Tetesi: Alliance Schools yalazimisha watoto kuchanga Tzs100,000 ili kushiriki mahafali 2019/viongozi mlikane hili

Tutaona Namna Nzuri Sana Ya Kulifuatilia Yaani Watu Wanavuna Pesa Bila Shaka Uelekeo December
 
Muda sio mrefu tutakuja ona uzi hapa ukisema "kikao cha harusi kimepitisha mchango wa sh. 100,000/- kama minimum ya kupewa card hivyo tunaiomba serikali iingilie kati"! Uzuri imeshatamkwa kwamba mwenye chake auze kwa bei atakayo!
 
Wanafunzi waliomaliza mitihani yao kidato cha nne Alliance Schools zaidi ya 200, wanatakiwa kuchanga 100,000/-TZS ili kushiriki mahafali ya kidato cha nne 2019. Iwapo kila mwanafunzi atatoa pesa hiyo ni zaidi ya 20,000,000/- Milioni Ishirini,

Mchango huo utahusisha mwanafunzi husika na wazazi wake wawili tu, yaani watu watatu (3).

Ili kuweza kuhusisha wadogo ama wakubwa wa mwanafuzi, yaani watoto wenziwe kwenye famila inabidi kila mtu anayezidi atoke 10,000/-TZS ili kuweza kuingia ndani ya ukumbi wa mahafali, kama huna ni kubaki nje na wanafamilia hawa washindwe kushudia mdogo ama mkubwa wao akitunukiwa cheti.

Yaani imekuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu maana laki moja kwa mahafali ambayo ni wajibu wa shule kwa wahitimu ni changamoto. Watu 3 wakati kiserikali familia ina watu 6. na ni ukweli hapa TZ kuna wajomba shangazi na watoto wao, mara zote kwenye sherehe kama hivi tunashirikishana, iweje bibi au babu kumuona mjukuu wake akihitimu form 4 alazimishwe kulipa TZS 10,000/-? inafahamika kula kwenye mahafali haiwezekani ndugu wote wa wahitimu wakala ama kwa ukweli kuwa itabidi chakula kiwe kingi sana ambacho lazima kitapoteza ubora wake, ama mtu tu hapendi kula nje ya chakula cha familia yake mwenyewe, kwa maana kwenye mahafali kula sio lazima, iweje ulazimishe mtu anayekuja kwenye mahafali ya ndugu yake atoe 10,000 eti lazima ale? unauhakika chakula unachoandaa kinakidhi mahitaji ya kila mshiriki? ya kiafya ya kijamii ya kidini etc?

Tunaomba Viongozi hasa Mkoa maana Rais naye anakazi nyingi na nyinyi ndio wasaidizi wake muingilike kati maana sio haki, kwa vile watoto ni haki yao kufanya na kuhudhuria mahafali isitumike kujipatia pesa kama kitapeli vile maana wazazi wangependa watoto wao washiriki. Ada wazazi walikwisha lipa zote, ni haki ya watoto kufanyiwa mahafali na shule. Hata kama kungekukwa na mchango basi 10,000TZS kwa mtoto. Suala la kula ni la watoto sio wazazi na familia yote maana nyumbani pia watakuwa wameandaa vyakula.

Wazazi na watoto wananyanyasika vile huwezi hitimu alliance ukafanyia mahafali Omega mfano tu.

Kama anaona lazima kuwanyonya wazazi na wahitimu basi agawe vyeti watoto warudi majumbani kwao kula na kunywa, lakni asinyime watoto na ndugu zao haki ya kushiriki mahafali kwa kisingizio cha kuwapa chakula kwa bei ya juu kupita maelezo, chakula ambacho sio lazima wote wanakihitaji na wengine hawataweza kukikutmia kwa sababu za kiafya

Asante kwa msaada wa wenu viongozi serikali-Mwanza
Acha kulia lia mkuu
Mtoto wako mlete mashenzini secondary school.
Huko kama haumudu acha kujikakamua utakuja kutoa ushuzi mbele za wakubwa.
 
