini, ukimwambia kuna mtoto anaitwa Obama, ambaye baba yake ni Mkenya na yuko bungeni tena Senetor, atakukodolea macho.

Leo hii tunatumia vigezo kuwa hata Mmarekani mweusi hawezi kuwa Raisi wa Marekani ili tuweze kuwabagua wengine. Historia itakuja kutuhukumu. Sisi tukisha aanza kubaguana na miongo michache ijayo, marekani ikampata Raisi mweusi, sijuhi tutakuwa tumewaacha kwenye mataa wajukuu zetu. Suala la Rice na Powel linaigia hapa kutokana na Utaifa, asili ya mtu na rangi yake, pia uzalendo. Itikadi na sera za mtu binafsi.
 
mzee Kyoma! kweli wewe ni kyoma kweli kweli!

Umenifurahisha na kunisaidia sehemu nyingine! Ninadhani hata Mugwishage ataamua kukubali yaishe. Ila mhindi no! nilichosema kuhusu Rais Mwafrika marekani sikumaanisha kwamba weusi hawana uwezo. Ila tu hiyo nafasi watapewa lini? 20, 50 100 years to come?

Hapa umemwaga vitu! tujadili mambo haya ni muhimu sana. Hatuwezi kuwa tunchaguliwa viongozi na kikundi kidogo cha watu. Madhara yake ni kama ya Mwalimu kumpitisha Mkapa huko CCM halafu ikambidi kuzunguka nchi nzima na uzee wake kumukampenia Mkapa! alikuwa hajulikani kabisa!!! Vinginevyo Mrema angechukua nchi mwaka 1995! Mrema alisikika na kujulikana! lakini Mkapa mhhhh!

"Salim alikataliwa kwa sababu ya sifa zake za uongozi na siyo kwa sababu ya uarabu wake. Sisi raia wa kawaida tunapewa mada tu ya kuzungusha akili yetu. Ebu jiulize kidogo! Viongozi wetu ni walewale toka tupate uhuru. Kundi hilo la Viongozi waliowengi ndani ya CCM, labda asilimia 85 wakiongozwa na Mkapa ndiyo waliuza mashirika yetu bure, hapa unaongelea mikasa ya IPTL, Ndege ya Raisi, Rada, NBC, Nyumba za Serikali, TTCL, Netgroup, Loliondo na Chavda, kununua nyumba ya ubalozi Italy kwa njia za udanganyifu, Kupitisha sheria za kuhararisha uchaguzi kwa njia ya rushwa-yaani kununua kura kama unanunua embe dodo, na ufisadi mwingi ambao tunaweza kuorodhesha mpaka kesho. Jemedari mkuu anayewasimamia walaji wote hawa ni Benjamin Mkapa.

Swali langu ni kwamba hao viongozi, wamekaa kikao na kuangalia mustakabali wa nchi yetu. Wakasema hii mikataba hewa, rushwa, na ufisadi inabidi vikomeshwe-kama alivyosema Kikwete kwenye hotuba yake ya kiini macho bungeni, na hata kama alivyo kiri Kingunge najuzi tu. Wakaendelea kusema kuwa tunamtaka kiongozi shupavu/madhubuti wa kusimama kidete na kuvunja mikataba yote hii alafu kuhkikisha waliokiuka taratibu wanafikishwa katika vyombo vya sheria kama zifanyavyo nchi nyingine.

majina mawili yako mezani, yaani Kikwete na Salim. Well, hata Mwandosa pia. Wakasema nani anafaa. Wakaanza panga kwa Salim kuwa huyu bwana ni mwarabu. Tukimpa nchi hana uzalendo. Ataiuza kwa waarabu wenzake. Kikwete anafaa. Huyu kijana anaweza kupangua mikataba yote na kuwafikisha mahakamani waliohusika. Waliohusika ni hakina nani? Mkapa, anna Mkapa, na viongozi asilimia 65 ya wanaopiga kura za kumpitisha mgobea urahisi. Huyo mwingine naye kibaka tu. Hivi ndivyo walivyomkataa Salim and you want me to buy that. "
 
Mzee Mkira,

Nakuelewa sana kuhusu wamarekani weusi. Lakini lazima uelewe kuwa wamarekani weusi hawatapewa uraisi. Muda muafaka utafika na kutakuwa hakuna pingamizi. Wananchi wa Marekani hawajawa tayari kuwa na Raisi mweusi na hawatakuwa tayari hata siku moja. Lazima wawepo watu weusi waliotayari kuwa maraisi wa Marekani. Wakiwepo, wananchi hawatakuwa na chaguo isipokuwa kusalimu amri kama nilivyoelezea nyuma. Kumbuka weusi hawakupewa uhuru wa kupiga kura huko Marekani. Wananchi wa Marekani hawakuwa tayari kuacha vitendo vya kibaguzi.

Walikuwepo weusi ambao walikuwa tayari kuwaongoza wananchi wa Marekani ili wafute sheria za kibaguzi. Watu hao miongoni mwao ni kama mwandishi James Baldwin ambaye maandishi yake mpaka sasa yanasomwa kama "American Literature" katika shule za wazungu na weusi. Wengine ni muhubiri Martin Luther King Jr. ambaye alipata wafuasi wa rangi zote. Taratibu sheria zikafutwa na jamii ikaanza kubadilika.

