Ally Kessy awashukia Zanzibar, Awataka Wabunge wa Zanzibar watoke nje kwa mambo yasiyo ya Muungano

Nakumbuka aliwahi kusema kwamba unaweza kuwaita wazanzibari wote kwa filimbi na wakasikia.
Kaka daa! Nimeecheka mbavu sina.Ina maana zanzibar nzima ni kama jkt mgulani? Maana hata Lugalo ukipuliza filimbi huenda askari wengine wasifike kwani filimbi yako haitasikika.
 
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazowahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Njia pekee ya kuondoa muingilio wa Wazanzibar kwenye masuala yasiyowahusu ni katiba mpya kama ilivyokuwa imeratibiwa na team ya Judge Warioba!.

Mengine haya ni mbwembwe tu na matumizi mabaya ya muda wa bunge. Huyu kessy mimi namwitaga Kessy Popo.
 
kiikwwli sioni mdingi wa hoja wa maneno yake zaidi ya kujaza chuki na hoja hii sio yake yy ametumika kipaza sauti tu ni hoja ya upinzani,swala hili ni mfumo tuliojiwekea toka enzi nna dahari hizi ni kauli za kichochezi ktk taifa letu (Chuo cha Amani)sikubaliani nae hata kidogo ni mchochezi
 
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazowahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Tatizo ni watanzania wenyewe, kweli mtanzania mwenye akili timamu aliamka asubuhi kuchagua mbunge kama huyu? walipewa hundi ya kununua Benzi wakanunua bodaboda na wanataka kuendesha bodaboda kama Benzi.
 
Kwenye bunge la katiba alisema anataka serikali tatu, ila wazanzibari muache unafiki mnajua wazi huu muungano unatetewa nakulindwa kwa jinsi ulivyo na CCM, inakuwaje kwenye uchaguzi kwa wingi wenu hamuipigi chini ikose majority?
Wapige chini mara wakati CUF ilishinda wakaporwa.
 
Zanzibar ni koloni la tanganyika, ukweli wanasimagwa.
Ni sawa na mtu akupe chakula, alafu akusimange
 
Katiba yenye rasimu ya Warioba hawaitaki,Zanzibar wanapandikiza mtu wao wanaona sawa.Huyu Kessy aache unafiki.Maana ni unafiki kama wa Tulia na kamati yake ya maadili.Mlevi aliyeingia bungeni kautwika hajadiliwi na kamati ya maadili.

Eti mtu aliyeomba moongozo ameleta fujo.Tulia hivi ana mme? je mme gani anashindwa kumshauri mkewe?
 
Kilichonitisha sana sio michango ya Kessy bali ni Idadi kubwa ya wabunge waliokuwa wakigonga meza na kushangilia.....kuna jambo kubwa hapa..
 
Dawa ya yote haya ilikuwa kwenye katiba ya Warioba. Wakaisigina, sasa wanakaza mishipa ya Shingo bure tuu.
 
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazowahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Kwa kweli Kessy ameeleza ukweli lakini amekosea kuwataka Wabunge wa Zanzibar kutoka kwenye Bunge la Jamhuri ya Tanzania. Jambo lililo sahihi hapa ni kwa Wabunge wa Tanganyika kutoka kwenye Bunge la Muungano na kwenda kutafuta Bunge la Tanganyika.

Kessy na wenzake waende wakaunde Bunge la Tanganyika kwani mambo yao kuzungumzwa kwenye Bunge la Tanzania si sahihi.
Kwa mwenye akili angeliona hili lakini watu kama Kessy hawana akili.
 
Mi sikuwahi kuwapenda wabunge wanaotokana na CCM kwa kuwa huwa hawajui kujenga hoja za maana zaidi ya kusubiri kuunga mkono hoja kwa kuegemea Chama chao kana kwamba Serikali inatumia mfumo wa kibunge (parliamentary system). Hata hivyo nimekuwa nikiliwazwa mara kwa mara kwa uropokaji mzuri wa Mbunge Kessy hasa dhidi 'ego' za wazanzibar ambao wanajidai wanataka uhuru baada ya kugunfua kuwa wana rasilimali ya mafuta. Go bhana Kessy utupe raha hata kidogo mana hatuwezi kuipata kwa wanaccm wenzako.
Nafikiri akili ingekuambia kuwa asiekuwepo ndie anahitaji kuwepo, Bunge la Tanganyika ni lipi?
 
Awataka wabunge wa Zanzibar kuanzia sasa wachangie Wizara zinazowahusu, Awataka wawe wanatoka nje pale bunge linapojadili mambo yasiyo ya Muungano, sio wanatujazia foleni ya kuongea hata kwa mambo yasio ya Muungano.

Ally Kessy Mbunge wa Nkasi, amesema Wazanzibar waache kuwanyonya Watanganyika. Ameyasema hayo wakati wa kuchangia Wizara ya mambo ya Nje.