Nakupa ushauri,pindi utapokuwa na familia yako au kama unayo tayari..uwe unashiriki mahafali na usijetumia nafasi yako ya kutokufanya sherehe kuwanyima jamaa au watoto wako haki ya kushereheka na kihitimu kuna furaha uliikosa au waliikosa ndugu na jamaa zako.Pia kuna taarifa wahudhuriaji huzipata na kujifunza bila kusahau Baraka ya kujumuika pamoja.
Thank God shule wanayosoma hakuna graduation wala mtihani wa darasa la saba. Mwakani September first born anaingia form one. Kutakuwa na mtihani wa kumaliza O lever ila hakuna graduation.
 
Yaani mimi kusema ukweli nilijiuliza sana umuhimu wa wazazi kwenda kwenye graduation. Mimi O level,A level yaani hakuna ndugu yangu alokuja kwenye graduation. Na niliona poa tu. University ndo kabisa hata kwenye graduation sikwenda maana nilikuwa kazini tayari. Yaani mimi sherehe wala huwa sioni kabisa umuhimu wake.
Mimi nimesoma shule zote sijawahi hata kuvaa joho tu.
Mpaka degree ya pili sikuvaa hilo joho nadhani hata PhD sitovaa
Yaani nikupe hela ya maafali wakati ada yenyewe nadunduliza?
 
Mimi PhD yangu nilidefend then nikamaliza. Hakuna cha joho wala nini. Inshort sijawahi vaa joho and iam OK with that. Mimi hujali vitu vya msingi tu.
 
Shuke nyingi za private hiyo ndio gharama ya graduation. Kama wazazi wameridhia hamna shida.
 
hujaelewa, uhudhurie usihudhurie Laki unatoa ndio ilivyo; sio tu laki ni kubwa bali ni lazima. nadhani umeelewa. na kwa vile mahafali inafanyika wiki 2 baada ya mtihani watoto wengine walikwisha safari kwenda Rukwa, Mbeya Kuja Dar Tabora etc lakni ama warudi kwa gharama zao ama wasirudi kwa hofu ya gharama laki lazima atoe wakati wa kuchukua cheti. Umeleewa???
Kama huudhurii unatoa ya nini? Na usipotoa watakufanya nini? Hili jambo siyo la kuja kulalamika hapa bali inabidi wazazi wenyewe waseme wazi kuwa hizo fedha ni nyingi na hatuwezi kutoa. Vinginevyo kama mna ile tabia ya nyumbu, ya kutokuwa na msimamo na kuogopa kuchekwa basi toeni. Ingekuwa mimi siku ya graduation namchukuwa mwanangu nampeleka mbuga za wanyama au shemu nyingine yoyote ya maana. u namfanyia sherehe nyumbani. Ni bora utumie fedha nyingi kwa utashi wako kuliko kulazimishwa kutoa fedha au kutoa kwa kufuata mkumbo.
 
Wanafunzi waliomaliza mitihani yao kidato cha nne Alliance Schools zaidi ya 200, wanatakiwa kuchanga 100,000/-TZS ili kushiriki mahafali ya kidato cha nne 2019. Iwapo kila mwanafunzi atatoa pesa hiyo ni zaidi ya 20,000,000/- Milioni Ishirini,

Mchango huo utahusisha mwanafunzi husika na wazazi wake wawili tu, yaani watu watatu (3).

Ili kuweza kuhusisha wadogo ama wakubwa wa mwanafuzi, yaani watoto wenziwe kwenye famila inabidi kila mtu anayezidi atoke 10,000/-TZS ili kuweza kuingia ndani ya ukumbi wa mahafali, kama huna ni kubaki nje na wanafamilia hawa washindwe kushudia mdogo ama mkubwa wao akitunukiwa cheti.