Wabaguzi wapo na watakuwepo mpaka mwisho wa dunia. Kitu kitakacho warahisishia weusi kupata nafasi hiyo mapema, ni ile dhana ya kuwa wamarekani hawana marafiki. Hata uwe mzungu, kama hutetei maslahi yao wanakutupa tu. Angalia historia ya Marekani na Ufaransa toka vita kuu ya pili ya dunia. Lakini Chirac alipoanza kumpa madonge Bush wakati wa uvamizi wa Iraq, hata Chips dume za kimarekani "French fries" zilianza kupewa jina jipya.

Bintie Rice, ni mtu wa nne kuukwaa uraisi kama likitokea jambo, ambalo sidhani. Hata hivyo, miaka ya 1920s hii ilikuwa ni miujiza kuota kitu kama hicho. Siku itafika, na wamarekani wakiona mweusi anayeweza kulinda maslahi yao, na yeye akawa yuko tayari, atawaongoza tu. Futa hawa matapeli akina Jesse Jackson, Sharpton na wengineo. Hawa wanaomba ubaguzi uendelee ili waweze kuendelea kuweka mkono kinywani.

Masuala uliyoyawekea wino mwekundu inatubidi tujiulize sisi wananchi na siyo matabaka ya watawala. Sisi wananchi tunatakiwa tuwe na mdahalo wa wenyewe kwa wenyewe. Mitaani kwenye michezo ya bao, uwanjani tunapokwenda kuangalia mpira kama alivyokuwa anafanya Steven Biko wa Afrika ya kusini. Tujadili matatizo yetu ya msingi kwanza alafu tufikie muafaka wa pamoja, alafu tuangalie nani atayatatua. Sisi tunafanya kinyume. Tunaangalia nani atatatua matatizo yetu ambayo hatuyajuhi, alafu tukisha mpata na kumpigia kura, ndipo tunayajadiri matatizo yenyewe.

Umeongelea suala la Mkapa. Hakuna mtu ambaye hakujua kuwa wakati Mkapa yuko wizara ya sayansi na Teknolojia ambako ndiko alitoka kugombea uraisi. Wizara yake ilikuwa ni miongoni mwa wizara zilizokuwa zimepamba moto kwa rushwa. Mpaka mwaka 1995, Tanzania ilikuwa na wanafunzi wachache kulinganisha na nchi nyingine za Afrika waliokuwa wanasoma katika vyuo vikuu nchi za nje.

Si ajabu kukuta kuwa nchi yetu ilikuwa inaongoza katika Afrika kwa kuwa na wanafunzi wanaosoma nchi za nje lakini wanalipiwa na Serikali. Hapa siongelei Scholarship zilizotolewa na Japan, china Russia, India au USAID. Nasema Serikali kutoa fedha zake (sijuhi katika mikopo au kwingineko), na kuwalipia wanafunzi kupitia balozi zetu nchi za nje. Serikali ilikuwa inashindwa kuwadhamini wanafunzi wa kutosha hapa IFM, ambao walikuwa wanasomea Computer Science chini ya dola elfu moja kwa mwaka, lakini iliweza kumpeleka mtu London akasomee Cooking kwa dola elfu kumi na sita kwa mwaka.

Walikuwepo wanafunzi wengi ambao hawakuwa na vigezo vya kwenda kusoma nje, lakini Serikali iliwalipia. Watu walisema sema kuwa huyu jamaa anaongoza wizara ya namna hii? Lakini mabingwa wa mizengwe wakasema huyu ni Mr. Clean. Ohoo, inawezekana watu wa chini yake wanaiba lakini yeye ni clean, siyo corrupt. Akaja na Slogan kuwa atapambana na Rushwa bila suluhu. Tulinunua hayo maneno na akaingia Ikulu. What happened? tena yeye afadhali alianza na ka mkwala kidogo.

Kila waziri aliyekuwa akikumbwa na kashfa, anawajibishwa ingawa bila kufikishwa mahakamani. Prof. Mbwilizi, Kilontsi Mporogomyi, na wengine. Pia akaja na vioja vya tume ya Warioba basi. Look now! Mpaka leo tunaambiwa kuwa yeye siyo corrupt isipokuwa watu wa chini yake ndiyo wezi. Tumerudi square one. tuliambiwa wakati anaingia madarakani ambapo wizara yake ilikuwa inanuka rushwa, na tumeambiwa wakati amemaliza muda wa uraisi kuwa ni clean wakati hakuna kilichobaki.

Hata Kikwete, tumeambiwa ngonjera nyingi na hatuulizi maswali. Ehe! ni mchapa kazi, anatabasamu vizuri (Raisi wa nchi huyo siyo Mr. Tanzania), anapendwa sana, hana mali labda marafiki zake ndiyo wana mali (hoops), ni mtu wa watu, (jamani, hatutafuti padri au Sheikh wa kwenda kuzika watu. Tunatafuta Raisi wa nchi), ohoo! Polls-kura za maoni zinaonyesha anapendwa na atashinda uraisi. Wanasiasa ni wajanja sana. Wanakwepa mijadala ya maana na sisi tunanunua hayo yote.

Sasa leo tunategemea kupata kitu tofauti na kile tulichopewa. Eti tumpe muda si unaona kaanza kwa kasi kusitisha uuzaji wa nyumba za Serikali ambazo hata na yeye amenunua. Ebu mtu anayejua nyumba ya Serikali ambayo ipo maeneo mazuri na haijauzwa anyoshe mkono! Kilichokuwa kinafanyika ni uporaji. Nyumba maeneo ya St Peters au karibu na Bahari inauzwa bila kungalia thamani ya kiwanja. Ehe! Serikali yake imefanya vizuri kutokupinga maamuzi ya mahakama ya kutengua sheria za kununua uongozi - Takrima. Ebo! yeye amekwisha kuwa Raisi kwa kuwanunua watu. Amekwisha jua kuwa watu wananunulika hata kama huna fedha. Unachotakiwa kuwa nacho ni marafiki tu. Ukiendelea kuruhusu ununuzi wa uongozi na akaja mtu baada ya miaka mitano mwenye marafiki kukuzidi wewe na wenye pesa kweli kweli utafanya je?