Amesema Wabunge kutoka Zanzibar wapo zaidi ya 54, wangekaa kule kwao hata Bunge lao lingeonekana dogo, wasingepata pa kukaa, hivyo wanapokuja wawe wapole.

Amedai wabunge wa Zanzibar wanataka haki sawa katika Uteuzi wa Mabalozi wakati Mabalozi wenyewe ni 21 tu. Kasema kwa kuwa Zanzibar inachangia Asilimia 4, hivyo na mabalozi inabidi wawe asilimia nne. Hata kama wapo Manaibu Balozi wamependelewa tu.

Huyu kaongea yale yaliyotakiwa wayaongee wapinzani na wa chama cha CCM na hususani kutoka Zanzibar

Na nimefurahi sana kwa kuwasemea maana wabunge wa CCM from Zanzibar wanaogopa kuyaongelea hayo maana wakifanya hivyo wanaogopa kutopata Uwaziri au kutengwa

Hata hivo suala la kusema kua ati mabalozi znz wasipate sawa na watangayika sio point na kama ni hivo tuu, maana Karume alipokubali Muungano huu na Nyerere hawakusema kua hii nchi ni ndogo na ipate mahitaji madogo hapo tunataka usawa uwepo baina ya nchi hizi mbili

Tunataka raha ya muungano wa nchi zoteeeeeee
 
ni lini Zanzibar walisema wanataka Muungano na Watanganyika ?
nashangaa Nyerere alivyokimbilia Zanzibar kufunga mkataba wa Muungano..
Mmesahau mlivyokua mkiingia Zanzibar kununua bidhaa ?
sasahivi hela za bandari ya Zanzibar mkusanye nyinyi, utalii mkusanye nyinyi, foreign exchange kutoka Zanzibar mkusanye nyinyi , misaada ya UN, FIFA iishie kwenu..
makusanyo hayo kutoka Zanzibar mnaingiza kwenye mfuko wa Muungano kuendesha miradi ya bara na Zanzibar kuambulia mazombie ya askari kutoka bara ili kuwadhibiti...
mmeizuia Zanzibar hata kujiunga na OIC ili isinufaike..
MBONA HAMUITISHI REFERENDUM ili Wazanzibar waamue kama wana hata shauku ya kuungana na machogo.

Kwa jina la Id na mchango wako wewe ni muhusika muhimu kwa huu muungano.

Kama kweli tunaupenda huu muungano, basi tuufanye kama mboni ya jicho letu au kioo cha miwani tuitumiayo kwa kuoneana kusomea. Tukisha uona huu muungano katika hali hizo nilizozitaja, basi hatuwezi kutumia msasa au tindikali. Tindikali haifai kusafishia jicho wala msasa kusafishia kioo cha miwani.
Maneno yako na baadhi ya wazanzibari wabunge na ya Mh Kessy kwa namna yanavyowasilishwa kwa umma ni kama tindikali na msasa kwa huu muungano.

Jirekebisheni namna ya kuziongelea hizi changamoto za muungano. Moja ya misamiati inayoleta hisia mbaya ni maneno UNYONYAJI, DHURUMU, ONEA. Iwapo tutaacha kutumia maneno haya na mengine yatakayo pana maana hasi dhidi ya pande moja ya muungano utajenga hisia mbaya ambayo huenda haikukusudiwa.

Basi ukitaka kuongelea swala la muungano jaribu kutokuwa na hisia kali au jaziba.
Tuulinde Muungano Wetu. Ng'ombe huenda haoni thamani ya mkia wake kwa sababu upo.
 
Hakuna shida. Wakiongelea ambayo sio ya muungano wote watoke. Kwani hili bunge la muungano na la tanganyika halipo wakawa wanaongea ya tanganyika pekee yao.

Kwanza tafuteni bunge la tanganyika mlipate....Kwa sasa halipo na tanganyika haichangii kitu ..fedha hizi ni za muungano hivyo tutabanana tu..hamtaki tuacheni tumu mue
 
Hiyo ni kweli unaweza kuzunguka kwa baiskeli isipokuwa utatumia muda mrefu, mimi na rafiki yangu tulizunguka zanzibar yote kwa gari tulitumia saa mbili na robo tukamalizia kwenda Tumbatu na boti
Mkuu Pemba mliendaje?
 
Quick response. Usitumie fallacy kumtafakali Ally Kessy. Bettry ya simu ikiwa mbovu nunua mpya weka kwenye simu.

And what exactly do you mean? Kwamba maCCM waliikataa rasimu ya Katiba iliyotokana na Tume ya Jaji Warioba is fallacy? What is fallacy?
 
Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ally Keissy amechafua hali ya hewa Bungeni baada ya kujadili hoja kuhusu Muungano, akiwataka wabunge wa Zanzibar kutojilinganisha na wa bara jambo lililozua mjadala lakini baada ye likawekwa sawa na Waziri January Makamba
 
Back
Top Bottom