Yaani imekuwa kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu maana laki moja kwa mahafali ambayo ni wajibu wa shule kwa wahitimu ni changamoto. Watu 3 wakati kiserikali familia ina watu 6. na ni ukweli hapa TZ kuna wajomba shangazi na watoto wao, mara zote kwenye sherehe kama hivi tunashirikishana, iweje bibi au babu kumuona mjukuu wake akihitimu form 4 alazimishwe kulipa TZS 10,000/-? inafahamika kula kwenye mahafali haiwezekani ndugu wote wa wahitimu wakala ama kwa ukweli kuwa itabidi chakula kiwe kingi sana ambacho lazima kitapoteza ubora wake, ama mtu tu hapendi kula nje ya chakula cha familia yake mwenyewe, kwa maana kwenye mahafali kula sio lazima, iweje ulazimishe mtu anayekuja kwenye mahafali ya ndugu yake atoe 10,000 eti lazima ale? unauhakika chakula unachoandaa kinakidhi mahitaji ya kila mshiriki? ya kiafya ya kijamii ya kidini etc?

Tunaomba Viongozi hasa Mkoa maana Rais naye anakazi nyingi na nyinyi ndio wasaidizi wake muingilike kati maana sio haki, kwa vile watoto ni haki yao kufanya na kuhudhuria mahafali isitumike kujipatia pesa kama kitapeli vile maana wazazi wangependa watoto wao washiriki. Ada wazazi walikwisha lipa zote, ni haki ya watoto kufanyiwa mahafali na shule. Hata kama kungekukwa na mchango basi 10,000TZS kwa mtoto. Suala la kula ni la watoto sio wazazi na familia yote maana nyumbani pia watakuwa wameandaa vyakula.

Wazazi na watoto wananyanyasika vile huwezi hitimu alliance ukafanyia mahafali Omega mfano tu.

Kama anaona lazima kuwanyonya wazazi na wahitimu basi agawe vyeti watoto warudi majumbani kwao kula na kunywa, lakni asinyime watoto na ndugu zao haki ya kushiriki mahafali kwa kisingizio cha kuwapa chakula kwa bei ya juu kupita maelezo, chakula ambacho sio lazima wote wanakihitaji na wengine hawataweza kukikutmia kwa sababu za kiafya

Asante kwa msaada wa wenu viongozi serikali-Mwanza
Millioni 200.
Mapambo.....
Vinywaji.....
Muziki.....
Chakula.....
Zawadi...... (wanafunzi na walimu)
Ukumbi....
Kodi......
Faida....?
Linganisha 100,000/= na ada ya 2.5Mln + kwa Mwaka.
Kwa ufupi kama uliweza kuwekeza zaidi ya 15Million kwa miaka minne,100k ya graduation sio issue.
100,000/3= 33,000/= per head.(baba,mama,mtoto) ni reasonable wrt to ada ya shule.
 
mrejesho tu ni kuwa serikali ilitia timu siku hiyo kuona hayo malipo ya 10,000 kwa kila kichwa kuanzia mtu wa 3 kuendelea maana baba na mama (watu 2)tu ndio waliruhusiwa kwa ile laki. Waliufyata in summary na watu kuserebuka; hela ipo ila kuibiwa hatupendagi ujinga aiseee

Tunaandika hapa sio kwa ajili ya vidampa kuongea upuuzi wao, tunakua serikali ipo hadi hapa. HONGERA SERIKALI

Na ni ujinga kudhani mtu akilalamika eti hana hela ya kutosha, mistaken view of poor Tanzanians;

Asanteni

Muda sio mrefu tutakuja ona uzi hapa ukisema "kikao cha harusi kimepitisha mchango wa sh. 100,000/- kama minimum ya kupewa card hivyo tunaiomba serikali iingilie kati"! Uzuri imeshatamkwa kwamba mwenye chake auze kwa bei atakayo!
 
Yaani mimi kusema ukweli nilijiuliza sana umuhimu wa wazazi kwenda kwenye graduation. Mimi O level,A level yaani hakuna ndugu yangu alokuja kwenye graduation. Na niliona poa tu. University ndo kabisa hata kwenye graduation sikwenda maana nilikuwa kazini tayari. Yaani mimi sherehe wala huwa sioni kabisa umuhimu wake.
Ulifanya vyema,
 
Back
Top Bottom