Yeye sasa hivi ni raisi na ana fedha na nguvu za dola na marafiki wenye vyombo vya habari. hakuna mtu kutumia fedha tena. Nawashangaa watu wanasema tumpe muda. Majambazi wa CCM hawawezi kumuweka mtu wanayejua fika kuwa atawakamata. Mchezo utakuwa ni wa soga kama alivyo anza ndivyo atakavyomaliza. Hatuwezi kupanda mbegu za Maharage na sasa hivi tunaona zinaanza kutoka ndani ya ardhi na ile mbegu inagawanyika ili kuruhusu mizizi kwenda chini na tawi kuja juu, alafu sisi tunaikodolea macho na kusema inaelekea huu utabadilika kuwa mwembe. I'm sorry!
 
Mzee Kyoma asnte kwa Lecturer yako. Nusura machozi yanitoke!

Leo kuna article huko ippmedia. Kumbukumbu yangu inakumbusha kuwa wakati ule wa kampeni JKM alisema hatafanya recycling alipohojiwa na BBC kiswahili. Lakini cha ajabu amemtetua tena Msekwa kuwa mwenyekiti wa bodi ya Mazingira!

Hii inanikumbusha siku moja niliongea na mchungaji mmoja kanisani huko ulaya! Nikawa ninajigamba kuwa sasa tumempata mtu ambaye ameahidi kufanya mambo ya kweli! Lakini yule mchungaji alinionya kuwa viongozi wengi hugeuka kuwa vipofu na viziwi mara tu wanapochaguliwa kushika hatamu! Moyoni nikasema
wapi! lakini ngoja tusubiri.

http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2006/06/03/67680.html

Tanzania kwa sasa ina watu milioni 37. Na ninaweza kusema kuna possible candidates wa nafasi kama hiyo labda wapo zaidi milioni 5. siyo kwamba sitaki Msekwa apewe lakini kama ni maisha Msekwa kesha ukata jamani! Ni kwa nini wengine nao wasipewe hizo nafasi.

Mfano, kila mara utasikia mtu mmoja ni mkurugenzi Mhimbili, ni huyo huyo ni speaker wa bunge la africa, ni mgurgenzi sehemu nyingine. Je tukiuliza mambo kama haya nao ni ubaguzi? mtu mmoja anakuwa na nafasi karibu 5. na zote hizo ni ulaji tu! Labda kama analipwa posho na nafasi moja tu! hapo sawa tu. Lakini kama kila nafasi ina malipo yake, ni kwanini badala ya kumpa mtu mmoja wasipewe watu watano ambao nao vipato vyao vitaongezeka lakini mapato yote hayo anarundikiwa mtu mmoja?

Kukusu kulipia mfano msomi mmoja nje ya nchi hata kama kozi zilikuwa si muhimu na wakati huku wakikataa kusomesha watanzania 10 nchini, Inauma lakini ndilo hilo kundi la hao wanaotuchagulia viongozi. Kwa hiyo wanachofanya ni kutaka kuendeleza kikundi chao ili baadaye waje washike nafasi zao. Na ukiuuliza watakwambia lakini si wamesoma! Mfano mtoto wa Sumaye alisomeshwa nje ya nchi na sasa yuko BOT.

Wakati Mkapa akiwa wizara ya science tulikuwa tunaambiwa kuwa schlorship ya nje ilikuwa ni kuanzia laki 3 hapo wizarani. sijui mtaji wao ulikuwa ni kiasi gani na walikuwa wanazinunua wapi? Secretaries ndiyo waliokuwa watoaji wakuu lakini bosi ni mhusika mkuu hawezi kukwepa hili!

Ndiyo maana ninakubaliana na swali la mzee ES kuwa ni kwa nini Jaji warioba hakwenda kwenye hiyo wizara ya science na tume yake ya Rushwa??

Hii imenipunguzia sana imani yangu kwake?

Ninamalizia kwa kusema asante na kama alivyosema JK nchi hii ina vichwa na wanaochangia mawazo yao humu ndani bila unafiki ni sehemu ya hivyo vichwa. Ila tu kama ilivyodokezwa somewhere ninasikia kuna baadhi ya viongozi wa sasa wanabeza hizi nguvu za forum!

Tena waombe mungu au wafanye tu kwa makusudi ili internet isiwafike wanachi huko mikoani, wilayani na vijijini au tu katika majumba ya watu walioko mijini. Na hapo ndipo watakapojua nguvu ya internet.
 
Mzee Kyoma,

(1). No question kuwa you got the juice, tatizo tu ni kwamba bado hujaweza kuya-transform mavitu yako yakawa sambamba na siasa za bongo, siku utakapozielewa siasa za bongo, then utakuwa right on top, kwani sio siri kuwa una mavitu ya kiutuuzima,

(2). Kuhusu Salim unaonekana kuwa very naive, lakini within CCM inaeleweka kuwa alinyimwa kwa sababu ya uarabu wake na mimi binafsi I am being honesty kuwa hata mimi binafsi nisingeweza kumpigia kura yangu, halafu kama alionewa wananchi wangepiga kelele na hasa upinzani, Now publicly hivi ni kweli ulitegemea viongozi wetu waseme kuwa tumenyima kutokana na uarabu wake? Au kuna taifa lolote duniani unal;olijua ambalo leo linaweza kusema hadharani kuwa hawamtaki kiongozi fulani kwa sababu ya rangi yake?

Mimi ninasema kuwa my understanding ambayo ni pamoja na kuifuatilia kwa makini hali ile ya siasa ya uchaguzi ndani ya CCM, ninaamini kuwa Salim alinyimwa kwa sababu ya uarabu wake, kwa sababu Salim amekuwa kiongozi kwa muda mrefu na wajumbe waliokuwa wanapiga kura wanamjua yeye kuliko JK, na Mwandosya! sasa ilikuwaje wakamnyima kura? Siku Ben antangaza kugombea urais 1995, pale mezani alikuwa na Salim na Warioba, sasa kama kweli walikuwa marafiki kiasi hiki ilikuwaje Ben akamgeuka mwenziwe dakika ya mwisho? Ben alitumia hela za serikali kibao kumsaidia Salim kuwa katibu wa OAU mbona uaris akamkatalia? Na baada ya uchaguzi mbona wananchi hawakulalamika kuwa Salim ameonewa? Yule bwana aliyemfunga Adis hadithi yake ni nzito kuliko ulivyoisema na tusingependa kuisema!

(3). Powell alikuwa antumiwa na kambi ya Bush kwa ajili ya matatizo ya kura kule Florida, serikali ya Bush ilipopewa urais na mahakama ilibidi ifanye kazi za ziada kujaribu kununua legitimate ndio maana kina Powell wakawekwa, ndio maana Bush baba akaanza kuwa rafiki wa Clinton, ndio maana yuel mhindi mwekundu wa Democrat akapewa uwaziri wa mawasiliano katika serikali ya Bush nia na madhumuni ilikuwa kuwatumia ktafuta heshima na ndio maana kwenye term ya pili ya Bush kushinda kwa halali mzee Powell akatemwa, na ni juzi amesema jinsi US ilivyokuwa wrong kuhusu Iraq meaning kwamba akiwa waziri hakuwa na uamuzi wa mwisho wala hakuna aliyekuwa anamsikiliza,

Rice ni expert wa Russia tu, na ni the only area ambayo Bush anamtumia lakini kama ni maamuzi ya Foreign Policy yanafanywa na Chenney na Rumsifield, Mweusi huko US ni mweusi tu na ndio maana Powell alipotaka kugombea urais 2000 alionywa na Republicans kuwa atajitafutia mauti buree, na besides hawa kina Powell na Rice hata weusi kule US hawaaamini kwani wanaitwa ni SELL OUT hawa maana mweusi wa huko anyeijua vizuri establishment ya huko haamini kuwa kuna mweusi anayeweza kupewa hizo nafasi unless awe a sell out!

The rest of your story ni convincing na ina juice, lakini tatizo ni very naive binadamu wote duniani ni wababguzi wa rangi in one way or another, huko US na maendeleo yote hivi ni kweli unaweza kutembea na msichna wa kizungu Harlem bila msuko suko toka kwa weusi wenzio? Hapa bongo vipi mbona hatuwezi kuwaoa wahindi? Ila tu siku zote utaona wahindi wana mwanamke mbongo kwa kujificha na wakizaa nao watoto wanawaficha huko pembeni? Vipi leo ukioa mzungu akuaneda naye kijijini?

Kama ni uwezo wa kuongoza Salim hakuwa hata na sababu ya kusema kwani unajulikana bro! Kule Adis aliajiri kina Bandora na waarabu wa
Oman hiyo tunajua sio siri, leo nenda UN kumejaa wa-Ghana na wa-West Africa ndio faida ya kuwa na kiongozi wa kutoka maeneo yenu na hilo linakubalika na dunia nzima, wazee waliomzunguka Bush kina Karl Rove ni wa-Texas wenziwe, Mwalimu alizungukwa na akina Butiku na The Apiyos, hawa ni wenziwe wa huko majuu, sasa na mzee Salim alizungukwa na wageni wenziwe kina Bandora na waarabu wa Oman ndio maana na sisi bongo we did the very natural nayo ni ku-stick na kina JK weusi wenzetu, ninasema kuwa Salimangekuwa na uwezo mkubwa wa kisisasa angelielewa hili na kulifanyia kazi mapema!

Wakati wa sisi wabongo kutawliwa na watu wenye rangi tofauti na yetu bado haujafika, sisi mpaka leo bado tunasikiliza tepu za Mwalimu kwa hiyo bado tuna uzalendo regardless na political progress zenu kina Kyoma, sisi wabongo bado na mimi nikiwa mmojawapo Tanzania ni ya watanzania, na mimi ni mTanzania, JK, Ben ndio sio malaika so is Salim, lakini given a choice Watanzania tulichagua tunaye fanana naye! Tena tunaweza kufanya tena hata leo uchaguzi ukirudiwa, na ndio maana juhudi zote za JM kujaribu kuwashawishi wapiga kura wake wampe Salim dakika ya mwisho ziligonga mwamba kwani walimwambia wazi wazi kuwa hawawezi kumpa kura zao mwarabu! Tusubiri labda kizazi kingine lakini not under our watch, hii sio siasa hii reality na ni very natural!
 
Kuhusu Msekwa ni kwamba sasa hivi kuna kampeni za uongozi wa CCM, Diallo ni Mtandao na ana interest zake katika huu uchaguzi na alimsaidia sana JK na michuzi ya kampeni, kwa hiyo JK amempa huyu mzee kwa matakwa ya Diallo,

lakini haibadili uchungu wako mzee Mkira kuwa hawa kina JK ni wale wale!
 
Hata mimi ninasakia kuwa kama si huyo aliyefungwa huko Ethiopia na Salimu au Mwingine ambaye alikuwa Bodyguard wake kuna mmoja wao ninasikia aliuawawa hivi hivi! Na mama yake bado analalamika hadi leo bila Majibu!

Watu wana dhambi ila tu huwa zimejificha! SASA kwanza wadogo zake wengi nisakia hawaicha Bongo! Anyway, kwa upande wangu nina imani SAlim na timu yake wasingefanya lolote! Lakini watu wamekuwa wagumu! Basi ni yale yale ya 2+2=22. Mwanzilishi wa hii hesabu ni Mkandara na siyo mimi ila inafuahisha sana!

ukiangalia tunasikia hata mwaka jana waliokuwa tishio lake ni wazanzibar na siyo wabara! Landa tuache kumjadili SAS maana ni siyo rahisi kupata mshindi!ilalabda tudadili hayo ya wino Mwekundu na tutaanzie topic yake Mzee Kyoma anzisha hiyo topic.
 
Mzee Mkira,

Don't get me wrong. Hakuna ubaya kwa Serikali kuwasomesha watu wake nje. Hata hivyo, Serikali zinazoongozwa na watu waliostarabika kwa manufaa ya nchi, wanakuwa na utaratibu unaoeleweka na kuheshimiwa. Mfano, kumsomesha mtu katika fani ambayo nchi inaihitaji (siyo inaitaka, manake kuna needs and wants), na wakati huo huo hakuna chuo kinachoweza kutoa huo utaalam katika nchi husika.

Kifuta machozi kwako Mzee Mkira, ni ukweli kuwa mali ya dhuluma uenda kwa dhuluma. Mpango huu ulihusisha makundi matatu 1. Watoto wa masikini waliokuwa wajanja 2. Watoto wa matajiri walioweza kuhonga 3. Watoto wa matabaka ya watawala na viongozi wa mashirika ya Umma. Pia ili ufanikiwe, ilitakiwa uwe na vitu viwili. 1. Fedha ya kuhonga 2. Connection-mtu wa kukupigia kifua. Ni watoto wachache sana wa matabaka ya watawla na viongozi wa mashirika ya Umma walioweza kumaliza shule kwa fedha ya wizi na udanganyifu.

Mtoto wa Sumaye uliye mtaja (ingawa sipendelei majungu), anaangukia kwenye kundi la mali ya dhuluma. Habari za uhakika kutoka Marekani, zinasema kuwa huyu kijana alikuwa katika jimbo la Texas katika shule moja ya weusi inayoitwa Texas Southern University. Aliingia shule muhula mmoja, lakini hakumaliza pia. Miaka yote alikuwa anapiga mzigo na kuzulula mitaani. Ilipokuwa inafika wakati wa ubalozi kutuma fedha kwenda shuleni, alikuwa yuko mstari wa mbele kwenda shule na kudai apewe fedha hizo. Baba yake alikwenda kwenye ziara huko Marekani iliyokuwa inanungunikiwa kwa kutumia mamilioni ya fedha. Alitembelea Texas na kukutana na mwanae. Aligundua kuwa mtoto asomi shule. Mama yake alifunga tena safari nyingine na kumrudisha nyumbani, kabla ya kumpeleka India. Sasa sijuhi ni yuleyule wa India ndiye yuko BOT au ana wawili.

Story hii ni ya mtoto wa Sumaye, lakini inafanana na asilimia zaidi ya 80 ya watoto wa matabaka ya watawala na viongozi wa mshirika ya Umma. Afadhali mtoto wa Sumaye alirudishwa na wazazi. Wengine walikuwa jela na wengine walirudishwa kwa lazima. Bad news hapa ni kwamba fedha ya walipa kodi, au ya mikopo ambayo tunakuja baadae kulipa kwa riba kubwa ilikwisha potea na haikuzaa matunda.

Kumbuka Raisi Kikwete wakati anaaga wizara ya mambo ya nje, aligusia suala zima la kifedha wakati Mkapa anachukuwa madaraka mwaka 1995. Alisema Balozi zetu zote nje zilikuwa hazina fedha na tulikuwa tunadaiwa. akamuomba Mkapa kutumia fedha ambazo Serikali ya Uganda inatulipa kufidia vita ya Nduli Amani (si maajabu hayo-eti waganda wanaopigana kila siku wanatulipa. bajeti yao kwa sasa inajitosheleza, sisi tunategemea wafadhili. Eti tunawazidi amani), hiyo fedha ndiyo ilikwenda kulipia mabalozi yetu.

Nikitumia style ya Raisi wa Iran katika Epistle yake kwa Bush, just an educated guess; Kwa kutumia hotuba ya Kikwete, Mkapa alipoingia madarakani, serikali ilikuwa imechacha kichizi. walikuwa na wanafunzi wengi nje waliokuwa wanawalipia kuzidi uwezo wa fedha walizokuwa nazo. Shule zilikuwa zikiwasumbua ofisi za balozi zetu huko UK na USA. Hali halisi ilipowakumba. Mkapa akaamua kusitisha zoezi zima. Waliokuwa wamepata kumaliza shule, wengi wao walikuwa ni watoto wa maskini lakini wajanja na baadhi ya watoto wa matajiri waliokuwa na connection.

Toka hapo, Serikali yetu ikawa haisomeshi tena watu wake nje kutoka katika mfuko wake. Zilizobaki zilikuwa ni zile za kiushikaji kama za watoto wa wakubwa kweli kweli. Hata hivyo, zikabakia zile unazosikia kwenye magazeti kuwa Serikali ya nchi fulani imetoa Scholarship kadha wa kadhaa ambazo zinapitia Serikalini. Kuna nyingine ni Scholarship za kweli, lakini kuna nyingine ni mikopo. Kama unavyojua masharti ya mikopo, Nchi tajiri kama marekani, wakikupa mkopo lazima ukutokee puani. Wanakuonyesha fedha kwenye karatasi, alafu wanasema lazima watu wako waje kusoma kwenye vyuo vyetu.

Mkiwa na viongozi mliowachagua ninyi, wanapashwa kukataa. Mzee ES anasema kule Marekani weusi si chochote wame sell out. Sasa swali la kujiuliza, ni jicho gani analotumia Bush kumuona mweusi wa Marekani ame sell out, lakini hilo jicho likamuona mweusi ambaye ni Raisi wa Tanzania, haja sell out. Ukweli ni kwamba kwa Bush, mweusi ni mweusi tu uwe Raisi wa Kenya au Jesse Jackson. Thamani yako inapatikana pale anaponufaika na weusi wako. How? ukitaka kupiga picha na Bush, nchi yako inapewa mkopo wa kuwasomesha watu wako, kwa masharti kuwa lazima waje kusoma Marekani ili zile fedha unazoziona kwenye karatasi ziende kunufaisha vyuo vyao.

wanapata faida mara mbili. 1. Vyuo vyao vinapata fedha za kujiendesha. 2. Nchi yao inapata faida kutokana na riba tutakayo lipa. kumsomesha mtu mmoja shule mpaka akamaliza, inaweza ikawa kwa makadilio ya dola elfu 30 mpaka sabini kutokana na kitu anachokuja kusomea (eg. music, what's up man?). Hilo deni la let's dola elfu 40 pamoja na riba yake unaweza kukuta tunailipa dola laki nane na tunafikia sehemu tunasema tumechoka deni halilipiki. Sasa wanakaa na kusema haya tunakusamehe deni, tunaanza kukopa upya.

Kumbuka, hata siku moja hawasemi Serikali imekopa. Serikali imepewa msaada wa dola kadha wa kadha. Mara chache sana inakuwa misaada kweli, lakini wakati wote ni mikopo. Soma magazeti kila siku. Serikali imepata msaada, mara chache watasema serikali imepata mkopo. lakini baada ya miaka kumi, unaambiwa tunadaiwa sana. Sasa hiyo fedha mmekopa lini wakati ilikuwa ni msaada siku zote. Utajaza mwenyewe....

Ndiyo maana kila nikisikia kiongozi yeyote wa nchi ya Kibepari anamsifia Raisi yeyote wa nchi masikini nasikia moyo unaniuma. Hotuba ya kiongozi wa nchi tajiri lazima uilipie gharama. Ilikuwa tofauti wakati wa vita baridi kati ya Urusi na Marekani. Wakati ule walitaka wawasomeshe bure ili muwe mapepari. Sasa hivi noma, yaani ni choo kijizi. Nashangaa kwa nini viongozi wetu hawaendi China, Russia, India, Turkey, hawa jamaa wanawasomesha vijana wetu bure kabisa bila masharti ya kukopeshwa. huu ndiyo uzalendo. Mzalendo ni yule anayekutakia mema. Japan imekuwa nayo ikitusaidia kwa elimu lakini vijana wetu wengi wanasomeshwa mambo ya vidudu dudu fulani vinatembea na kufanya kazi kama binadamu, sijuhi vinaitwa Robots au robotics (whatever). Sasa hapa Manzese kwa mfuga mbwa havitusaidii, labda kwa kutafuta ajira huko majuu na wakamwaga mapesa nyumbani ili na sisi tufungue baa za kuwanywesha ndugu zao. Lakini kuna Electronics etc.

Unyama wa Ubepari hauishii hapo. Mara nyingi, wanakuambia masharti ya mkopo huo wa shule, ukimaliza lazima urudi nyumbani. Kwa kisingizio cha kusaidia nchi yako. Ukweli ni kuwa hawataki ufanye kazi na upate fedha za kurudisha nyumbani. wanataka mbaki maskini tu. Wao wanataka fedha iingie tu. Ndiyo maana nawasifu sana vijana wa kijiweni hapa kwetu Manzese waliokuwa wanachonga Bank statement na kupeleka ubalozini. Maafisa wa ubalozi walikuwa wakihesabu zile Bank statements na kusherehekea kuwa wanaliingizia taifa lao fedha, kumbe zile ni fedha zinazotoka kwenye taifa lao kuja nyumbani Tanzania.

Hawa vijana ni majemedari na wzalendo wa kweli kuliko matabaka ya watawala yanayotuingizia kwenye mikataba ya kihuni kama hii. Hawa vijana wanatuma fedha nyumbani kwa kupitia Western union. Ingawa muhusika anapewa fedha ya madafu, lakini Serikali inapata dola bwana. Fedha ndogondogo wanazotuma watanzania zinaliingizia taifa pato la fedha za kigeni. Tukifanya utafiti, unaweza kukuta hizi fedha zinachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la taifa na bajeti ya nchi. Si hilo tu, wanajenga vibanda majumbani kwao kutokana na kupigika na schedule, hivyo kutoa viajira vidogo vidogo. Wanasomesha ndugu zao. wanawatunza wazazi wao.

Wazazi na ndugu zao wkitumiwa fedha, wanakwenda kununua vitu na kusababisha mzunguko wa fedha nchini kwetu. ukichunguza kwa makini, utagundua kuwa vijana wanao fanya hivyo, ni wale waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na sita. Hawa wangekuwa na sisi hapa kwa mfuga mbwa, wangekuwa wameliwa na funza. Ukijumlisha hawa vijana duniani kote waliko, na ukajumlisha vijifedha wanavyotuma na viajila vidogovidogo wanavyotoa, kwa ujumla wao, utakuta wanatoa ajira kwa watu wetu kuzidi serikali za mikoa mitatu au minne ya hapa nyumbani inavyotoa ajira kwa watu wake.

Bahati mbaya, wasomi wetu wanasubiri fedha za wafadhili ili waweze kufanya utafiti. na sisi ambao hatujaenda shule, tunatumia busara za wahenga ili kutambua umuhimu wa hawa vijana. Ili swala nimeliingiza kwenye mada hii ya Jamal kwa sababu linahusu uzalendo na asili ya mtu. Hawa ndiyo wazalendo kweli kweli (siongelei wale wanaoiba vile vidubwasha vya computer). Hakika tungejua kwa utafiti umuhimu wa hawa vijana kwa taifa letu, tungewapa hata hizo wanazolilia sijuhi dual nini tena? ehe, manake wape uhuru wa kufanya biashara, kuingia na kutoka nchini, kuwekeza katika nchi yao wakati wana uraia wa nchi nyingine ili wasije wakalipishwa kodi kubwa kama wageni (by the way kuna tax holidays; so who cares anyway?). Hawa ndiyo wawekezaji wa kweli. Nikama wachezaji wa timu za kulipwa walioko nje, na mara kwa mara wanarudi kulisaidia taifa lao wanapotakiwa.

Mimi naona tungewapa msaada wote wanaohitaji ili kuendeleza taifa letu. Labda nisiwe Naive kama alivyonishauri Mzee ES kwa sababu upande mwingine wa shilingi kuna madhala ya hiyo Dual thing. Uzalendo usiniponze.
 
Mzee ES

Karibu kwanza kwa mfuga mbwa tupate ile ya kupandisha mabega kidogo. Shukurani kwa shule yako na ushauri kwangu. Maelezo uliyoyatoa, hoja zangu za mwanzo zinayapinga. Busara zinanituma nisijirudie rudie. Mimi nabaki na msimamo wangu kwa sababu sijaona sehemu ulipozibomoa hoja zangu.

Nikusihihishe kidogo mzee, just trying to make records straight (ung'eng'e nao unanipiga chenga kidogo). Mkapa alipokwenda kutangaza nia yake ya kugombea uraisi pale katika ukumbi wa jengo la sayansi na elimu ya juu kwa wakati ule 1995, aliandamana na Jenerari Ulimwengu pamoja na Warioba na siyo Salim. Mkapa alikaa katikati, Ulimwengu upande wa kushoto wa Mkapa na Warioba upande wa kulia wa Mkapa. Tembelea ITV kama wana kumbukumbu za mikanda yao. Pia kumbuka kipindi kile Salim alikuwa Ethiopia. Hata vijana wa CCM ambao hawakutaka kujulikana, walitangaza rasmi safari ya kwenda kumuomba aje kugombea Uraisi na kweli walikwenda na wakarudi kapa kwasababu alikataa.

Mwalimu alipokuwa anahutubia katika hotel ya Kilimanjaro 1995, aliyatoa matatizo yaliyokuwa yanaikabili nchi yetu kwa jinsi alivyo yaona yeye. Akasema mgombea lazima awe na sifa za kukabiliana na yale aliyoyaona. Katika vichekesho vyake pale, aliwashauri CCM kuacha mizengwe ya kumpata mgombea uraisi. Alisema mizengwe ilikuwa inasaidia nyuma lakini siyo sasa. Alisema vingozi wazuri wapo CCM lakini wanachukiwa na wala rushwa. Mzee ES labda niishie hapo. Aliyekuwa anaongea ni kinara wa mizengwe. Unafikiri mizengwe imeisha CCM? Unafikiri pia kuwa viongozi wazuri hawachukiwa na wala rushwa? Je unakubaliana na utafiti wangu wa kwa mfuga mbwa kuwa asilimia kubwa ya viongozi wa CCM ni wala rushwa?

Sikubaliani na wewe kuwa hakuna nchi yoyote, inayoweza kusema waziwazi kuwa hatumchagui mtu huyu kwa sababu ya uarabu, utusi, uhutu, uhaya, uchaga, ugogo, au ukuja, wake. wabaguzi muda wote huwa wana underestamate madhala ya ubaguzi. Sometimes it gets real nusty out there! hivi unafikiri makaburu wa afrika kusini walikuwa wanaona haya kusema nyani hawezi kuwa Raisi? Rwanda je? kwani kisa cha kuwamua kuwafyeka kilikuwa nini? ni kwamba mtusi hawezi kutuongoza. haikuwa jando hiyo walikuwa wanasema redioni. Mtu anayekuita mende atashindwa kukwambia kuwa si kuchagui kwa sababu wewe ni mende?

Marekani je? hivi walipokuwa wanasema 3 equals 1, unafikiri walikuwa wanaona haya. Katiba ya marekani huwa hawafanyi amendments kijinga jinga. You can count how many times. Not over 18 times in over 200yrs of independence!. Mojawapo ya amendments kati ya hizo 17, 18 or so; ilikuwa kuhararisha mtu mweusi kuwa ni mtu anayeweweza kupiga kura. Wewe unasema kutamka wazi, it was in the constitution. Tena hawa nasikia fedha zao zimeandikwa GOD ambaye ameumba watu wote. It is nasty my friends.

Umesahau India juzijuzi tu? Yule mwanadada anagombea uwaziri mkuu, wanamwambia hatukuchagui kwasababu ya asilia yako ya Uingereza. Wanaompinga wanasema waziwazi kwenye vyombo vya habari. lakini kama nilivyosema, hizi nchi zimeendelea sana, watu wengi wanaona mbele zaidi ya chuki za watu binafsi. Walimchagua. Sisi kwa sababu tunaanza anza mambo ya kibaguzi ndo tunaoneana haya. Hawa viongozi wanaonunua uongozi kwa kura, alafu wanawapaka matope wenzao kwa kueneza chuki. Tuchukulie mfano, Salim ni mgombea wa Chadema na Kikwete CCM, Salim ana wafuasi kama mimi tusioamini mambo ya ubaguzi na wale waliompigia kura CCM, na Kikwete na Mzee ES. Mfano polls zetu zinasema Kikwete na Salim ngoma sawa 45% to 43% may be with marginal of error etc. Jinsi alivyokuwa anautaka Uraisi, kikwete will go nusty. Hapo hakuna haya tena, ni kama mfa maji.

Kibaya zaidi, mimi na wewe ndiyo tutaanza kuzipiga mtaani. Wao wanalindwa. Ndiyo maana nasema tusinunue chuki zao. Sisi inabidi tuwe tunajadiliana jinsi ya kuwakabili wote wawili badala ya kupanda mbegu za kuja kushikana. Ubaguzi ni sawa na mtu mwenye ugonjwa wa kuhara. Huwezi kuwa na control ya vile vijidubwasha vinavyo ruhusu kinyesi kipite au la! unaweza kukuta umeharisha mbele za watu bila wewe mwenyewe kupenda.

Labda mzee swali la mwisho kwa wewe anayezijua siasa za hapa bongo, unasema hawawezi kutamka waziwazi kuwa tunakukataa kwa sababu ya uarabu, je wanaweza kutamka hadharani kuwa tunakukataa kwa sababu sisi ni wala rushwa? utatuweka ndani baba sisi hatukutaki, tunataka mtu atakaye tutunzia siri zetu ili tuweze kujisitiri. Hayo maneno unaweza kuyasikia Redioni? je siyo kweli kwamba wanahitaji mtu wa kuwatunza?

Yaani nani anaanza kusema huyu mwarabu, kwa hiyo? Mfano Mkapa anasema je? ndani ya moyo wake kabisa achana na mambo ya wazi. Kwamba huyu Salim ni Mwarabu na nitahakikisha hapati uraisi? Kwa nini? kwasababu uarabu utafanya nini? atauza nchi siyo? Huyo ni Mkapa anasema kimomomoyo kabla ya kuingia Kimwaga. Atauza nchi? dhamili ya Mkapa itampinga pale pale. Itamwambia Atauza nchi kama wewe ulivyofanya? Sasa kinachokuuma nini nini? Unatetea maslahi ya nani?

If you can't think, you will never ask questions! ili tuweze kuwauliza maswali hawa waheshimiwa, inabidi tuwe tunajiuliza maswali wenyewe. Hivi ndivyo tutaikomboa nchi. Naamini mijadala ya kwenye mtandao itakuwa ni mwanzo wa ukombozi wa nchi za Afrika.


Kuhusu Powel, data zako naona bado hazina uhakika. Ile hanging chad na recount x10 ya Florida ilikuja baada ya uchaguzi, yaani baada ya kupiga kura. Bush alikuwa anamuhitaji Powel kwenye kampeni za uchaguzi. Wala hata hakwenda Florida. Florida walikuwepo mafia hakina James Baker.

Nikimalizia kwa Mkira. Internet inavyoonekana italeta mapinduzi pale nyumbani. Lakini tuache porojo, chuki, na soga. Tuwe tunashusha nondo kweli kweli kama za mzee ES. Haya majadiliano tunayoyafanya yanawanyima usingizi watawala wetu. Watanzania hatuna utamaduni wa kujisomea vitabu. Angalau internet, nikienda kuchungulia pornography kwenye cafe pale mapipa, napata muda wa kufungua e-mail yangu pia na hata kuchart kwenye hizi forum. Hii inasaidia kuwavutia watu kusoma. Maandishi ni maandishi tu. Hata yawe kwenye kioo. Si unakumbuka wakina Tomas Paine walivyo mkimbiza mkoloni huko Marekani kwa barua zilizoitwa epistle. Uzuri ni kuwa na viongozi wetu hawapendi au hawana tabia ya kujishughulisha na kupekuwa vitabu. Hii tecknolojia ya computer inawapiga chenga. Tutakuwa tunawaletea mavitus mpaka waseme hawa vijana wamelogwa nini? labda wavifunge vicafe vyote.

Si umeona majuzi tu majadiliano ya uhakika ya vihiyo Bungeni na kwenye baraza la mawaziri yalivyo leta matumaini. Sitta karopoka juzi kuwa wanataarifa za vihiyo. Yeye anasema siyo wengi lakini ni wengi. Hii mijadala inatakiwa iwe mikubwa sana na tuwaweke viongozi wetu kwenye miamba ya Kaya mashapo. Wataachia ngazi wenyewe.
 
Kyoma,
Mwenzetu mwana historia hasaaa!. Tunakuhitaji sana na wala usije tuacha ktk mataa. Swali moja tu, mbona lugha yako na Mzee Es zinafanana sana?.....utafikiri pacha! Au ndio yule Meagainstkikwete na baadaye Sam.
 
Back
Top Bottom